KERO Kero ya foleni NATTA Mwanza, mistari ya Zebra nayo imefutika, ni kero hasa asubuhi

KERO Kero ya foleni NATTA Mwanza, mistari ya Zebra nayo imefutika, ni kero hasa asubuhi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaomba sana wahusika watutatulie kero ya usafiri katika eneo la NATTA jijini Mwanza. Mimi binafsi napitia eneo hili mara kwa mara, na hali ya foleni imekuwa mbaya sana. Pale kuna vituo viwili vya daladala—kimoja cha kwenda mjini na kingine cha kutoka mjini—lakini miundombinu iliyokuwepo haifanyi kazi ipasavyo.

Kulikuwa na mataa ya kuongozea magari (traffic lights), lakini kwa sasa hayafanyi kazi kabisa. Pia, kivuko cha waenda kwa miguu (zebra) kilichokuwepo kimefutika, jambo linalosababisha usumbufu mkubwa kwa watembea kwa miguu na magari. Hali hii imechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la foleni, hasa katika njia panda ya kuelekea Bugando Hospital.

Mfano halisi ni siku ya Jumatatu tarehe 11, majira ya saa 7 mchana, ambapo tulikaa kwenye foleni kwa takribani masaa mawili. Kwa kweli kuingia mjini kupitia eneo hili imekuwa ni kero kubwa sana. Tunaomba mamlaka husika zichukue hatua za haraka kurekebisha mataa na kuweka alama za barabarani ili kupunguza msongamano na kurahisisha usafiri.
photo_2026-05-19_18-08-31 (2).jpg
photo_2026-05-19_18-08-31.jpg
photo_2026-05-19_18-08-30.jpg
photo_2026-05-19_18-08-29.jpg
 
Back
Top Bottom