DOKEZO Kero IFM Mwanza Campus, mamlaka husika tusaidie wanafunzi

DOKEZO Kero IFM Mwanza Campus, mamlaka husika tusaidie wanafunzi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mbwa kala mbwaa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2013
Posts
218
Reaction score
389
Naandika hapa jamiiforums ili kupata msaada baada ya meneja wa campus daktari Ally Zawadi kushindwa kutusaidia.

BAADHI YA KERO:

1: UBOVU WA MAZINGIRA YA KUJIFUNZIA
Kwa muda sasa, kampasi hii imepoteza mwelekeo. Tupo wanafunzi zaidi ya 1000 hapa Mwanza na tunalipa ada isio pungua milioni moja kwa mwanafunzi, meaning kwa mwaka tunalipa zaidi ya bilion moja chuoni. Ina maana IFM wameshindwa kununua jenereta lake?

Siku ya Jana Jumatano ya tarehe 14.12.2022 Umeme ulikatika saa moja jioni tukiwa katikati ya mitihani na ikaahirishwa tukiwa tumeanza kufanya.

Leo Tena mchana umeme umekatika. Kwa kuwa madarasa baadhi hayana vioo kulingana na partition zake hivyo kuwa Giza hata mchana, tumerundikwa katika madarasa machache yenye mwanga hafifu huku joto likiwa Kali.

Kwa kuwa chuo kimepanga rock City Mall, tunapata shida kwani kwa idadi ywtu , maeneo ya kujisomea Ni machache mno.

Usalama wetu upo wapi? Afya zetu zipo na usalama gani? Ada zetu zinatumika wapi Kama hata kununua jenereta hamuwezi? Mnafundisha financial management ilhali mambo madogo mnashindwa ku manage.

2: CUSTOMER SERVICE YA HOVYO
Baadhi ya watumishi Wana customer service ya hovyo kabisa, hasa ofisi ya admission na examination office.
Wanafunzi wakiwa na shida ya kutatuliwa, madam L.N wa examination office huwajibu hovyo na kufoka! Pia ofisi ya admission Ina watu wasio jali wanafunzi na wenye lugha ngumu. Hapa kinara wao ni Mr T na Mr E.F. Nimetumia initials kwani mamlaka zinawajua waliopo ofisi hiIlzi

Kwa ujumla, Kuna shida na IFM MWANZA CAMPUS itazamwe na mamlaka zinazo husika ili wanafunzi tusiendelee kutaabika.

NAWASILISHA.
Mwanafunzi, Mwanza Campus.

Soma pia:

 
Mbona campus zinazotoa kozi kama hizo ni nyingi nyie mnafuata jina sasa muache kulalamika
 
Pole sana mkuu, sio Mwanza tu hata main campus ifm ina tatizo la eneo kulinganisha na idafi ya wanafunzi.

Wanafunzi lundo kaenek kadogo na bado course zinazidi kuongezwa kila mwaka.
 
Pole sana mkuu, sio Mwanza tu hata main campus ifm ina tatizo la eneo kulinganisha na idafi ya wanafunzi.

Wanafunzi lundo kaenek kadogo na bado course zinazidi kuongezwa kila mwaka.
Asante Sana. Kinacho kera hapa Mwanza ni huduma mbovu. Baadhi ya maofisa wanasahau Kama sisi ndio wqteja wao. Tunapo wapelekea shida wanajibu hovyo. Mfano Ni Campus manager Dr Zawadii na mdada Anaitwa Luciana. Wamulike hii campus kutatua
 
Mbona campus zinazotoa kozi kama hizo ni nyingi nyie mnafuata jina sasa muache kulalamika
Kitaaluma, kwa maana ya walimu na ufundishaji, Hawa jamaa wapo vizuri. Warekebishe tu hizi KERO ndogondogo ili kuboresha mazingira ya kujifunzia
 
Naona biashara ya Makamba ya majenereta inaporomotiwa
 
Binafsi nimemaliza mwaka Jana hapo campus ya Mwanza. Mtoa mada anasema kweli, kinacho itafuna hio campus ni hizo idara mbili, examinations office na admission. Wafanyakaz wake wanajifanya miungu watu. Huyo bidada Alie kosa mwili, Lusiana wa examination Ni shida. Unapo kwemda na Jambo la kukusaidia, anaweza kuamua tu kukujibu hovyo kabisa kuwa Hana muda huo mchafu! Hapo admission ukiwa unaomba kuingia chuo Ni Jambo la kawaida kujibiwa dry na hovyo na akina telekako na yule mwingine bonge bonge wa admission, Ferdinand Kama nakumbuka jina vizuri.
Haya yashughulikieni
 
Wahusika watakua wamesikia. Udhaifu popote hauwezi kukosekana, Ila hakuna kitu kinaudhi Kama dharau. Sisi Ni wateja. Huyo mtajwa katika examination office ni kawaida kujibu jeuri na kejeli kwa wanafunzi wanao enda kupata huduma kwake. Menejimenti ifanye uchunguzi tu rahisi itagundua kuwa mwiba unao zuia ukuaji wa campus ni ofisi ya admission na hapo examination. Maofisa wake hawana weledi wa kazi. Jipu lingine Ni computer lab, Mr Swai anaomba Hadi buku kwetu wanafunzi, sijui hawamlipi mshahara🤣🤣
 
Back
Top Bottom