Kero za askari wa usalama barabarani: Utaratibu wa kutoza adhabu barabarani uangaliwe upya

Kero za askari wa usalama barabarani: Utaratibu wa kutoza adhabu barabarani uangaliwe upya

Lakini pia madereva wengi hawataki kufuata sheria za usalama barabarani.

Kwanini mnaendesha magari kwa mwendokasi?

Mwendokasi ni kosa la kisheria.

Hivi mnapataga muda wa kujitafakali kuhusu maisha?

Hivi mnawapenda wategemezi wenu?

Hata kama ninyi wenyewe pengine mmefika pa kujikataa na kwamba chochote kikitokea hamna cha kupoteza , Je vipi kuhusu wategemezi wenu hamna huruma nao? Mliwazaa waje wateseke wakose mahitaji ya msingi?

Maisha ya siku hizi siyo ya kutegemea ndugu akulelee mwanao wakati wake analea kwa mbinde.

Tutafakali zaidi.
Hivi wewe unamiliki hata pikipiki! Kwani adhabu za fine wanazotoza zinatokana na mwendo kasi pekee? Huna habari kuwa baadhi ya makosa wanayotoza fine ni kutokana na tafsiri potofu ya sheria?
 
Siku moja nipo safari na mutukaa yangu nikasimamishwa..! Wakati nataka maelezo ya kunisimamisha likapita gari la bwana mmoja mwenye asili ya mkoa wa Bukoba akiwa mafuta na Mark X yake nyeupe. Aliposimamishwa akaambiwa umezidisha mwendo, akauliza tu kosa ni hilo tu? Akaambiwa ndio! Akasema haya andika haraka..! Akapewa nyaraka yake ya malipo akaendelea na safari. Mimi nilibakia pale na muda ukaenda sana tukieleweshana.
Ninachotaka kusema ni kwmba baadhi ya madereva sisi, hasa wengi wetu hatupendi kutoa fine hata kama tunajua tuna makosa..! Ndio maana askari wanatumia mwaya huo kufanya yao.
Maendeleo ya nchi yanaanza na wewe..! Ukiambiwa una makosa na ukiandikiwa fine uwe na moyo mkunjufu wa kulipa fine, hapo tutapunguza maelezo nakuitana chemba.. Ambako mwisho wa siku kunazua kuchukiana na kurushiana maneno ya shombo...!
Shida sio Askari waadilifu, kuna watafuta makosa na Chao. Hao baba, hao. Makosa yao ni yakutengeneza.
 
Hivi wewe unamiliki hata pikipiki! Kwani adhabu za fine wanazotoza zinatokana na mwendo kasi pekee? Huna habari kuwa baadhi ya makosa wanayotoza fine ni kutokana na tafsiri potofu ya sheria?


Mfano makosa gani hayo?
 
Hivi wewe unamiliki hata pikipiki! Kwani adhabu za fine wanazotoza zinatokana na mwendo kasi pekee? Huna habari kuwa baadhi ya makosa wanayotoza fine ni kutokana na tafsiri potofu ya sheria?
Kweli mkuuu, kuna haha ya kubainishamakosa ya kutoza fine.
 
Na kuna mara nyingine Sheria za Barabani haziwataki Madereva, Kwa mfano unakuta Ishara na Alama nyingi zimefutika na Vibao havipo kabisa sasa hilo ni kosa la nani?


Lakini impliedly huwa inajulikana kuwa uwapo maeneo ya mijini speed limit ni ngapi na maeneo ya highway porini ni ngapi ?
Matharani kwa maeneo ya mijini wanasemaga isizi 50 kph na maporini isizidi 70-80 kph if not mistaken.

Sasa hiyo kila dereva anapaswa kuwa nayo in his or her mind hata bila kutegemea alama ya barabarani.

Au siyo?
 
Leo ukiwa na spare tyre za kujia, Askari wengine kwao ok, wengine ni kosa la fine, wanataka limu kubwa. Ukiwa na fire extinguisher ndogo wengine ok, wengine fine, ukibeba mchanga kama fire extinguisher hawaelewi, hawajuwi hata nini fire extinguisher.
Mara stika,, reflector... Mara ndogo, mara zimepauka. Ni kerooo.
Hakuna atakaelalamika kutozwa kosa linalokubalika
Mfano makosa gani hayo?
 
Kuna mmama Hapo junction ya Massana mweusi tii ana roho mbaya jaman[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yaan hatak maelezo wala chochote akikudaka anakuandikia na ikitokea una daiwa anaforce ulipe happhapo ili akuandikie nyingine
Ukidaiwa faini ya nyuma hakuna askari unachomoka siku hizi ,
Wana bonus unapolipa deni ,
 
Makosa ya barabarani yalitumika kama token ya kukusanya mapato , kwenye utawala wa tano
Hata ukusanyaji wa madeni kwa faini zilizobet kuna mapato yanaenda kama bonus kwa askari aliyekamata deni hilo, ndo maana kuna baadhi ya sehemu askari trafiki anakamata magari hata yaliyopaki na kuamuru yalipe

So its like a chain, askari wanaandika sana makosa ili watengeneze faida za kutosha wanapokamata magari yenye madeni na pesa ya bonus.

