Kesho (30-03-2021) ninaenda kufanya "Oral Interview" kwenye N.G.O huku Dar. Niombeeni kwa Mungu ndugu zangu, mtaani maisha ni magumu sana

Kesho (30-03-2021) ninaenda kufanya "Oral Interview" kwenye N.G.O huku Dar. Niombeeni kwa Mungu ndugu zangu, mtaani maisha ni magumu sana

Tunawaombea wote 9. Hakuna kufanya ubaguzi wa maombi kwa Mungu.
Habari zenu ndugu zangu wa jamiiforums.

Kesho (30-03-2021) saa 4 asubuhi ninaenda kufanya "Oral Interview" kwenye N.G.O moja huku Dar. Niombeeni kwa Mungu ndugu zangu mtaani maisha ni magumu sana.

Tulifanya written Interview tukiwa watu 20, tumechujwa na kubaki 9 ambao kesho ndio tunapambania kombe ili wawili waibuke kidedea na 7 watakaobaki warudi tena mitaani kupambana na maisha. Je, Infantry Soldier atavuka Interview hii na kuachana na biashara yake ya kuendesha Taxi Bubu?

Mwambie Mungu anisaidie nivuke salama challenge hii kwa maana mshahara wa hawa jamaa zangu ni mnono kweli kweli.

 
Wewe tayari una ajira. Inawezekana wenzako hawana hata simu janja ya kuwawezesha kuingia JF.
Huo uwezekano umeujulia wapi? Vp kama wao pia wapo humu JF lakini hawaamini katika nguvu za Mungu?

Vp kama pia walikuwa nazo simu janja ila wakahonga kwa wanawake zao. All in all, niombee kwa maana ninataka kuachana na kuendesha Taxi kwa maana hainilipi vizuri sasa hivi.
 
2018 niliitwa pia kweny NGO moja hivi ipo kule ushuani
Nilifanya written interview na oral siku hiyo
Baada ya week mbili niliitwa tena kufanya Oral ikiwa ni ya Pili hii ukiacha ile ya kwanza hii ilijikita zaidi kweny taasis husika na bada ya interview nilipata nafas ya kufahamishwa miradi iliyo kua ikisimamiwa na hiyo NGo pia nilipata kufahamu taratibu zote za ofice husika na jamaa wali niambia kabisa kua we ndo mtu tunae kuhitaji kwa hiyo ume fit hii nafas nikapewa ahadi ya kupigiwa simu j3 nifike ofis husika na vyeti na ishu nyngnezo za kiofis bas nika ondoka pale nikiwa natumain kubwa kua ile kazi. Nime ipata na ukizingatia nili fanya vzur zile interview zote
Ajab j3 ilifika nikawa nasubiri sim yao naona kimyaaa
Nika subir mpka saa10 jion kimya na
Uzuri nilikua nime save namba ya alie niita interview ile ya kwanza bas nika mpigia j4 nakumueleza kua interview ya mwisho mli ahidi kunipigia j3 lakini haikua hivo na leo n j4 mbona kimya
Bas nilijibiwa subiri tuta kupigia kinyonge sana nili pokea ile kauli yake na kusema acha nisibir nika subir sasa yapata miaka 3 [emoji23][emoji23] nime ona huu uzi wako bas ndo ume nikumbusha ili tukio hili ..
kikubwa hii ili nifanya nikate tamaa ya kuajiriwa na zaidi tu nifocus na biashara zang mdogo mdogo najua ntatoboa
Mm pia ilinitokea hii hadi HRM ananoambia karibu on board na haya ndio mazingira utakayokuwepo lol mwisho wa siku napokea email We regret to inform you,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom