Kesho (30-03-2021) ninaenda kufanya "Oral Interview" kwenye N.G.O huku Dar. Niombeeni kwa Mungu ndugu zangu, mtaani maisha ni magumu sana

Kesho (30-03-2021) ninaenda kufanya "Oral Interview" kwenye N.G.O huku Dar. Niombeeni kwa Mungu ndugu zangu, mtaani maisha ni magumu sana

Kila la Kheri. Mungu akutangulie.
oo my love kumbe so wewe kuna jamaa anaitwa Bujibuji alikuja hapa na kutuambia umefariki, kumbe sio wewe. nimekuona hapa hadi machozi ya furaha yamenitoka kabisa...huyu jamaa ni muongo sana,mbaya zaidi ile namba yako haipatiani.
klichokuwa kimebaki cha kunipa matumaini ni huyo wa TBC na wewe sio ila nilijiuiza sana sana ni lini umeanza kazi TBC.
PLEASE nitumie namba yako ya sasa, Moyo wang utulie.
 
Mungu anao watu wengi sana mitaani ambao kesho watafanya intaviu na wote hao aliwaambia wajisaidie wenyewe naye atswsaidia, hivyo ni jukumu lako kijisaidia, ila ukitaka nikuombee tuma mgao wangu kabisa maana mkipata mnajificha.
ni kitabu kipi Mungu ameyasema hayo ya kwako?
 
Nafikiri huwa wanauliza kwanza kujua value yako ( unajithaminisha vipi ), kutokana na ulicho nacho kuanzia uzoefu wake, na elimu yako. Pili watakupa mshahara ambao upo kwemye scale husika katika nafasi husika, ila kama wamekuita kama mtu special mnaweza vutana na wakakupa unachotaka au mnaweza kukubalina some terms.
Oohh Sawa
 
Habari zenu ndugu zangu wa jamiiforums.

Kesho (30-03-2021) ninaenda kufanya "Oral Interview" kwenye N.G.O moja huku Dar. Niombeeni kwa Mungu ndugu zangu mtaani maisha ni magumu sana.

Tulifanya written Interview tukiwa watu 20, tumechujwa na kubaki 9 ambao kesho ndio tunapambania kombe ili wawili waibuke kidedea na 7 watakaobaki warudi tena mitaani kupambana na maisha. Je, Infantry Soldier atavuka Interview hii na kuachana na biashara yake ya kuendesha Taxi Bubu?

Mwambie Mungu anisaidie nivuke salama challenge hii kwa maana mshahara wa hawa jamaa zangu ni mnono kweli kweli.

Tatizo unapoteza sana muda JF.
Tatizo ninaendesha Taxi na abiria hakuna kama zamani sababu ya bajaj zimekuwa nyingi. Nisipopiga story JF nikapige wapi?
Tafuta kijiwe kingine ili muda unaoupoteza JF uingize ngawira. Unaweza kutumia hii smartphone ikakuingizia kipato
 
Tatizo ninaendesha Taxi na abiria hakuna kama zamani sababu ya bajaj zimekuwa nyingi. Nisipopiga story JF nikapige wapi?

Kwani ni lazima ung’ang’ane mjini tu! Jiongeze, sisi tulioko vijijini na pembezoni na miji mbona tunaishi vizuri tu kwa kujilimia mashamba, bustani n.k. Mentality ya kupenda kukaa mijini na huna pesa ndiyo itakufanya uendelee kujuta! Asilimia kubwa ya watanzania tupo vijijini vizuri kabisa bila pressure yoyote! Mnaopenda kukaa mijini na wakati hamna kazi yoyote ya kufanya mkisubiri kuajiriwa tu kaeni tu, lakini siku moja hadi mawe yayasema!
 
Sawa mkuu
 
Kwani ni lazima ung’ang’ane mjini tu! Jiongeze, sisi tulioko vijijini na pembezoni na miji mbona tunaishi vizuri tu
Sio kila anayekaa kijijini ana maisha mazuri. Mimi nimefanya kazi Morogoro na Simanjiro vijijini miezi sita kwa kila kijiji nimeona umasikini wa kutisha yaaani baba, mama na watoto wanalala chumba kimoja.

Wenye maisha mazuri vijijini ni 3% tu ya wakazi wa huko. Wengi wao ni walevi wa kutupwa. Labda wewe ni sehemu ya hiyo 3% na usiaminishe watu eti woooote wanaokaa vijijini wana maisha bora
 
Basi endelea kutamba hapo mjini hadi siku moja mawe yataongea! Sasa mnatuletea pumba huku ili tuwasaidie nini! Kama kijijini kunawaka moto basi mjini ndiyo kunawaka moto zaidi! Kijijini hatupangi nyumba. Huko mjini utapanga na nini wakati huna kitu! Rudini vijijini haraka sana tuwape mashamba ya kulima!
 
Asilimia kubwa ya watanzania tupo vijijini vizuri kabisa bila pressure yoyote!
Uongo huu mkuu. Asilimia kubwa ya wakazi wa vijijini wanaishi katika umasikini wa kutupwa. Ninaendaga likizo kijijini hivyo ninaifahamu hali halisi ya huko.

Wenye unafuu wa maisha ni 3% pekee ya wakazi wote huku wengi wao wakiwa ni watumishi wa serikali kama walimu, askari pamoja na maafisa kilimo/mifugo.
 
Basi endelea kuonyeshana ubavu na jiji lakini siku moja hadi mawe yatasema!
 
Back
Top Bottom