Kero za kudate mume wa mtu

Wee DA Anne ulimkomeshajee, huyo mubabaa,
Nimechekaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]r
 
Kuna mada niliona asbh

Ungekuwa wewe,ungemshauri nini huyu mtu?


Ameandika hivi;
""HabariNipo ktk fumbo sijui nini nifanya
Ni Mimi ni mtu wa imani,Kuna wakati nilipitia shida nikapiga goti nikamuomba Mungu aniinulie mtu wa kunisaidia
Baada ya mda akainuka mume wa mtu,Cha achabu vile vitu nilivyoomba yeye akavifanya Kwa asilimia kubwa.
Baadae nikawa najiuliza hivi aliyenijibu ni Mungu kweli ?

Nikawa siamini,nikawa nafanya juhudi niachane naye kwani kiimani ni dhambi,lkn Cha ajabu kila ninavyopambana kumuacha linatokea tatizo na anayelisolve ni huyo huyo.
Napambana Tena kumuondoa mara naota ndoto ikielezea huyo ni mtu mwemaaaa hautakiwi kumuondoa ktk maisha Yako.
Kiimani naona nakosea,lkn nifanyajee mwenzenu

Je niamini ni Mungu alimuinua,na wakati wa kumuondoa ukifika atamuondoa mwenyewe au nifanyajee Mana Kuna muda najiuliza kweli Mungu anaweza niletea married man kama msaada wangu?lkn nakumbuka nilioomba Kwa imani,nashindwa kumjudge Mungu,
Nimepitia MENGI MAGUMU,lkn aliyesimama na Mimi ni huyo peke yake
Amekuwa zaidi ya ndugu,
Japo sielew fumbo hili
Naomba watu wa imani mnisaidie fumbo hili mana Mimi nimeshindwa kulifumbua"
 

Attachments

  • Screenshot_20240921-212856.jpg
    437.1 KB · Views: 5
U see!umenipata ninachosema sasa...mcheps alikuwa fundi,akkakupagawisha alivyoweza,na mtoto akakuzalia see you now upo hapa UNASHUKURU unazeeka pamoja na mke wako
Ulitaka azeeke na mchepuko?
Utaota moto na uliyeokota nae kuni
Ndiyo maana amerudi kwa wife wake
 
Wee DA Anne ulimkomeshajee, huyo mubabaa,
Nimechekaaa [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]r
😂😂😂😂
Yaani mtu sijawahi kuwa na mazoea naye
Siku hiyo nikashangaa amenipigia..
Akauliza kwanza,upo Na nani hapo karibu?
Nikamwambiaa Niko mwenyewe..
Hee nikaona anatiririka wee
Matatizo yake yooootee.. toka anamtongoza huyo mkewe..mara anasema mkewe alimdanganya miaka
Amegundua eti ni mkubwa kuliko yeye
Aisee yaani nyie wanaume sio watu😂

Nikamwambia hakuna mtu ambaye hana matatizo.
 
Ni huyo huyo Mume wa mtu ameletewa na Mungu, kwa maombi yake. Lol
 
Wanaume wote tuliooa tungeamua kutulia tu na wake zetu majumbani, wasimbe wote mjini mngetembea na madera yenye viraka matakoni dadeq😡
😂😂😂 madera yanaraukaga makwapani kushuka chini. Ikirauka aaah, unachomekea chini ya ziwa na hivi ni mashangazi, ndala kiasi chake dera inakaa sawa sawa maisha yanasonga 🤣
 
Ninapochoka kwa waume za watu, kutoa siri za familia yao kwa mchepuko.
Najiuliza wanawezajee kufanya hivyo? Hawana hata uoga? Aibu je?
Aaaaah
 
Mungu hawezi kukuinulia mume wa mtu awe msaada kwako hata siku moja,kutembea na mume wa mtu ni dhambi ya USALITI,usaliti unaleta maumivu kwa msalitiwa,usaliti unaondoa upendo,usaliti unaleta chuki,usaliti unaleta roho ya kisasi,usaliti unaondoa amani,usaliti unaondoa baraka ...huyo dada hakutakiwa kuanza kutembea na mume wa mtu akiwa katoka kwenye maombi,alivyotoa tu hiyo nafasi alimpa shetani nafasi akajigeuza kama malaika wa nuru,hapo anadhani ni Mungu hapana,agizo la Mungu ni ndoa iheshimiwe...kama kweli ni mtu wa imani na maombi alitakiwa kujua pia namna ya kutafakari majibu kwa njia ya roho na sio njia ya mwili...binafsi ningemshauri pombe toba na rehema na aachane na huyo mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…