KERO: Masanja Mkandamizaji kutumia Ulokole kinyume na maadili ya Kipentekoste

bampami

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2011
Posts
5,699
Reaction score
4,117
Habari ya mda Huu..

Asilimia kubwa ya watu duniani wanaamini uwepo wa Mungu, na uwepo huu wa Mungu umeleta Imani tofauti tofauti za ambazo binadamu huziishi. Na Imani hizi zinaheshimiwa, wapo wenzetu waroma, wakatholiki, wapentekoste, kila imani inataratibu zake na miiko yake inayoheshimiwa na kila muumini wa dini hiyo.


Kwa upande wa wapentekoste, sote twajua namna miiko yao ilivyo hasa katika mavazi, tumeona kwa waroma tumeona kwa waanglikana, zaidi sana hata kwa wenzetu waislamu.Uwepo wa dini hizi umekuwa msaada sana kwa jamii hasa kuibadilisha jamii na hasa vijana kuwa na miiko na heshima.

Lakini siku za hivi karibuni, kumekuwepo na wimbi la vijana wanaokimbilia ulokole lakini matendo yao hayaendani na miiko ya kilokole, bika kupepesa pepesa kumekuwa na celebrity huyu anayefahamika kama "Massanja mkandamizaji" ama "Emmanuel Mgaya" huyu amekuwa akijiita PASTOR.

Kumekuwa na malalamiko mengi hasa toka wa vijana wakilokole wakilalamika mienendo ya celebrity huyu na mavazi yake yasiyoendana na miiko ya kilokole, ki ukweki kuna wakati ukimwona ni kama kijana mwingine tu wa mitaani, kuvaa mlegezo, kusuka nywele, kofia kuvalia nyuma, hivi haviendani na miiko ya kikristo.

Kwenye jamii inaonyesha picha kuwa Anajifichia kwenye mwamvuli wa kipentekoste ili hali si mpentekoste...sasa unamdanganya nani massanja? hata moyo wako ukushuhudie kuwa.

Unachokifanya hakiendani na maadili ya kipentekoste, kumbuka wewe ni kioo na ni maarufu, hivyo either ubadili namna unavyovaa au uache kutumia ulokole kama kivuli cha maovu!

HAPO ALIKUWA ANAKUNYWA ULANZI
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

"massanja mkandamizaji" kujiita ameokoka tena mchungaji mtarajiwa!!!

[emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115][emoji115]

Unaharibu Taratibu za kipentekoste!


Ujumbe huu ukufikie mahali pote ulipo
u
 
Nani alikwambia kila celebrity kanisani kafuata injili? Hiyo chumvi tu kwenye mboga, ukizingatia kuna biashara kubwa huko. Ndio maana kila siku unawaona kanisa la "nabii" mpya linapokatwa pochi nene zaidi. Rose Muhando si yule pale, Oo Yesu, Yesu (wakati ana pesa) alivyofulia akamiss msikitini (kasahau kashatuimbia kila kitu ni possible kwa Yesu) mara ghafla huyooo kwenye ngada.
 
Unaweza ukavaa suruali bwaga kama gunia la mashineni lakini kama moyoni hakuna Mungu ni buree.
Infact kuvaa milegezo na kusuka kweli inaweza ikatia mashaka ila kuvalia kama hapo kwenye picha sijaona sana ubaya
" Chakula ni kwa tumbo na tumbo ni kwa chakula lakini roho ni kwa Bwana"
 
Blaza men nwenye bm
 
Biblia imetoa mwongozo wa mavazi kwa wakiristo wore.
Huwezi vaa vibaya ukasema sio tatizo eti kwakuwa una moyo safi
Ni sawa upewe mahubiri na shetani useme eti nafuata maneno yake sijali matendo yake.shetani atabaki kuwa shetani na kamwe hawezi mtukuza Mungu.
 
Milokole mishamba siipendi kama nini, kwa hiyo ukiokoka ndo umeambiwa uvae magunia, kama huwezi kwenda na wakati pita hivi [emoji118]
Labda wanataka avae suruali za maselebresheni ndio ataonekana ameokoka. Mi sijaona tatizo na mavazi yake.
 
Nakubaliana na hoja yako kwa 99.999%. Hilo ni tatizo la kubeba Biblia kama mzigo bila kujua kilichomo ndani yake.



#nakwenda_zimbabwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…