Habari zenu ndugu zangu wa jamiiforums.
Kesho (30-03-2021) ninaenda kufanya "Oral Interview" kwenye N.G.O moja huku Dar. Niombeeni kwa Mungu ndugu zangu mtaani maisha ni magumu sana.
Tulifanya written Interview tukiwa watu 20, tumechujwa na kubaki 9 ambao kesho ndio tunapambania kombe ili wawili waibuke kidedea na 7 watakaobaki warudi tena mitaani kupambana na maisha. Je, Infantry Soldier atavuka Interview hii na kuachana na biashara yake ya kuendesha Taxi Bubu?
Mwambie Mungu anisaidie nivuke salama challenge hii kwa maana mshahara wa hawa jamaa zangu ni mnono kweli kweli.
Maisha yamekuwa magumu sana huku uswahilini kwetu. Ninatamani hata kuuza hii Taxi bubu yangu (Chaser Avante GX-100) nifungue walau pub ndogo. Sasa ni karibia mwezi wa saba huu tangia nianze biashara hii ya kuendesha Taxi bubu. Nilianza mwezi wa tano (May) mwaka huu wa 2020. Biashara imekuwa...