Kesho 31/3/2015 Ndio Uzinduzi wa Kampeni ya NDIO/HAPANA kwa Katiba pendekezwa.

Kesho 31/3/2015 Ndio Uzinduzi wa Kampeni ya NDIO/HAPANA kwa Katiba pendekezwa.

Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2007
Posts
18,772
Reaction score
8,939

Kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni kampeni za NDIO na HAPANA zinaanza
Kesho tarehe 31 Machi, maana kampeni ni siku 30 kabla ya siku ya kupiga kura ya maoni ambayo ni Aprili 30.

Je unaijua kamati yako ya ndio au hapana?

Je mmetangaziwa lolote na Tume ya Uchaguzi juu ya kuanza kwa kampeni?

Kama hapana,

kataa mwenendo wa maisha ya kuvunja sheria, kwa namna maandalizi yalivyo hatuwezi kuwa na Kura ya Maoni bora.
 
kila siku tbc wanarusha hiyo ndiyo kampeini ndugu

Mkuu hao watakuwa wamevunja sheria ambayo ilipitishw Bungeni, na kesho ndio Rasmi siku ya kwanza Ya kampeni ili kura iweze kufanyika Tarehe 30/4/2015, na hili lisipo fanyika Maana yake ni Sheria Imevunjwa na nadhani itabidi sheria irudishwe bungeni na Tarehe mpya Ipangwe ili kampeni zianze na tarehe mpya ipangwe.
 
Nina mashaka kama wewe ni mtanzania. maana sisi tunajua nchi inavyoendeshwa. pia tambua katika hatua za kusonga mbele huwa 0,+1 au 0,-1 huvyo zote ni hatua. sisi tunapiga hatua kwa kurudi nyuma.
 
Mimi nauliza tu, watu wameshaandikishwa wote?? na sheria ilisema lazima ziwepo siku 60 za elimu kwa wananchi ili waielewe na hilo lilikuwa jukumu la tume ya uchaguzi, sasa zimekuwa siku 30?? Lubuva anasema siku 30 wanaweza waandikisha maliza watanzania wote?? Hii nchi tuna matatizo makubwa sana, na kwa mwendo huu tutabaki omba omba milele yote.. vitu vya muhimu hatuna maandalizi, lakini vitu vya kijinga kama kukimbiza mwenge, sijui ..day, hizo pesa zake huwa zipo na zinaandaliwa mapema tu...
 
Mimi niko kundi la Banana (Ndizi); vipi mwenzangu? Chungwa au? Kimsingi, kama magamba wangeendesha mchakato inavyotakiwa, Katiba ilitakiwa kuwa na makundi mawili tu - NDIO au HAPANA. Lakini saa hizi kila mtu anaongea lake:-

(a) Kuna wa NDIO (magamba and the like)
(b) Kuna wa HAPANA (Maaskofu)
(c) Kuna waliosusa (UKAWA)
(d) Kuna undecided (Masheikh wa Kadhi)
(e) Kuna wasio na mpango (wanaouza nyaraka za nchi kwa tende)
(f) n.k.
 
nina mashaka kama wewe ni mtanzania. Maana sisi tunajua nchi inavyoendeshwa. Pia tambua katika hatua za kusonga mbele huwa 0,+1 au 0,-1 huvyo zote ni hatua. Sisi tunapiga hatua kwa kurudi nyuma.

sisi tunapiga hatua kwenda mbele na ndiyo maana mchakamchaka wa kuelekea kuipigia kura katiba inayopendekezwa unaendelea huo ndio mpango mzima.
 
kwa mujibu wa sheria ya kura ya maoni kampeni za ndio na hapana zinaanza
kesho tarehe 31 machi, maana kampeni ni siku 30 kabla ya siku ya kupiga kura ya maoni ambayo ni aprili 30.

je unaijua kamati yako ya ndio au hapana?

Je mmetangaziwa lolote na tume ya uchaguzi juu ya kuanza kwa kampeni?

