Hata mi ndo nashangaa, Yani JF sikuhizi inaendelea kua ya utoto sana... Yani jamaa kama kumi wameamua anaenda kuomba msamaha na hivyo ndo hivyo hakuna lengine ..
Hapa ikumbukwe ni JPM ndo kamualika Uhuru, JPM ndo kaamua wakutane chato na si DSM... Rais anaye alika ndo hua anachagua haya yote .....
Ninachoweza kusema ni kwamba labda JPM amechoka na mawaziri wake kufanya mikutano na mawaziri wa Kenya na Ku sign makubaliano ambayo hayaendi popote ameamua hao kama viongozi wawili waketi ana Kwa ana bila mbwe mbwe za aherehe wala wanahabari waongeshane kama mandugu. Unakumbuka ile CoW ya (Ke, Ug na RW?) Muungano wa EAC ilikua haupigi hatua yoyote Hadi pale Marais wa nchi hizo tatu walipotupilia mbali mawaziri na kukutana ana Kwa ana bila mbwe mbwe na sherehe.
Ukiangalia Uhuru naye style yake hua anependa kuunda urafiki wa kibinafsi na Marais wengine... Kwahivyo hakuna siku Uhuru atakataa mualiko wa kukutana ana kwa ana Kwa mazungumzo na pia kujuana vizuri ili kutengeneza urafiki .. Marais wakiongeleshana moja Kwa moja hua wanapata nafasi ya kujuana vizuri, hua wanalazimika kuongea ki ukweli kama Tu vile unaongea na mtu mtaani bila diplomatic protocols... Hii inaweza kufanya nchi hizi mbili zianze kua na uhusiano Bora zaidi manake Marais wawili wanaaminiana... Hata raia wa kutoka nchi hizi mbili akiuliwa ndani ya nchi nyengine itakua inawezeaha rais wa huyo aliefariki kumpigia simu ya kibinafsi huyo rais mwengine na waongeleshane vizuri bila uhasama wowote .