Kero ya kuripoti kazini baada ya kupangiwa ajira na sekretarieti ya ajira, halafu unaambiwa urudi nyumbani mpaka upigiwe simu kuitwa!

Pole sana,haya uliyoandika hapa,nenda ukawaambie wahusika ofisini, yawezekana ni mjinga mmoja tu,anakujibu eti ondoka,tutakuita kwa simu bila kujali utasafirije.Hii ina madhara kwako wewe na pia kwa akina dada pia,kwani utateseka sehemu ya malazi,chakula n.k,huku kwa upande wa akina dada,watafikia sehemu wafanye umalaya usiokua rasmi na matokeo yake wapate magonjwa,wayapeleke kwa watakaowaoa,kwani warajirahisisha ili wapate hifadhi na chakula pamoja na mahitaji yao mengine,kutoka kwa wale wanaotumia fursa za hivyo kujinufaisha.
 
Ukisoma Barua Ile ya kupangiwa Kituo inamtaka mwajiri afanye uhakiki Wa vyeti vyako Kwanza ndipo akupokee rasmi. Nadhani hicho ndo kinakula muda
Hicho ni kisingizio tu!! 1. Vyeti vilivyopandishwa kwenye mfumo vimethibitishwa kisheria na mahakama au wakili. 2. Wakati wa usaili (written interview) wahusika walikagua vyeti halisi kwa kuwatumia watu wenye utaalam wa kuhakiki vyeti na wanakula posho kwa kazi hiyo.
3. Wakati wa usaili wa oral walikagua tena vyeti na kuvihakiki!!
4. Wakati unaporipoti kituoni ulikopangiwa ajira unaenda na vyeti halisi wanavikagua, wanavihakiki na kuchukua nakala yake.
Kwa hiyo vyeti vimehakikiwa mara nne!! Hakuna sababu ya kudai bado wanahakiki tena!! Vinginevyo kabla ya placement kwa kuwa vyeti vipo kwenye mfumo wa ajira basi vitumwe NECTA na kwenye vyuo walikosoma vihakikiwe na zoezi hilo ni jepesi na la haraka sana. Kisha ndio watoe placement!! Watanzania wanatesana kwa visingizio visivyokuwa na sababu!!
 
Nyie vijana hamjitambui muwe mnauliza ili mpate kujua mambo, ukienda kuripoti kituo cha kazi ukiambiwa rudi nyumban tena inabidi ushukuru umepewa muda wa kujiandaa vzuri kwa maisha mapya... Hapo maana yake umepewa siku sio chini ya 14 kurudi kujiandaa... Hapo maana yake rudi kavute pumzi wakat wanajiandaa kukuingiza ktk mfumo wa Payroll... Hapo maana yake hawajataka ubaki kazini wakat taratibu za stahiki zako kama mtumish hazijakamilika, kumbuka mifumo ya serikal inafanya kazi kwa mawasiliano na documents sahihi... As long as umetoa namba zako za cm na email sahihi tuliza komwe lako nyumban utaitwa... Halafu pia ukiripoti kituoni na kuambiwa rudi utapigiwa cm ni vizuri uombe namba ya wahusika acheni uoga wa kijinga... Zamani watu walikua wanaripoti kituoni wanaanza kazi then mishahara inachelewa hata miezi 3 unaishi vipi..? Ndiyo maana sikuhiz wanachukua taarifa zako zote wakishakamilisha taratibu ndio unaitwa kazini... Serikal sio private sector... All in all mkipata kazi fanyeni kazi kwa bidii weledi uaminifu na mkubali kujifunza kazi kwa waliotangulia na kamwe msiige tabia mbaya mtakazozikuta kwasabab kilamtu kaingia kazini na anafanya kazi kwa malengo take binafsi...
 
Nchi hii ina wapumbavu wengi Sana! Kama anaiba matrilioni ya hela na bado yupo tu, hiyo wala hawajali kabisa!
 
Kama ni hivyo basi apewe nauli aliyotumia kuripoti kwa mujibu wa maagizo aliyopewa kwenye barua, kisha apewe nauli ya kurudi nyumbani akisubiri kuitwa tena!!
 
Mimi sikatai hayo maelezo ya kurudi kusubiri taratibu. Ninachokataa ni kutokupewa nauli ya kuja na kurudi tena nyumbani wakati walikuita wenyewe!! Hoja yangu ni kuwa utarudije wakati huna nauli? Usijifanye hujui kama mtu anaweza kuwa hana nauli!! Kuripoti kwa mara ya kwanza hiyo ni safari rasmi lazima ilipiwe nauli kamili!!
 
Serikal sio private sector... Jipange
Ukirudi kuripoti rasmi ndio utalipwa nauli na mizigo nk...
 
Naomba waziri mwenye dhamana alitolee ufafanuzi jambo hili kama TAARIFA KWA UMMA. Vinginevyo tutamwomba mama yetu SAMIA ambaye anastahili pongezi sana kwa kuruhusu maelfu ya nafasi za ajira alitolee ufafanuzi jambo hili kisha AMWAJIBISHE waziri mwenye dhamana kwa kuruhusu utaratibu usio rafiki wa kushughulikia waajiriwa wapya!! Hawa ndio huwa wanaigombanishsha serikali na raia wake, ni hujuma kwa serikali. Lazima washughulikiwe!!
 
Hata
Serikal sio private sector... Jipange
Ukirudi kuripoti rasmi ndio utalipwa nauli na mizigo nk...
niliporipoti na barua ya kupangiwa kituo ilikuwa ni rasmi na ni lazima igharimiwe!! Ni kwa kigezo kipi unasema sijaripoti rasmi wakati nilikuwa barua rasmi inayonitaka niripoti ndani ya siku 14 vunginevyo nafasi yangu atapewa mwingine? Hivi haiwezekani kuwa na utaratibu rafiki usiokuwa na usumbufu?
 