Kama hapana,

kataa mwenendo wa maisha ya kuvunja sheria, kwa namna maandalizi yalivyo hatuwezi kuwa na kura ya maoni bora.

kura ya ndiyo haiepukiki kwa jinsi watanzania walivyo na shauku ya kuiona tanzania mpya yenye neema isiyofungamana na ubaguzi,udini na ukabila.

Hima watanzania tujiandae kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa ya taifa na vizazi vyetu.
 
katiba ishafeli,hakuna kitu

christine nakuonea huruma maana umeingia kichwakichwa na kisha kuropoka katiba imeshafeli bila kueleza imefeli kivipi? Acha kujilisha upepo hili goma linasonga kwa spidi ya ajabu we kalia kuzubaa unakosa kuungana na mamilioni ya watanzania watakaoiunga mkono katiba pendekezwa.

Epuka kupoteza kura yako!
 
mimi niko kundi la banana (ndizi); vipi mwenzangu? Chungwa au? Kimsingi, kama magamba wangeendesha mchakato inavyotakiwa, katiba ilitakiwa kuwa na makundi mawili tu - ndio au hapana. Lakini saa hizi kila mtu anaongea lake:-

(a) kuna wa ndio (magamba and the like)
(b) kuna wa hapana (maaskofu)
(c) kuna waliosusa (ukawa)
(d) kuna undecided (masheikh wa kadhi)
(e) kuna wasio na mpango (wanaouza nyaraka za nchi kwa tende)
(f) n.k.

wee dudus na christine msiwe viraka nyie, mnajifanya maduduwasha! Hayo makundi mnawapangia watu gani na kwa mamlaka ya nani, msipoteze muda wenu mkaja kujilaumu siku ya kupiga kura mtakapojikuta mko 2, tumieni akili acheni kuchepuka nyie.
 
Mimi nauliza tu, watu wameshaandikishwa wote?? na sheria ilisema lazima ziwepo siku 60 za elimu kwa wananchi ili waielewe na hilo lilikuwa jukumu la tume ya uchaguzi, sasa zimekuwa siku 30?? Lubuva anasema siku 30 wanaweza waandikisha maliza watanzania wote?? Hii nchi tuna matatizo makubwa sana, na kwa mwendo huu tutabaki omba omba milele yote.. vitu vya muhimu hatuna maandalizi, lakini vitu vya kijinga kama kukimbiza mwenge, sijui ..day, hizo pesa zake huwa zipo na zinaandaliwa mapema tu...

ACHA KUTUSUMBUA NA MASWALI YAKO YA KIZUSHI NENDA KAWAULIZE TUME YA UCHAGUZI,WENZIO TUNAJIANDAA KUPIGA KURA WEWE USIWE KAMA FISI ALIYEALIKWA HARUSI 2 akashindwa kuatend zote kwa kukalia kumangamanga.
 
christine nakuonea huruma maana umeingia kichwakichwa na kisha kuropoka katiba imeshafeli bila kueleza imefeli kivipi? Acha kujilisha upepo hili goma linasonga kwa spidi ya ajabu we kalia kuzubaa unakosa kuungana na mamilioni ya watanzania watakaoiunga mkono katiba pendekezwa.

Epuka kupoteza kura yako!

yani nawewe kwa akili yako unataka kuipigia kura ya NDIO katiba ya joka lenye makengeza?
 
tunaenda kwenye kura ya maoni kwa vitambulisho vipi? Vipya au vya zamani?

kama lilivyo jina lako we zero kweli na sio mfuatiliaji wa taarifa za nchi yako kiasi kwamba hujui nini kinaendelea sasa kwa kukusaidia nenda tume ya uchaguzi utapata data usituchafulie hali ya hewa humu.
 
yani nawewe kwa akili yako unataka kuipigia kura ya ndio katiba ya joka lenye makengeza?

huyo mtu unayemtaja ndugu hana katiba, katiba ni ya serikali tu na sio ya mtu mwingine zaidi, yeye alikuwa mchangiaji kama wengine kwenye kamati yake
 
Back
Top Bottom