Mahakama ,zingekuwa huru , huu mchezo ungeisha
Bonus zifutyee hizoo, zinatudhalilisha
 
Lakini impliedly huwa inajulikana kuwa uwapo maeneo ya mijini speed limit ni ngapi na maeneo ya highway porini ni ngapi ?
Matharani kwa maeneo ya mijini wanasemaga isizi 50 kph na maporini isizidi 70-80 kph if not mistaken.
Sharia za wapi hizo! unaongelea hizo za Malori na Mabasi?
Una Gari dogo halafu wewe ni mgeni wa Barabara na unarukhsa ya kutembea hadi 120kph Barabara haina alama wala Vibao lakini imejaa Matrafiki na Mashine zao za faini
Huo ni uonevu dhidi yetu watumiaji wa vyombo
 
Ni wazi kuwa wapo askari ambao ni wasumbufu ambao hutafuta kumaliza stresses zao kwa madereva.

Pia kwa upande wa madereva kuna tatizo kubwa la kutofuata sheria za usalama barabarani bila shuruti.

Sasa kila upande ujitafakali na kujirekebisha.
 
Kulikuwa na haha gani kuweka penaiti ya adhabu ya fine 30,000= kuwa 15k ambayo no half way kwa wananchi tuliochoka hiviii!
 
Kuna gari ukiendesha hata kama ni jipya askari lazima akusumbue
Jaribu kuendesha kirikuu utakuja leta mrejesho

Haijui barabara huyo, ye anadhani ukitii sheria umemkwepa trafuki!!

Hapo Salenda hapo, kuna taa mbili sehemu fupi, hapo hapo kuna trafiki walafi hao!! Wanabambikia hao, yaan mi nimepita na green na wanyuma yangu watatu wakapita bado kang'ang'ania nimevuka na red!! Na anakomaa uso mkavuuu
 
Wanaingiza Mabilioni ya faini haramu lakini kununua Vibao vya Ishara na kupakaa alama za kwenye lami kunawashinda
susp.png
 
Wakati wa uongozi wa Mwendazake ajali zilipungua sana kutokea kama ilivyokuwa kwenye maswala ya kiharifu.

Mimi nakwambia jaribu kufuata sheria halafu askari akukamate kisha mwambia Mbona nimefuata sheria yote hayo unayoniambia ni usumbufu na kufanya nianze kufikiria unatengeza mazingira ya kutaka rushwa.

Kama kweli ukiwa mwaminifu kwenye mwendo wa kisheria na hayo maswala mengine ukimwambia hivyo anakuachia uende zako.

Tatizo madereva wengi wako rough !
 
Sharia za wapi hizo! unaongelea hizo za Malori na Mabasi?
Una Gari dogo halafu wewe ni mgeni wa Barabara na unarukhsa ya kutembea hadi 120kph Barabara haina alama wala Vibao lakini imejaa Matrafiki na Mashine zao za faini
Huo ni uonevu dhidi yetu watumiaji wa vyombo


Kumbe magari madogo yanaruhusiwa kisheria kwenda mwendo wa 120 Kph?

Basi kuna shida ya kisheria mahali.

Wengine mwendo usizidi 70-80 wengine 120 kph?!

Ipo shida.

Sheria iandikwe kwa uwazi .
 
Wengine mwendo usizidi 70-80 wengine 120 kph?!
70kph ni kwa Malori na 80kph ni kwa Mabasi Magari madogo ni mguu wako na kiwese chako kwenye tenki ila 120kph ni mwendo wa kujihami
 
Mfano makosa gani hayo?
Gari yako imekuwa registered kama private na ina uwezo wa kubeba abiria 6. Sasa unaamua kwenda shamba kubeba gunia zako mbili za mpunga, kwa kuwa haziwezi kuenea unatoa seat ya nyuma ili gunia zikae vizuri. Traffic polisi akikukamata anakutoza fine eti kwa nini umetoa seat na kuweka gunia za mpunga. Ukienda kutaarifu wakubwa wake wanabaki wanashangaa kuwa kwa nini huyo mwenzao hajui kuwa ile ni private na gari ina plate namba ya njano!
 
70kph ni kwa Malori na 80kph ni kwa Mabasi Magari madogo ni mguu wako na kiwese chako kwenye tenki ila 120kph ni mwendo wa kujihami


[emoji14][emoji14][emoji14]

Kumbe ndiyo hivyo? Seriously?!

Hatari!
 
Kama una gari Dogo tembea mwana


Mmnh hapana aisee!

Nina maono /Vissions zangu!

Kwa hiyo napaswa kujiangalia sana jinsi nienendeavyo na yanipasa kujifunza jinsi ya kujizuia na uharibifu unaweza kuepukika.

Ajali zinaepukika na kukingika.

Sitaki kubeti for life.

Magari ni vyombo vilivyotengenezwa na Wanadamu .

Hitilafu yawezajitokeza wakati wowote.

Hatakama utasema unafanya regular servicing bado huwezi kuwa na 100% assurance ya wale mafundi kule kama wamefanya kila kitu kwa ufanisi sababu ni Wanadamu kunaweza kuwa na -+ confidence level/error(s).
 
Back
Top Bottom