Hili swala lina changamoto kwa pande zote mbili...yaani kwa Wasimamizi wa sheria na Raia wenyewe.
Na chohote utakachopendekeza bado mtarudi palepale kwani watekekelezaji ni wale wale.
Na tuweke unafiki pembeni...hivi ni nani anapenda kutoa faini ya 30,000 au zaidi ya hiyo hata kama anakutwa na kosa?...kodi tu zenyewe tunalipa kwa kushikana mashati...sasa basi msisahau kuwa hata hao Trafiki wanatoka ndani ya Wananchi hao hao ila tu wao wamesimama upande wa pili wa uzio.
Sidhani kama hata wana haja ya kubuni kosa maana kwenye kila Gari kumi sidhani kama watakosa walau nusu ya hayo yenye kosa moja au jingine...na kama ni Muendeshaji wa mara kwa mara utagundua ya kuwa unaweza kukamatwa na Trafiki kwenye pointi A na usikutikane na kosa lakini kwenye pointi B ukaingia kwenye 18, huwa inategemea tu Trafiki unayemkuta ataulizia nini.
Na changamoto iliyopo ni kuwa ukijifanya Mjuaji ni wewe ndio upo kwenye nafasi ya kupoteza maana yeye pale yupo kazini anapopatia mshahara wake ili hali wewe labda ndio unaenda kazini kwako ukapate mkate wako wa siku.
Option pekee rahisi inayobaki ni kujishusha, kuomba msamaha na "kufinya" kaki au buku mbili asikuandikie 30,000, au pia usichelewe kazini au kwenye dili zako....na hapo pia ukute keshakusanya za malengo ya kiofisi (za sirikali) na sasa anahitaji tu ya mboga au ya kwenye kiti kirefu baada ya kazi.
Nilishawahi kung'ang'aniwa kisa tu kioo cha mlango hakishuki, nikaambiwa ni kosa na linakidhi kuandikiwa faini...kuna siku nikaambiwa tairi za nyuma zimechongwa niandikiwe...kuna siku nikaambiwa waipers zimechoka niandikiwe n.k.....kiufupi mambo ni mengi hivyo akikutaka atahakikisha hakukosi.