Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji23] [emoji23] [emoji23]Nusu niipotezee topic, nilijua umeanza darasa lako la kufunda, ila huyu bashite akishachoka kukaa huko bondeni, makomeo akimrudisha, tunaomba arudi moja kwa moja kolomije kulima vitunguu.
Simu yako ndio lile toleo jipya
kama mmechafuliwa bila kufikshwa kileleni, chepukeni!Unapoona kwenye mahusiano watu wanagombana lakini hawaachani jua hao wanapendana sana na hutimiziana haja zao mubashara kabisa! Hufikishana kileleni!!!
Mahusiano mengi yamevunjika kutokana na tatizo sugu la kutofikishana kileleni hakika hii ni Kero kubwa mno
Elimu ina pande mbili, unaweza kusoma na ukafaulu mitihani lakini usielimike na mwingine anaweza asisome elimu rasmi lakini akaelimika na kuwa mtu bora kabisa
Ni katika hilo la elimu kuna utashi utayari kujituma kuelewa na kiwango cha IQ pia! Kuna watu kwa njia za ajabu kabisa wamepata mafanikio yanayoliliwa na wengi lakini kwakuwa kiwango chao cha ufahamu ni kidogo sana wamejikuta wanaangukia pua na kufeli kabisa
Kwenye mfumo wa taa za magari kuna taa inawaka sana inaitwa spotlight...hii haiwashwi hovyo! Dar es salaam ni spotlight ya nchi kuna tofauti kubwa sana kati ya rc wa Kigoma na rc wa Dar
Chochote kinachofanywa Dar kinakuwa kama mwongozo wa kwingine kote
Mtu ambaye anabamba sana kwasasa kwenye mijadala ni bwana Makonda (bashite?) vyovyote iwavyo kati ya wengi wanaomponda wengine ni kutokana tu na wivu na kijicho! U-rc wa Dar si nafasi ndogo ati pesa hata kama huitaki itakufuata tu na ukiikataa basi unahitaji kupimwa akili
Tumjadili rc kwa hulka yake ya kutotimiza yale anayoyaanzisha. Hili halina tofauti na ile Kero ya kutofikishwa kileleni
Hulka hii mbaya ni sawa na chumba kile cha mahututi gereza la fikra
Haya yameishia wapi?
Vitambulisho maalum vya walimu ili wapande bure
Dar tuitakayo
Operation Ondoa ombaomba
Kero za wanadarisalama
Na operation nyingine nyingi zilizifeli kabisa
Shida ni moja maandalizi na kushirikishana hakuna. Lakini Dar ni jiji lenye wataalam na wasomi wa kila kaliba iweje hakuna kujadiliana kwanza?
La dawa za kulevya ndio bye-bye tumeachwa na hamu zetu hatujafikishwa kileleni tunachafuliwa tu kila wakati
Kama ukiamua kuwa banditu baki hivyohivyo usiwe kama mkate mgumu mbele ya chai
Mwanaume kakaa mahabusu siku zaidi ya 100 lakini katoka na tabasamu wewe Leo kuombwa tu kuonyesha vyeti unamwaga michozi hadharani! Nini maana ya kuwa kiongozi?
Unapenda lakini cha ajabu hutaki nikupe koni.... Sijui kabisa upoje ati.[emoji23][emoji23][emoji23] wapenda ngono tumekuja tunakutana na intelligensia ya ajabu!!! Mkuu kapangilia hoja yake vizuri sana
Zimeishia njianiCha kushangaza sana kumbe haya mambo yanaambukiza. Nimejaribu kuangalia sekta nyingine mambo ni yaleyale! Operation za jeshi la police za tinted na spotlight sijui zimeishia wapi
Mkuu badilisha hicho kiambishi from Tumebakwa kuwa nimebakwa,Mshana upo vizuri sana,umelete hoja nzuri na umeipangilia.Tumebakwa tukaachwa njiani
Bro umenivuta vizuri sana,nikajua yale mambo ya faragha sheikh..kumbe ufundi flani tu wa kiuandishi katika kuivuta hadhira.Cha kushangaza sana kumbe haya mambo yanaambukiza. Nimejaribu kuangalia sekta nyingine mambo ni yaleyale! Operation za jeshi la police za tinted na spotlight sijui zimeishia wapi