Kero ya Kukatika Umeme Mara kwa Mara: Wiki hii kukatika umeme kunanitesa kuliko zile siku 10 za mgao

Kero ya Kukatika Umeme Mara kwa Mara: Wiki hii kukatika umeme kunanitesa kuliko zile siku 10 za mgao

Waziri wa Nishati mh Makamba kwa mbwembwe nyingi alituaminisha kwamba tatizo la umeme itakuwa hadidhi baada ya kufanyia matengenezo makubwa mitambo ya kufua umeme kwa mda wa siku kumi. Tena akaenda mbali anasema ya kwamba mitambo hiyo ni mibovu kwa sababu kwa kipindi chote cha marehemu JPM haikufanyiwa matengenezo kwa sababu makundi waliogopa kuizima mitambo hiyo ili kuifanyia matengenezo kwa kuogopa JPM. Lakini ajabu kubwa ni kwamba baada ya matengenezo ya mitambo hiyo ndiyo tatizo la umeme limeongezeka zaidi.

Je mafundi waliiharibu mitambo hiyo badala ya kuutengeza? Na kama siyo hivyo ni bora warudishie ubovu ulikuwepo katika mitambo hiyo ili kutunusulu na tatizo hili la umeme. Kwani ilipokuwa mibovu hatukushuhudia tatizo hili la kukatika kwa umeme kila siku

RUSSIA NA UKRAINE SITISHENI VITA MNAUA RAIA WASIYO NA HATIA
Tatizo likiisha Kabisa tutauzaje majenereta wewe acha tu.
 
Jana umeme umekata kuanzia saa 12 jioni mpaka leo 3/3 saa 3 asubuhi.


Umerudi saa 3 umekaa mpaka saa 8 mchana umekata tena wakarudisha saa 1.

Mpaka saa tatu umeshitua karibia mara 4.


Shida ni nini?


TANESCO naombi mnijibu

Hii hali itaendelea mpaka lini?

Wiki ijayo naagiza generator kutoka China.

No way out!
Ndugu mpendwa Mteja wetu
Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.
Jina
Eneo
Wilaya
Namba ya simu
Tatizo
Toka lini
Namba ya taarifa
Ahsante sana
TANESCO Huduma kwa Wateja
SIMU : 0748550000
 
Hilo tatzo kubwa la umeme umeliona wapi.

Umeme ukikatika mtaani kwenu unahisi ni Nchi nzima.
Usiwe una pinga tu hoja ya mtu,mbona hata mm nipo wilaya frani hivi umeme week nzima unakatika kila wakati,au wewe ndio makamba mwenyewe nini?
 
Usiwe una pinga tu hoja ya mtu,mbona hata mm nipo wilaya frani hivi umeme week nzima unakatika kila wakati,au wewe ndio makamba mwenyewe nini?
Walamba viatu hao huwa wanamuambiaga kwamba anakubalika sana na kwamba yeye ni waziri genius
 
Inasikitisha sana kuona jinsi shirika hili linavyoendeshwa.Miaka 60 ya uhuru lakini bado umeme ni wa shida hapa nchini.

Walau miaka michache iliyopita hapakuwa na makatizo Makali ya umeme kiasi hiki. Ina maana vyanzo vya umeme hapo nyuma vilikuwa tofauti na sasa?

Tuliaminishwa mgao mkubwa uliopita siku za karibuni ungekuwa mwisho Lakini inasikitisha kuona kila mara umeme bado unakatika kwa sababu zisizoisha.

Je, Tukisema shirika la TANESCO lina shida mahala itakuwa tunakosea?
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu
Tunafurahia kukuhudumia, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.
Jina
Eneo
Wilaya
Namba ya simu
Tatizo
Toka lini
Namba ya taarifa
Ahsante sana
TANESCO Huduma kwa Wateja
SIMU : 0748550000
Umeme umekatika asubuhi hii 8:30
Hakuna taarifa yoyote tuliyopewa na Tanesco Kahama

Mkoa: Shinyanga
Wilaya: Kahama
Kata: Nyahanga
Eneo/mtaa: Lugela
Simu: 0767659145
 
Umeme umekatika asubuhi hii 8:30
Hakuna taarifa yoyote tuliyopewa na Tanesco Kahama

Mkoa: Shinyanga
Wilaya: Kahama
Kata: Nyahanga
Eneo/mtaa: Lugela
Simu: 0767659145
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi tafadhali
 
🐒🐒🐒
0_20220223_195313.jpg
 
Umeme umekatika asubuhi hii 8:30
Hakuna taarifa yoyote tuliyopewa na Tanesco Kahama

Mkoa: Shinyanga
Wilaya: Kahama
Kata: Nyahanga
Eneo/mtaa: Lugela
Simu: 0767659145
Hats mwanza Nyegezi wamekata SAA mbili asubuhi hii
 
Wiki hii kukatika umeme kunanitesa kuliko kawaida, wanakata asubuhi saa 12 wanarudisha jioni saa 12 na nusu. Masaa zaidi ya 12.

Niseme wazi siku zile 10 za mgao zilizotolewa sikuwa na kazi nyingi sana hivyo wala sikuona kama ni issue sana na wala sikuathirika.

Balaa lipo wiki hii nina kazi nyingi zinazohitaji umeme lakini ndio hivyo tena.

Nimeshindwa kuvumilia bora nitoe hili dukuduku roho yangu itulie.
Nunua generator mkuu maana ndiyo lengo majenereta yamekaa sana stoo na mafuta nayo bei juu lita tsh 2706 huku Tanganyika sijui kwa wenzetu Tanzania wao ni bei gani?
 
Alafu mama anasema tangu aingie madarakani ameleta miradi ya kutosha sa sielewi ana maainisha nn wakati umeme ukiendelea kukata Kila siku
 
Back
Top Bottom