Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,589
Hivi unashindwa kujieleza bila kutukana mtu, kichwa changu kikiwa kizito au chepesi kina kusaidia nini.We jamaa una kichwa kizito kishenzi kuelewa!!! Hivi umeambiwa mizigo ya Zambia na Malawi au umeambiwa Wachina wana projects za bandari sehemu kadhaa Afrika kwa ajili ya ku-facilitate biashara zao?!
Hebu rudia kusoma hapa:Halafu ona tena unavyoropoka!! Umeambiwa bandari ya Tanga haiwezi kuchangia mapato au umeambiwa suala la bomba la mafuta kupita Tanga lilikuja by chance baada ya Total kushituka dakika za mwisho kutumia Mombasa? Again, soma tena hapa:
Wapi nimezungumzia suala la bandari ya Tanga kuingiza kipato kidogo au kikubwa?
Hilo suala la Bandari Huru ya Zanzibar na Muungano wapi na wapi?! Umeambiwa bandari ni suala la muungano?!
Angalia kiroja chako kingine! Eti mbona sijazungumzia suala la bandari ya Mtwara! Ulitaka nizungumzie kitu ambacho hakikuwa sehemu ya mjadala??!! Kama ni mara yako ya kwanza kuingia kwenye mijadala ya bandari; kwangu mimi nishafanya hiyo mijadala mara kadhaa na ndio maana wala sikuona sababu ya kufungua hyo link uliyoweka kwa sababu hakuna cha maana utakachoniambia ambacho sikifahamu!! Ikiwa unachanganya madesa kwa mambo yaliyo wazi kabisa hayo yaliyojificha sijui utajadili vipi!!!
Investment projects ni topic of my interest!! Nishajadili sana humu jamvini masuala ya bandari, reli, madini na gas na kwa kawaida, huwa siongei kabla ya kufanya utafiti!!!
Hata suala la bandari ya Mtwara nishawahi kulijadili hapa mara kibao tu siku za nyuma! Post yangu ya karibuni kabisa kuhusu bandari ya Mtwara ni ile ya February 19! Hii hapa:Hapo nilizungumzia bandari ya Mtwara kwa sababu hoja ilihusu bandari ya Mtwara!!
Hapa hoja ni bandari ya Bagamoyo we unataka nizungumzie bandari ya Mtwara... wapi na wapi! Ndo maana nikakuambia unaleta siasa!!
Unaleta siasa kwa sababu unahangaika kuonesha nini serikali inafanya na matokeo yake; unachanganya madesa! Unaambiwa biashara za Wachina, wewe unaleta habari za copper ya Zambia! Unaambiwa kutakuwa na impact ndogo kwenye ujenzi wewe unaleta habari za kuingiza kipato!!!
Soma uelewe kabla hujakurupuka ku-comment!!!
Unanishangaza sana kuona unasema mijadala ya bandari unaijuwa na unashindwa kuona kwanini Total walichaguwa bandari ya Tanga na kuiacha Mombasa. Kama umeshindwa kufunguwa link kwa kuogopa ukweli basi pitia hata comment zangu za zamani uone nilivyojadiliana na wakenya hapa JF kuhusu swala zima la bandari ya Tanga Vs bandari za Kenya.
Tanga ilichaguliwa kutokana na geographic location yake. Bandari ya Tanga inakingwa na visiwa vya Pemba na Unguja kutokana na mawimbi makali ya kipindi cha mvua za monsoon zinazo toka mashatiki ya mbali. Bandari ya Tanga ina uhakika wa kuweza kupokea meli mwaka mzima na majira yote. Rais Museven mwenyewe na Total walikataa kwenda Mombasa kwasababu wangekuwa na uhakika wa miezi tisa tu ya kupakia mafuta yao kinyume na bandari ya Tanga inayotoa uhakika wa miezi yote kumi na mbili. Najuwa hupemdi kusoma link labda nikuwekee picha ya hayo maneno.
Kama wewe mjadili mkubwa wa hayo mambo ungelijuwa hili na kulitamka. Katika kanda hii ya Afrika Mashariki, ni Tanzania na Djibouti tu ndio wanabadari iliyo na maji yalio tulia. Wengine wote Kenya, Somalia, Mozambique wana mabahari yenye dhoruba na mushkeli ya hali mbaya ya hewa.
Unag'ang'ania kuwa wakenya wanakimbili kuchukuwa fursa hapa Afrika Mashariki, lakini hutaki kusema kwa gharama gani. Are they really getting value for money. Sijawai kuona mfanyabiashara ananunua bidhaa na kujaza duka bila kuwa na uhakika kama alichonacho kitauzika. Hivyo ndivyo wakenya wanavyofanya hivi sasa, no consensus kama bidhaa wanazo ziweka dukani zitanunulika au la, na reli ikiwa ni moja ya hizo bidhaa. Lamu port inategemea sana Ethiopia na South Sudan huku nchi hizo zinajiweka mkao wakula na Djibouti.
Narudia kule nilikoanza, niliweka badari zote hapa Tanzania pamoja na Mtwara kuonyesha fursa zilizokuwepo, na kwanini hatutaki kukimbilia mikopo isiyokuwa na mbele wala nyuma ilimradi na sisi tuonekane tupo. Hivi unajuwa na sisi Tanzania tuna mafuta yanayosubiri kuthibitishwa, Congo na wao wanayo wanasubiri kuthibitishwa na kukubaliana na Uganda ili waanze kuyavuna na kuyapitisha Tanga. Sasa ukisema mafuta hayataleta revenue kubwa kwanini nchi zinaigia gharama kubwa kujenga mtandao wakuwezesha biashara hiyo kufanyika?? Hivi unajuwa hata watu wangapi wataajiriwa kwenye mradi huo, au supporting companies ngapi zitaanza kutokana na mradi huo?
Sasa ukija kwenye badari ya Bagamoyo, unasema ulijadili, what was the conclusion of that discussion??. Kwanini hiyo bandari haijajengwa mpaka leo?? Ndio maana nikwambia hatuwezi kuwa ndio mzee kwa wachina kila siku huku tunawauza wajukuu zetu kwa bila kujiangalia kwenye kioo. Bagamoyo is still ongoing project lakini striking points ndio zinakwamisha, na sitaki kuingia kiundani kwasababu majadiliamo bado yanaendekea.