UTANGULIZI
Tanzania ni miongoni mwa nchi kubwa(kwa eneo na idadi ya watu) barani Afrika.Ni nchi iliyojaliwa rasilimali nyingi na za kutosha,imejaliwa kuwa na watu wenye akili na vipaji.Aidha Tanzania ni kisiwa cha amani.Pamoja na utajiri huo ,bado nchi yetu inachangamoto lukuki.Umasikini,ukosefu wa ajira,uzalishaji hafifu,ukusanyaji wa mapato kidogo,Huduma za kijamii duni na changamoto zingine nyingi.
Ili kuondoa kero hizo ,natamani Tanzania yangu iwe hivi ndani ya miaka 5-10 ijayo.
1. ILI KUBORESHA SEKTA YA KILIMO NA MIFUGO(UTI WA MGONGO WA UCHUMI WA NCHI) NAPENDEKEZA;
SERIKALI IPUNGUZE MUDA WA KUSTAAFU KUTOKA MIAKA 60-55 . Hii itapunguza tatizo la ajira kwa kiasi chake kwani vijana nao watapata fursa ya kushika nafasi zilizoachwa na wastaafu. Kadhalika ili kutowatelekeza wastaafu serikali inaweza ikawa inatoa mafunzo ya namna ya kujikimu baada ya kustaafu. Mafunzo haya yanatakiwa yafanyike miaka 5 ya mwisho ya kuelekea kustaafu. Katika kipindi cha mwisho cha kustaafu,wastaafu wakutanishwe na wataalamu mbalimbali ambao watawapa ushauri juu ya maisha ya uzeeni sambamba na namna nzuri ya kutumia fedha zao za kiinua mgongo.
6. ILI KUBANA MATUMIZI YA SERIKALI NAKUONGEZA MAPATO, NAPENDEKEZA PIA,
Naishukuru jamii forums kwakuja na wazo hili la stories of change.
NAOMBA KUWASILISHA

- Kuanzishwe kliniki za kilimo na mifugo kila kijiji.Kliniki hizi ziwe na wataalamu na vifaa kwa ajili ya tiba ,uzalishaji na ushauri kwa wakulima na wafugaji.Wataalamu hawa kazi yao kubwa itakuwa ni kuhakikisha kuna uzalishaji wenye tija kwenye maeneo yao ya kazi na watathiminiwe kwa kigezo hicho.Wazo hili litaleta faida zifuatazo. ajira kuongezeka(takribani ajira 38,000 za maafsa mifugo na kilimo zitatengenezwa nchi nzima).Uzalishaji utaongezeka,pato la mwanachi litaongezeka na serikali itaongeza mapato.Ajira binafsi pia zitaongezeka.
- MAAFISA WA KODI (WALAU WAWILI)WA AJIRIWE KILA KIJIJI/MTAA. Kazi kuu ya maafsa hawa itakuwa ni kutoa elimu ya kulipa kodi, faida zake na aina ya kodi kwa rika zote. Jamii nyingi hazijui maana ya kodi,wengi hudhani kulipa kodi ni kuonewa au kunyonywa kumbe ni wajibu.Elimu ya kodi ikimfikia mwananchi mmoja mmoja, serikali itapata mapato ya kutosha kuhudumia nchi.Kodi hiyo katika ngazi ya kijiji ikusanywe kwa mtindo huu; Kutokana na ugumu wa matumizi ya EFD, kuwepo na vitabu maalumu vya stakabadhi ambavyo vinatolewa na TRA kwa wafanya biashara, ambapo wafanyabiashara watalazimika kutoa stakabadhi hizo kwa wanunuzi mara baada kuuziana bidhaa. Kila mwezi wafanyabiashara watatakiwa kuwasilisha vitabu hivyo vya stakabadhi kwa maofsa wa TRA wa kijiji/mtaa kwa ajiri ya kukadiriwa kodi na kulipa. Maofsa wa TRA wa kijiji/mtaa watakuwa na mfumo maalumu wa tehama ambao utatuma majumuisho ya kodi kwenye ngazi za juu. Faida ya wazo hili ni kwamba, tutakuwa tumetengeneza ajira za kutosha kwa ma afsa kodi lakini pia mapato mengi ya kodi yatakusanywa na hivyo nchi kuweza kuhudumia raia wake ikiwemo na kuwa na uwezo wa kulipa mishahara.Hi pia itarahisisha ukusanyaji wa kodi ya majengo.