Mtu ambaye yupo pwani mkuranga na anateseka aje nyumbani kwangu akae Hadi atakapo itwa kazini.Namaanisha mtu ambaye ametokea mkoani sio aliopo Dar .Utakula utalala pazuri na ukihitaji kwenda mjini kama nauli ipo ntakupa mara Moja Moja kama unaenda mjini.Mimi ni Me na Niko nafamilia yangu.Sijali ke au Me, yeyote anayesumbuka.Hatutahitaji malipo yoyote kutoka kwako.Karibu sana
 
Wakigoma kukubaliana na wee bas kila siku fika ofc Kisha sain nenda zako au kaa kwenye benchi la wageni ikifika muda wa chai nenda rud Tena hapo

Nina maan yngu kubwa
Duh mambo n mengi mi nilidhani ukishapata tu kazi umemalizq kumbe kuna hili sakata tena jamani!!!!!!
 
Duh mambo n mengi mi nilidhani ukishapata tu kazi umemalizq kumbe kuna hili sakata tena jamani!!!!!!
Lipo sana!! Ni heri wale wanaopangiwa karibu na nyumbani kwao!! Hapo kusubiria haina usumbufu hata kama ni mwezi!! Sasa mtu alijua anaripoti kazini na alitafuta nauli ya kwenda tu tena kwa kukopa akijua akipokelewa atarudishiwa nauli na kupewa posho ya kujikimu!! Anachokutana nacho huko wengi wanajinyamazia huku wakiugulia maumivu makali moyoni!! Fikiria mtu hana nauli ya kurudi nyumbani, hana ndugu kwenye mji huo anafanyaje?
 
Tanzania ni nchi nzuri sana lakini waliopewa dhamana ya kushughulikia mambo mbalimbali kama maafisa utumishi hutesa sana watu!! Yaani mtu anaamua kujitoa ufahamu na kujifanya haoni tatizo lolote kwenye utaratibu huu!! Yaani mtu anaona haiwezekani mtu akose nauli!! haiwezekani akose pesa ya kujikimu!! Utafikiri ni mtanzania aliyeshuka kutoka mbinguni na haijui hali halisi ya baadhi ya watanzania wenzetu!! Nakumbuka huko nyuma mwanafunzi anaenda chuo akiwa amepata mkopo wa bodi ya mikopo ya wanafunzi halafu anakaa mwezi mzima kabla ya kupewa pesa hizo! Sasa unajiuliza hawa wanafikiri huyu mwanafunzi ataishi vipi wakati anasubiria boom? Ashukuriwe Mungu jambo hilo lilipewa ufumbuzi. Hili nalo naamini hawa miungu watu watashughulikiwa na mambo yatakuwa sawa. Cha maana tu ni kuwa tuendelee kupaza sauti!! Ninaamini hata baadhi ya viongozi wakubwa serikalini watashangaa kuwa kumekuwepo na utaratibu wa hovyo namna hiyo hapa tanzania kwa namna ambavyo waajiriwa wapya wanafanyiwa!!
 
Unarudije home kupumzika?anatakiwa kufika ofisini daily akisubir taratibu ziendelee,

Mimi nilipopewa barua yangu na Utumishi ofisi za maktaba pale 10 years ago,nilienda kuripoti kituoni,wakakagua vyeti,then wakanambia subiri,sikurudi home nikaongea na boss wangu wa wakati ule;nikachukua gest nikalipa wiki moja,nikifatilia malipo na nikiendelea kujifunza kazi,wiki ilipoisha hela ya gest ikakata,nikampeleka boss pale gest akanidhamin nikae wiki nyingine nikiprocess malipo,wiki ilofuata nikalipwa Ile laki tatu nikalipa deni la gest,na ofisin Kuna kazi ilipigwa nikajumuishwa nikalipwa kama laki 4.

Nikatafuta chumba nikalipa miezi 3,laki 3 manake ilikuwa chumba na sebule self,nikapewa godoro la kuanzia maisha na mama mwenye nyumba,na hapo ndipo maisha ya utumishi na kujitegemea yakaanza rasmi.Asante mama mcha kwa kunifadhil wakati ule mama,🙏(alikuwaga boss utumishi mkoa flan,sahivi ashastaafu)tukajenga na urafiki hadi leo 🙏
,
 
Aisee, uandishi huu...

Ulipangiwa wapi Mzee?

USHAURI: Rekebisha andiko lako. Ni refu na ingependeza likawa na paragraphs

I'm sorry if I have offended you anyway..
 
Aisee, uandishi huu...

Ulipangiwa wapi Mzee?

USHAURI: Rekebisha andiko lako. Ni refu na ingependeza likawa na paragraphs

I'm sorry if I have offended you anyway..
Kwanza inaonesha kuwa hujasoma andiko langu. Maana ungesoma ungejua kuwa ninaongea niliyoyaona kwa waajiriwa wapya! Kwa taarifa yako mimi ni mtumishi wa umma mstaafu!! Ninaandika hapa kwa manufaa mapana ya watanzania wanaonyanyasika kwenye ajira mpya!! Nimeandika kwa kirefu ili kutoa picha halisi ya tatizo. Shida ni kwamba kuna vwatu ni wavivu hata kusoma nusu ukurasa tu, wanaona ni taabu!! Ila kitu kizuri ni kwamba wewe ni mvivu pekee kati ya wasomaji karibia kama 40 hivi waliochangia kwenye uzi huu!! Jitafakari!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…