KERO: Umeme wa kununua kwa zamu na nyumba za kupanga ni janga

KERO: Umeme wa kununua kwa zamu na nyumba za kupanga ni janga

Wakuu, nimepita sehemu hii jioni kuna ugomvi mkubwa kisa ni zamu za umeme, kiukweli hizi luku ni nzuri kama wapangaji wako wachache na wanaelewana vinginevyo ni majanga.

Hivi haiwezekani kila mpangaji akawa na mita yake kama vile switch?

Mabachela inakula kwao zaidi wanaotoka asubuhi kurudi usiku hasa wale wasio na vifaa vingi vya umeme lakini kwenye malipo wanalipa sawa, ukute anawasha taa tu ghetto akirudi.

Vipi una ushuhuda wowote kwenye hili?
Siku hizi kuna tecnolojia kila mpangaji anafungiwa kipima umeme chake sijui vinaitwaaje yaani unalipa kulingana na matumizi yako bei yake havizidi 20 ,000 kugombana kwa ajili ya umeme ilikuwa zamani
 
Mfano umenunua umeme wa elfu 10,000 unapata unit 22 pale unaenda kuingiZa kwenye miter lakini kwenye kile kidude chako labda tuseme umenunua kipya kinasoma sifuri ukiweka na kuanza kutumia inasoma mwisho wa siku unit zako 22 zikiisha unaongeza mwingine
Practicality yake ipoje. Ni meter mfano wa hizi LUKU ama ni device nyingine kabisa.
Je ni legal, je gharama zake.

Nasikia hizi submeter ni kwa akili ya kutazama matumizi yako tu, lakin huwezi kutumiwa kujaza umeme wako pekee lazima ukajaze kwenye LUKU meter ya nyumba nzima.

Sasa inasaidia nini hapo
 
Hii safi kabisa,ntanunua kwa ajili ya wife wangu,, huyu ndiye amekuwa jini mnyonya umeme hapa nyumbani,nina wapangaji sita,wanne ni mabaharia na wawili ni family ndogo ndogo za toto moja moja,wapangaji hawana shida na mtu,wanalipa hela za maji na umeme kwa wakati na kwa usahihi kabisa,tatizo ni mke wangu,hazimi taa usiku wala mchana,vyumba vyote,hazimi tv,music system,sana sana atapunguza sauti tu,jiko la plate la kizamani amelileta sijui kaliokota wapi,anapikia kuanzia makande mpaka magimbi,anakausha nguo na blower(heat blower) maji ya kuoga anachemsha kwa jug(kettle?) Yaani kama vile ana uvomvi na watu hapa,nikimuambia anavuta mdomo wiki!! Sijui nimuuze? Ila hapana aisee,nampenda sana!
Mfano umenunua umeme wa elfu 10,000 unapata unit 22 pale unaenda kuingiZa kwenye miter lakini kwenye kile kidude chako labda tuseme umenunua kipya kinasoma sifuri ukiweka na kuanza kutumia inasoma mwisho wa siku unit zako 22 zikiisha unaongeza mwingine
 
Wakubwa salama!

Nitoe pole sana kwa changamoto hizi.

Kuna ufumbuzi wa hili tatizo.

Kuna submeter ambazo zinafungwa kwa kila chumba cha mtumiaji ambavyo

itamwezesha mtumiaji kuweza kununua luku yake mwenyewe kwa njia ya simu, hasa tigo pesa. Atapata tokeni za umeme na kuziweka kwenye hiyo submeter.

Kama mtumiaji atashindwa kuweka umeme basi atalala giza mwenyewe na siyo nyumba nzima. Na maji pia vivyo hivyo

IMG_5248.JPG


Submeter ya umeme

IMG_5250.JPG


Submeter ya maji.

Kwa maelezo zaidi tembelea www.edcom.co.tz

Shukrani
 
Hebu tufanye nimenunua umeme units 20.
Nikaweka kwenye LUKU meter (ile ya nyumba nzima) haya nina hicho kifaa changu getto kinasoma matumizi yangu tu.

Wakat kifaa kinasoma nimetumia units 12 mara umeme unaisha kwenye LUKU (kumbuka kuna wapangaji wengine)

Je, nitakaa Giza kusubiri huyo mpangaji aliyetumia share ya units zangu akanunue umeme aweke ili namie nifidie units zangu 8 zilizobaki??

Mie nikajua hicho kifaa kina separate matumizi ya units ya kila mtu kumbe Hamna kitu.