- Kila kata/kijiji/mtaa kiwe na afsa masoko.Kazi kubwa ya afsa masoko iwe ni kuwatafutia masoko na fursa wananchi wa eneo analo fanyia kazi.Hali hii itapunguza kero kubwa ya wananchi kukosa masoko ya bidhaa zao wanazozalisha.Ma afsa masoko watatakiwa kuwa wabunifu ili kuhakikisha wana nchi wanapata sehemu ya kuuza bidhaa zao kwa bei yenye tija. Wazo hili pia litaongeza nafasi ya ajira hasa kwa ma afsa masoko sambamba na sekta nyingine zisizo rasmi kukua.
- KILA KIJIJI/MTAA KUWEPO NA AFSA ARDHI NA AFSA SHERIA MMOJA. Kazi kubwa ya watu hawa itakuwa ni kuhakikisha ardhi ya eneo wanalofanyia kazi imepimwa na kuthaminiwa. Na hivyo kupunguza migogoro ya ardhi. Watashirikiana pia na ma afsa kodi kuhakikisha kila mwananchi analipia kodi ya ardhi kama inavyotakiwa. Faida ya wazo hili, ajira za ma afsa ardhi na sheria zitaongezeka na serikali itaongeza mapato yake kupitia ardhi.Kadhalika utapeli wa viwanja na mashamba utakoma.
SERIKALI IPUNGUZE MUDA WA KUSTAAFU KUTOKA MIAKA 60-55 . Hii itapunguza tatizo la ajira kwa kiasi chake kwani vijana nao watapata fursa ya kushika nafasi zilizoachwa na wastaafu. Kadhalika ili kutowatelekeza wastaafu serikali inaweza ikawa inatoa mafunzo ya namna ya kujikimu baada ya kustaafu. Mafunzo haya yanatakiwa yafanyike miaka 5 ya mwisho ya kuelekea kustaafu. Katika kipindi cha mwisho cha kustaafu,wastaafu wakutanishwe na wataalamu mbalimbali ambao watawapa ushauri juu ya maisha ya uzeeni sambamba na namna nzuri ya kutumia fedha zao za kiinua mgongo.
6. ILI KUBANA MATUMIZI YA SERIKALI NAKUONGEZA MAPATO, NAPENDEKEZA PIA,
- Magari yote ya serikali yatumie nishati ya gesi
- kila mtu alipe kodi
- Mtu asiteuliwe kushika nyadhifa mbili za uongozi kwa wakati mmoja(wapewe na wengine provided wana sifa)
- Mawaziri na manaibu waziri wasiwe wabunge na kinyume chake.
- Wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wapimwe kwa ubunifu wao wa kuleta ustawi na maendeleo katika maeneo yao ya utawala na si kwa vitisho.
- Elimu bila malipo iondolewe pia,Angalau wazazi wachangie tsh 50,000/= kwa mwaka kama ada. Hii italeta ahueni kwenye shule, hasa ukizingatia mabadiliko ya sera ya elimu ya sasa.Ambayo inahitaji gharama kubwa kuutekeleza mtaala.Pia napendekeza ruzuku inayotolewa sasa na serikali ibadilishwe na kuwa posho kwa walimu.Shule zihudumiwe na ada za wanafunzi.
- Ili kupunguza umasikini kwa wafanya kazi,bodi ya mkopo ipunguze asilimia za makato yake kwa wanufaika wa bodi ya mikopo angalau mpaka asilimia 5.Hii itapunguza maumivu wanayoyapata wanufaika na kuleta unafuu kwenye mishahara ya wanufaika.
Naishukuru jamii forums kwakuja na wazo hili la stories of change.
NAOMBA KUWASILISHA
Upvote
4