Kero: Msafara wa Rais umekuwa mateso kwa watumiaji wa barabara

namraroh

Senior Member
Joined
Sep 9, 2010
Posts
114
Reaction score
125
Ni kawaida kwa viongozi wetu kuwa na misafara mikubwa na yenye mbwembwe kibao, lakini kwa mtukufu rais wangu wa awamu hii umekuwa kero na mateso kwa watumiaji wa barabara kwa kuzingatia kwamba mara nyingi anasafiri kwa barabara, hali imekuwa mbaya na mateso ya hali ya juu.

Leo wakati naelekea Mpwapwa tumekwamishwa kwa zaidi ya saa moja kwenye kituo cha mafuta jirani na kituo kikuu cha mabasi Morogoro, kwa kweli nashauri wahusika wabuni njia mbadala ya kumsafirisha rais wangu.
 
Ni bora atumie ndege kupunguza foleni na kuchelewesha watu ikizingatiwa na hizi tochi.
 
Ni kawaida kwa viongozi wetu kuwa na misafara mikubwa na yenye mbwembwe kibao, lakini kwa mtukufu rais wangu wa awamu hii umekuwa kero na mateso kwa watumiaji wa barabara, kwa kuzingatia kwamba mara nyingi anasafiri kwa barabara, hali imekuwa mbaya na mateso ya hali ya juu, leo wakati naelekea Mpwapwa tumekwmishwa kwa zaidi ya saa moja kwenye kituo cha mafuta jirani na kituo kikuu cha mabasi Morogoro, kwa kweli nashauri wahusika wabuni njia mbadala ya kumsafirisha rais wangu!
kumbe mzee wa msoga Alitukanwa bure wakati alipokuwa anatumia usafiri wa Anga afanyapo ziara mikoani?
 
Na Mimi pia yamenikuta hayo oil com kihonda Nimekaa zaidi ya saa moja Kimsubr mtukufu apite nimekereka sana
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Inaudhi sana.Anakwamisha watu kuwahi sehemu zao za kazi
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Eti kwa sababu ya kutaka sifa kuwa anatumia usafiri wa barabara ndio atese Watanzania wengine ambao pia wanahitaji barabara kwa kufanya shughuli zao!!! Hii haikubaliki kabisa!

Halafu sio kweli kwamba kutumia magari anaokoa pesa....Usikute ndio anazidisha gharama kuliko angetumia usafiri wa anga.
 
Ni kawaida kwa viongozi wetu kuwa na misafara mikubwa na yenye mbwembwe kibao, lakini kwa mtukufu rais wangu wa awamu hii umekuwa kero na mateso kwa watumiaji wa barabara, kwa kuzingatia kwamba mara nyingi anasafiri kwa barabara, hali imekuwa mbaya na mateso ya hali ya juu, leo wakati naelekea Mpwapwa tumekwmishwa kwa zaidi ya saa moja kwenye kituo cha mafuta jirani na kituo kikuu cha mabasi Morogoro, kwa kweli nashauri wahusika wabuni njia mbadala ya kumsafirisha rais wangu!
Huo msafara huwa ni kero sana Kwa abiria Wa daladala
 
Acheni ujinga kwani wote wanaopanda ndege wanajua kingereza?
 
Ni kawaida kwa viongozi wetu kuwa na misafara mikubwa na yenye mbwembwe kibao, lakini kwa mtukufu rais wangu wa awamu hii umekuwa kero na mateso kwa watumiaji wa barabara, kwa kuzingatia kwamba mara nyingi anasafiri kwa barabara, hali imekuwa mbaya na mateso ya hali ya juu, leo wakati naelekea Mpwapwa tumekwmishwa kwa zaidi ya saa moja kwenye kituo cha mafuta jirani na kituo kikuu cha mabasi Morogoro, kwa kweli nashauri wahusika wabuni njia mbadala ya kumsafirisha rais wangu!
Safi, na nyie mikoani msafe kidogo maana huku dar ni kero.
 
Ila Kwann asipande hizo bombadia zake au mabovu yatutoe kafara sisis
 
Back
Top Bottom