Kero za Muungano zimebadilika, What if Muungano ukavunjika?

Wakati mwingine unanishangaza, mbele ya kubakwa kote huku, unasema hivyo?
Wako wanaume wa aina mbili, aina ya kwanza ni wale wanaume wenye roho ngumu, vinganganizi ambao wakipenda, ni wamependa, hata mwanamke afanye vitimbi gani, hawaachi, mwanamke atagongwa, atakuwa gawa gawa, as long as amependwa, ataendelea kupendwa.

Type ya pili ni wale wanaume wenye roho ndogo, roho nyepesi, roho laini, mwanamke amepigwa tuu nje, yeye anaacha penzi linakufa.

Mimi ni ile type ya kwanza and this is my true story Enyi Waume, Wapendeni Wake Zenu!-Wife Kanirudia Saa12:00 asubuhi!-Bado Nampenda!

Na hii ni scenario ya huu muungano wetu Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?

P
 
Paskali, Pascal Mayalla, I am sure that's not you!!!!
 
Kikubwa tu ni fedha nyingi zinatoka bara kwenda visiwani na viongozi wengi walioko madarakani sasa hivi ni wazanzibari, Kama nchi ina Raisi wake kwanini itegemee fedha kutoka bara? Inamaana kama ilikuwa kwamba bara ndio ina support Zanzibar basi Zanzibar ilitakiwa kuwa Mkoa lakini sio nchi.
 
Nimesitushwa kuwa Tshs 50billion fedha za kutoka Bara ndio zinajenga uwanja wa AFCON Zanzibar, wakati huku mabarabara yana mashimo kibao nchi nzima.
CCM imekaa kama mfu!
 
Nimesitushwa kuwa Tshs 50billion fedha za kutoka Bara ndio zinajenga uwanja wa AFCON Zanzibar, wakati huku mabarabara yana mashimo kibao nchi nzima.
CCM imekaa kama mfu!
leo hii gerezani kariakoo pale katikati ya jiji mitaro inatoa uchafu na harufu mbaya tena barabara ni mbovu sio masihara halafu tunashindwa kufanya maendeleo in the expense of someone else
 
Ukitaka kujua Nyerere hakuwa kiongozi mzuri kihivyo kama wanavyomsifia just angalia muundo wa huu muungano ulivyo ni obvious Nyerere alikurupuka, Tanganyika haipo ila Zanzibar ipo
kwa sasa wao wanamaraisi wawili kwa mpigo tanganyika hakuna.
Ni bora mfumo ungekuwa wa marais wawe watatu.

Na sis tungekuwa na rais wa tanganyika
 
Baada ya October 29 utaifa na mjadala wa Muungano umeibuka kwa kasi na sasa ni Ajenda ya maandamano yajayo, yakifanyika hata kidogo kukawa na na mabango ya kutaka Tanganyika, italeta hisia mpya kabisa kwenye siasa za Muungano
 
Tanganyika haina mwenyewe.
Na ndio maana watu wajinga wajinga kama Mzanzibari Simai wanaweza kutoa uharo wao hata Bunge letu Tukufu na hawafanywi lolote.
 
Paskali, Pascal Mayalla, I am sure that's not you!!!!
Mkuu Jidu, Jidu La Mabambasi , kumbe wewe hutujui Wasukuma tukipenda!,
This is me
and this is my true story Enyi Waume, Wapendeni Wake Zenu!-Wife Kanirudia Saa12:00 asubuhi!-Bado Nampenda!

Na hii ni scenario ya huu muungano wetu Tangu lini Mke Ndani Ya Ndoa Akaomba Uhuru ili Kutoka Nje Ya Ndoa? Aruhusiwe?

Tena sio mimi tuu, we hujawahi sikia story fulani ya Chifu Burito na mambo ya kupenda? Baba Mzazi wa Mwalimu Nyerere, Chief Burito alioa wake 22. Je, alikuwa na Watoto Wangapi?
P
 
Mkuu namjua Jidu kuwa ni msukuma pori, tena wa huko Ngudu!
Sidhani kama anaweza kukubaliana nawe katika suala hili.

Naungana na Jidu kwa kusema kuwa nchi imefitinika.
Watu wasio waTanganyika wanainyonya literally Tanganyika dry.
Si kitu cha kujivunia hicho.
Walati vijana wetu wanaomaliza vyuo vikuu, wakuu wa wilaya ni Wazanzibari, wakurugenzi wa Halmashauri zetu wazanzibari.
Kama huamini nenda Kinondoni.
Wapi na wapi?
Fedha zetu zinaenda kusiko, lini fedha za Zanzibar zikajenga hata hospitali huku Bara?
Utacheka na kukubali situation hii?
Usipoelewa hili basi unajikuta kuwa ni fala la mjini.
 
Mkuu nikiri kuwa sijakuelewa!
Unajaribu kuififisha mada iliyo mbele yetu kiaina!
 
Nimesitushwa kuwa Tshs 50billion fedha za kutoka Bara ndio zinajenga uwanja wa AFCON Zanzibar, wakati huku mabarabara yana mashimo kibao nchi nzima.
CCM imekaa kama mfu!
Mkuu Maso, masopakyindi , unashitushwa nini?, hujui kupenda wewe?, mara ngapi sisi wanaume, una mu entertain demu, huku nyumbani kwako kuna hali ngumu?
Zanzibar ni kama mke, mara ngapi unajenga kwa wakwe kabla ya kwenu?.
Kwa taarifa tuu, Tanzania mbale ya Zanzibar, ni tunawapenda kwa penzi mshumaa, unamulikia wengine huku kwako unateketea, au penzi mama maboga, anasuka sana mikeka, lakini watoto wake wanalala chini!.
Kwa vile hakuna elimu yoyote kwa umma inayofundishwa kuhusu huu muungano wetu, Zanzibar ina haki zote za JMT kama sehemu nyingine yoyote, over and above ule mgao wake wa asilimia 4.5% ya mikopo yote na fedha za misaada ya wafadhili.

Sijui tuna wanaume wa aina gani siku hizi unamuonea wivu mke wako kumpendezesha?

P
 
Kwani hoa wazanzibery wako wangapi kwenye mkoa wao naona kama wanatuchosha tuu🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️
 
Basi niambie tu
Mke wako ana kusanya na kulipa kodi?
Mkeo ana pelka pelka fedha kwa kificho kwa mahawara zake?
Mke anajenga hospitali na mabarabara
Mkeo kawaida ya kupeleka pesa kusiko julikana?
Mbaya zaidi mkeo ana kawaida ya kuwatesa, kuwateka na kuwaweka ndani watu?
Mkeo ana tabia ya kuwa na mahusiano nje ya makubaliano na watu wengine?
Mkeo anaua tu bila huruma na ukimuuliza atakwambia we mzee una drama?
Mkeo ana tabia y ya kukucharaza bakora hadharani au kutumia mawifi zako kukuita Yuda Msaliti

Kama huyondo mkeo nawe unaridhika naye ije mvua lije jua , basi nikupe pole tu!
 
Ntu yeyote anafikiri suruhu yeye ni kutengana ni Donat yake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…