Kero ya Kukatika Umeme Mara kwa Mara: Wiki hii kukatika umeme kunanitesa kuliko zile siku 10 za mgao

Kero ya Kukatika Umeme Mara kwa Mara: Wiki hii kukatika umeme kunanitesa kuliko zile siku 10 za mgao

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Wiki hii kukatika umeme kunanitesa kuliko kawaida, wanakata asubuhi saa 12 wanarudisha jioni saa 12 na nusu. Masaa zaidi ya 12.

Niseme wazi siku zile 10 za mgao zilizotolewa sikuwa na kazi nyingi sana hivyo wala sikuona kama ni issue sana na wala sikuathirika.

Balaa lipo wiki hii nina kazi nyingi zinazohitaji umeme lakini ndio hivyo tena.

Nimeshindwa kuvumilia bora nitoe hili dukuduku roho yangu itulie.
 
Ukipita kwenye ofisi za tanesco ndo utagundua kuwa Tanzania tatizo la umeme haliwezi kwisha maana wale jamaa wanatengeneza matatizo maksudi ukiwakuta pale nje asubuh walivyo wengi bila kukata umeme wengi watakosa kazi za kufanya kiufupi wanatengeneza matatizo ili wapate hela za maintenance.
 
Wiki hii kukatika umeme kunanitesa kuliko kawaida, wanakata asubuhi saa 12 wanarudisha jioni saa 12 na nusu. Masaa zaidi ya 12.

Niseme wazi siku zile 10 za mgao zilizotolewa sikuwa na kazi nyingi sana hivyo wala sikuona kama ni issue sana na wala sikuathirika.

Balaa lipo wiki hii nina kazi nyingi zinazohitaji umeme lakini ndio hivyo tena.

Nimeshindwa kuvumilia bora nitoe hili dukuduku roho yangu itulie.
majenereta si yapo mkuu.
 
Chukulia ndo mtu unategemea saluni
Watengenezaji na wauzaji wa juices za matunda!

Wauza juice ya miwa.

Watu wa saluni.

Wapo wanaotegemea vibanda umiza kulisha familia zao.

Hili swala la kutegemea TANESCO nchi nzima linaumiza sana.
 
Back
Top Bottom