Kero za nyumba za kupanga: Wamama wanaoshinda vibarazani/ makoridoni kwenye mikeka wanakosesha amani wapangaji wengine

We hatari mzee
 
Pale keko palivyokaa ovyo wanakaa karibu na choo kuchafu wameweka mkeke wanapiga story wengine wanasukana..Kuna jamaa aliingia chooni alikuwa anaharisha alipotoka wakawambia "polee" jamaa alihisi aibu sana
 
Mkuu,bora umeme na maji,mimi nimejikuta mfukoni mweupe baada ya kula tunda kimasihara na mtoto wa faza/hs na akaniachia UTI sugu na doz za sindano za kutosha
Bado kuna sindano ya hayo makitu? Si kuna AZUMA? [emoji23][emoji23]
 
Kuna nyumba nilihama baada ya mwezi tu kutokana na wamama. Kuna mama mmoja alikuwa mlokole akiniona tu naingia ndani anakuja kunipa ratiba za kanisani kwake na kunishauri niokoke.

Mara aniletee kikombe cha baraka chenye picha ya mchungaji wao.Mwanamke akija kunitembelea anakuja kuniuliza huyu ndiyo mkwe? Ukimjibu sio anasema hata kama ni yeye okoka Mungu akuoneshe ubavu wako.

Nikaona isiwe tabu ngoja nihame tu na kikombe chake nikakiacha.
 
Panga Nyumba ya pekee yako mkuu
 
Mwamba ulikosea, ungejifanya umempokea bwana.Mngefanya maombi ya pamoja.Hakika ungeiyona hazina.
 
huyo ungemletea pigo za kibedui unamvuta geto unampelekea moto yy mwenyewe ataacha mazoea
 
si useme tuu kwamba wanapenda kujifunga kanga moja tuuu ama wanavaa dera bila nguo zingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…