Rejea mazungumzo Yako ya awali,umesema biblia ni uongo,ukweli ndio ule uliniambia hizo ni myth,ndio maana namuuliza ukweli ni Nini?
Ni post gani nimeandika biblia ni uongo ?? Inaelekea unakuwa unasoma kwa jaziba hata huelewi nilichokiandika
Dr. J.K. Elliott, wa kitengo cha Thiolojia na Tafiti za Kidini wa Chuo Kikuu cha Leeds, ameandika makala iliyochapishwa katika jarida la The Times, London (10 Septemba, 1987) yenye kichwa "Kutazama mizizi ya Biblia".
Ndani ya makala yake, ameeleza kuwa: "Zaidi ya miswada 5,000 inayojumuisha Agano Jipya lote au sehemu yake iliyo katika lugha ya asili.
Miswada hii imepangika katika madaraja ya kuanzia karne ya pili hadi kuvumbuliwa kwa uchapaji.
Imekisiwa kuwa hakuna hata watu wawili wanaoafikiana kwa kila kitu.
Bila shaka, maandishi yote ya mkono yanastahili kuwa na makosa ya bahati mbaya wakati wa kunukuu.
Hata hivyo, katika kazi za kitiolojia si jambo la kushangaza kuwa mabadiliko ya kufikirika sana yaliingizwa ili kuondosha au kubadili maelezo ambayo waandishi wanayaona kuwa hayapendezi.
Pia kulikuwa na mwelekeo wa wanukuzi wa kuongeza ufafanuzi au fasiri.
Mabadiliko ya hadhari yanadhaniwa kuwa yameingizwa katika zama za mwanzo kabla ya kuanzishwa hali ya kanisa ya Agano Jipya.
Mwandishi aliendelea kufafanua kuwa "hakuna hata mswada mmoja wenye matini isiyobadilishwa kutoka katika uasilia wa ukamilifu wake, na kwa hiyo, "hakuna awezae kuchagua mswada wowote miongoni mwa miswada hiyo na kuuamini kwa imani ya pekee eti mswada huo ndio wenye ukiritimba wa kuwa ndio maneno asilia ya watunzi."
Aliendelea kusema zaidi: "Kama mtu ataendelea kupinga na kudai kuwa maandiko asilia yamenusurika pahala fulani kwenye maelfu ya miswada iliyopo, basi mtu huyo atalazimika asome miswada yote hiyo, hatua kwa hatua, ili kukusanya tofauti miongoni mwa miswada hiyo, kisha atathimini, lahaja kwa lahaja, ili ajue ni mswada upi wenye [matini] asilia na upi ndio wa matini ya nafasi ya pili.
Matarajio kama hayo yaliwakatisha tamaa wasomi wengi wa Biblia walioaminia yaliyomo katika matini zilizochapwa za zama za mwanzo, wasomi hao walichukua ushahidi wa miswada waliyoiona kuwa ni bora.
Hata matoleo ya Agano Jipya kwa Kigiriki yaliyochapwa kisasa, vilevile mafafanuzi ya kisasa yametegemea chapa hizo za zama za mwanzo; kwa kawaida hufuata utaratibu huu wa kujenga matini zao kwa kutumia msingi finyu ambao hauonekani kuwa ni wa asili kikamilifu."