Muda mwingine jaribu kufikiri nje ya siasa, nilichoandika mimi kinahusiana nini na maswala ya siasa? Umegusia Zambia na Malawi walitakia watumie bandari ya Bagamoyo, lakini wachina wamekimbilia Kenya kwasababu sisi tumeleta siasa. First of all, mizigo ya Zambia na Malawi isinge pita Bagamoyo na wala haitakuja kupita Bagamoyo. Bandari ya Bagamoyo ilikuwa na maudhui yake tofauti na unavyo fikiria wewe.
Swala la Zanzibar kuwa bandari huru, ni swala lililo jichanganya na mambo ya muungano, kwamba kama Zanzibar ikiwa bandari huru, itachagia vipi kuzorotesha mapato ya bara. Malumbano yameenda nyuma mbele mpaka Kikwete na Sheni wakakubaliana jinsi ya kutatua tatizo zima pamoja na swala la mafuta ya Zanzibar.
Nashangaa unasema eti bandari ya Tanga haitaingiza kipato kikubwa kutokokana na mafuta ya Uganda. If that's the case kwanini wakenya wameumia sana kuukosa mradi huo? Mafuta, sisal, perishable goods, industrial goods yote hiyo unaona hakuna kipato. Mbona hujaongelea bandari ya
mbayo itakuwa na reli yake mpaka ziwa Nyasa na kuudumia mizigo ya Malawi mpaka Zimbabwe.
Kinacho kuumiza hapa ni sisi kutokuchangamkia fursa za wachina. Umeshindwa kuchambuwa kwanini tumekuwa tunavuta mguu na swala la uwekezaji wa wachina. Imani yako ni kuwa wachina ni watu wakufanya vitu haraka haraka, lakini haujiulizi hiyo haraka inakuja kwa gharama gani?. Mchina anakupa mradi haraka haraka lakini gharama yake ni Mara tatu kuliko gharama halisi na hakuna uhakika kama huo mkopo utaweza kuilipa. Tunamiradi mingi na wachina lakini sio kila mradi lazima tuseme "ndio mzee"
Soma kwa makini mrejesho huu hapa chini upate mawili matatu.
Kenyans carry the burden of China's high cost loans
We jamaa una kichwa kizito kishenzi kuelewa!!! Hivi umeambiwa mizigo ya Zambia na Malawi au umeambiwa Wachina wana projects za bandari sehemu kadhaa Afrika kwa ajili ya ku-facilitate biashara zao?!
Hebu rudia kusoma hapa:
Hapa umeambiwa miradi ya China barani Afrika! Kwa wanaofuatilia masuala ya marine transportation wanafahamu what's going on.
China ni kama wameigawa Afrika into blocks ili kurahisisha biashara zao... hakuna aliyetaja habari ya shaba ya Zambia hapa wala magogo ya DRC!!!
Halafu pamoja na kueleweshwa; bado unarudia tena jambo lile lile... mara oh, Malawi na Zambia hawawezi kupitishia mizigo Bagamoyo!!
Halafu ona hilo la Tanga!! Umeambiwa bandari ya Tanga haiwezi kuchangia mapato au umeambiwa suala la bomba la mafuta kupita Tanga lilikuja by chance baada ya Total kushituka dakika za mwisho kutumia Mombasa? Again, soma tena hapa kwa vituo:
Mradi wa bomba la mafuta Tanga umekuja by chance baada ya Total kushituka dakika za mwisho kutumia bandari ya Mombasa!!!
Miradi ya Tanga ambayo ipo au ilikuwa kwenye pipeline ni mradi wa deep sea port na Mwambani port... mmoja ni mradi wa TPA na mwingine ni mradi wa VIP Engineering under Mwambani Port & Railway Corridor Company!!!
Huo mradi wa bomba la mafuta utakuwa na impact ndogo sana katika ujenzi wa bandari... zaidi tu ya kupanua miundombinu ya hapa na pale.
Wapi nimezungumzia suala la bandari ya Tanga kuingiza kipato kidogo au kikubwa?
Hilo suala la Bandari Huru ya Zanzibar na Muungano wapi na wapi?! Umeambiwa bandari ni suala la muungano?!
Angalia kiroja chako kingine! Eti mbona sijazungumzia suala la bandari ya Mtwara! Ulitaka nizungumzie kitu ambacho hakikuwa sehemu ya mjadala??!! Kama ni mara yako ya kwanza kuingia kwenye mijadala ya bandari; kwangu mimi nishafanya hiyo mijadala mara kadhaa na ndio maana wala sikuona sababu ya kufungua hyo link uliyoweka kwa sababu hakuna cha maana utakachosema ambacho watu hatujakijadili hapa!!
Na hata hilo suala la gharama tushawahi kujadili hapa takribani miaka 3 iliyopita!! Mjadala ulihusu mikopo ya muda mrefu yenye riba ndogo lakini total ya unacholipa kinakuwa kikubwa maradufu!!!
Investment projects ni topic of my interest!! Nishajadili sana humu jamvini masuala ya bandari, reli, madini na gas na kwa kawaida, huwa siongei kabla ya kufanya utafiti!!!
Hata suala la bandari ya Mtwara nishawahi kulijadili hapa mara kibao tu siku za nyuma! Post yangu ya karibuni kabisa kuhusu bandari ya Mtwara ni ile ya February 19! Hii hapa:
Kuhusu Mtwara... uzuri wa pale ni natural habor lakini bado huwezi kuchanganya bandari ya kawaida na oil shippers terminal! Kwa gas boom iliyo kusini, biashara ikishachanganya bandari ya Mtwara itakuwa bize sana na mimeli ya kusafirisha gas na ile mimeli ni mikubwa mno... mtu akifunga nanga; wengine mnasubiri!!!
Hayo mambo ya kusubiri ndo asiyoyataka Mchina na ndio maana akaamua aanze moja! I guess hata kiusalama not advisable!
Kwahiyo, si kwamba bandari ya sasa ya Mtwara nayo inatakiwa kupanuliwa kwa ajili ya meli za mafuta lakini hata ukitaka kujenga bandari nyingine bado huwezi kujenga pale pale! Na ndio maana hata Dangote ametaka kujenga bandari yake kwa sababu inaonekana ana uzoefu wa bandari zinazohudumia meli za mafuta kwa sababu kule Nigeria zipo sana na karibu zote kama sio zote zinajengwa separately.
Hapo nilizungumzia bandari ya Mtwara kwa sababu hoja ilihusu bandari ya Mtwara!!
Hapa hoja ni bandari ya Bagamoyo we unataka nizungumzie bandari ya Mtwara... wapi na wapi! Ndo maana nikakuambia unaleta siasa!!
Unaleta siasa kwa sababu unahangaika kuonesha nini serikali inafanya na matokeo yake; unachanganya madesa! Unaambiwa biashara za Wachina, wewe unaleta habari za copper ya Zambia! Unaambiwa kutakuwa na impact ndogo kwenye ujenzi wewe unaleta habari za kuingiza kipato!!!
Soma uelewe kabla hujakurupuka ku-comment!!!
Halafu ulivyo kiroja eti inaniuma kwa sababu hatuchangamkii fursa za Wachina!! Asiyechangamkia fursa za Wachina ni nani?! Au kwa akili yako unaamini Uchina na Uturuki ni tofauti?!
Unatamba kutochangamkia fursa za Wachina halafu inakuja nchi maskini kama Ethiopia unaiomba msaada wakati na yenyewe inasaidiwa na Wachina!! Anakuja Jacob Zuma unamuomba msaada wakati hao BRICS wenyewe huwa wanapiga magoti kwa China!!