Ni kweli kinapunguza tatizo kwa 50%, bado hiyo 50% ya kuzuia units za mpangaji A kutumiwa na mpangaji B bila ruhusa yake.

Labda sijaelewa vizuri ufanyaji kazi wa hicho kifaa.
Umeme ukiisha haununui ww watanunua wenzio mpaka ww kwako ufike 20 mm sioni kama ni usumbufu kwa sababu kamma ulikua unalipa pesa wa wote elfu20 kwa mwezi ile submeter itakusaidia kujua matumizi yako kama ulikua unanyonywa au ww hnawanyonya wenzio
 
Hebu tufanye nimenunua umeme units 20.
Nikaweka kwenye LUKU meter (ile ya nyumba nzima) haya nina hicho kifaa changu getto kinasoma matumizi yangu tu.

Wakat kifaa kinasoma nimetumia units 12 mara umeme unaisha kwenye LUKU (kumbuka kuna wapangaji wengine)

Je, nitakaa Giza kusubiri huyo mpangaji aliyetumia share ya units zangu akanunue umeme aweke ili namie nifidie units zangu 8 zilizobaki??

Mie nikajua hicho kifaa kina separate matumizi ya units ya kila mtu kumbe Hamna kitu.

Ni kweli kinapunguza tatizo kwa 50%, bado hiyo 50% ya kuzuia units za mpangaji A kutumiwa na mpangaji B bila ruhusa yake.

Labda sijaelewa vizuri ufanyaji kazi wa hicho kifaa.
Haki separate matumizi, chenyewe kinaonyesha unit ulizotumia, kuepuka kulipa kulipa umeme sawa kila mpangaji.
Kwa scanerio ka iyo itabidi ulale giza mpaka wenzako walipie, vinginevyo ununue meta yako pekee Tanesco.
 
Practicality yake ipoje. Ni meter mfano wa hizi LUKU ama ni device nyingine kabisa.
Je ni legal (kisheria), je gharama zake.

Nasikia hizi submeter ni kwa akili ya kutazama matumizi yako tu, lakin huwezi kuzitumia kujaza umeme wako pekee lazima ukajaze kwenye LUKU meter ya nyumba nzima.

Sasa inasaidia nini hapo
Insaidia kujua matumizi yako kama unalipa pesa nyingi halafu matumizi machache au unalipa pesa chache matumizi ni makubwa
 
Njia nzuri ya kitumia hizo energy meter (kwh meter) sijui ndo mnaita sub meter ni hii kama nielezavyo hapa chini.

Kama mna vyumba vitano, kila chumba kinafungwa meter yake ya kusoma matumizi.

Mtu mmoja ajitolee kuweka record za meter zote kwa mfumo wa maandishi, kwa mfano leo meter zote zinasoma 0 tumeweka umeme wa 30000 tukapata labda unit 100 baada ya siku 20 umeme ukaisha, mtunza kumbukumbu ana wajibu wa kupitia kila meter kuangalia unit zilizotumika, atakuta kuna , 3 , 7, 12 , 50, 28 hapo jumla itakua unit 100, kwa hyo mtazidisha unit zilizotumika kwa bei ya 350 au 100 itategemea na tarrif ya Luku yenu, kwa hyo alietumia unit 3 analipa zake kama 1000 hivi akiongeza na zile service charge anaeeza lipa 1200 hivi, wa unit 50 nae mnamzidishia na 350 au 100.
 
Hebu tufanye nimenunua umeme units 20.
Nikaweka kwenye LUKU meter (ile ya nyumba nzima) haya nina hicho kifaa changu getto kinasoma matumizi yangu tu.

Wakat kifaa kinasoma nimetumia units 12 mara umeme unaisha kwenye LUKU (kumbuka kuna wapangaji wengine)

Je, nitakaa Giza kusubiri huyo mpangaji aliyetumia share ya units zangu akanunue umeme aweke ili namie nifidie units zangu 8 zilizobaki??

Mie nikajua hicho kifaa kina separate matumizi ya units ya kila mtu kumbe Hamna kitu.

Ni kweli kinapunguza tatizo kwa 50%, bado hiyo 50% ya kuzuia units za mpangaji A kutumiwa na mpangaji B bila ruhusa yake.

Labda sijaelewa vizuri ufanyaji kazi wa hicho kifaa.
Uko sawa icho kifaa kinakupa haki yako 100%
 
Back
Top Bottom