Chendembe
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 444
- 488
Nitangulize kupongeza wote waliohusika kubadili utaratibu wa kutoza adhabu za vyombo vya usafiri barabarani badala ya ule wa awali ambapo mahakama pekee ndio ilikuwa inatoza.
Hakika, walikuwa na nia njema ya kuondoa usimamaji wa vyombo vya usafiri kusubiri hukumu ya mahakama.
Pamoja na nia hiyo nzuri, watekelezaji wa sheria hiyo wamekuwa wakitumia nafasi yao vibaya na kusababisha kero kubwaaa kwa wasafirishaji/wasafiri na kuikosesha serikali mapato. Tatizo kubwa ni kukosa busara, hekima ,utovu wa nidhamu, na huruka za kujipatia kipato kwa baadhi ya Askari wetu.
Nadhani wanajiwekea malengo ya kukusanya kipato Chao zaidi kuliko cha serikali kwa siku.
Nashawishika pia kuamini labda baadhi ya vituo vya polisi yanakuwa ni malengo ya kituo kizima kwa vile sijawahi sikia mkuuu wa kituo yeyote kuwai kuwawajibisha askakali wa usalama barabarani. Mbaya zaidi, hata kama ukienda kituoni kulalamika juu yao, unazinguliwa tu.
Sio siri, yanajulikana mengi katikati idara hii ya polisi wa usalama barabarani.
Ivi wakuu wa kituo/RPCs hawajuwi michango ya siku wanayotozwa wasafirishaji wa abiria mijini maarufu daladala?
Nini kinatokea Kama hutoi michango hiyo?
Kuna nini Kati ya Traffic na vi carry, malori ya mchanga na hata mabasi yaendayo mikoani?
Wenzetu hawa hawana kushauri, kuelimisha Wala onyooo. Mwendo wa kutishia kuandikia makosa mawili au matatu.
Pamoja na lengo zuri lililokakusudiwa katika kuanzisha utaratibu huu, nashauri serikali iondoe mamlaka ya kutoza faini za barabarani kwa askali wetu kwakuwa inadhalilisha wananchi na kupelekea kupoteza Imani kwa jeshi hili.
Serikali ibainishe makosa ya kutozwa faini kuzuwia Tabia ya askali waovu kutunga makosa wapendavyo.
Ukaguzi wa magari uwe sehemu maalumu kuzuwia Askari waovu kufuata magari mbali ya miji na kutekeleza uonevu wao ili wapate kipato kama wafanyavyo Traffic was Tunduru ambako Traffic wanatoka na gari la binafsi nje ya mji na kukamata pikipiki/magari na kutoza faini kulingana na sura ya Mwenye chombo.