Kesho 31/3/2015 Ndio Uzinduzi wa Kampeni ya NDIO/HAPANA kwa Katiba pendekezwa.

Kesho 31/3/2015 Ndio Uzinduzi wa Kampeni ya NDIO/HAPANA kwa Katiba pendekezwa.

sasa mbona hamtoi hiyo elimu, me nnachoona hapo mtu akitotofautiana na mawazo yenu tu mnampa mipasho badala ya kumpa hiyo elimu.

Mtu akitofautiana na mnachikiamini haitakiwi mumshambulie ila inatakiwa mumjibu kwa hoja huo ndo u'great thinker

duu pole ndugu, lakini si umeshaisoma katiba inayopendekezwa surazote 19?
 
Jamaa kauliza vizuri tu!
Tunaenda kwenye kura ya maoni kwa vitambulisho vipi? Vipya au vya zamani?
ona wewe ulivyomjibu!

kama lilivyo jina lako we zero kweli na sio mfuatiliaji wa taarifa za nchi yako kiasi kwamba hujui nini kinaendelea sasa kwa kukusaidia nenda tume ya uchaguzi utapata data usituchafulie hali ya hewa humu.
Sasa hapa nani anaechafua hali ya hewa kati yako wewe na yeye?
Sasa kama waelimishaji wenyewe ndo mna mipasho hivi kweli hayo mnayoyapigia debe ndo yataeleweka kweli?
 
Mimi niko kundi la Banana (Ndizi); vipi mwenzangu? Chungwa au? Kimsingi, kama magamba wangeendesha mchakato inavyotakiwa, Katiba ilitakiwa kuwa na makundi mawili tu - NDIO au HAPANA. Lakini saa hizi kila mtu anaongea lake:-

(a) Kuna wa NDIO (magamba and the like)
(b) Kuna wa HAPANA (Maaskofu)
(c) Kuna waliosusa (UKAWA)
(d) Kuna undecided (Masheikh wa Kadhi)
(e) Kuna wasio na mpango (wanaouza nyaraka za nchi kwa tende)
(f) n.k.

Jamani kila mara ninapoona watu wanaharibu maana na mantiki ya kitu huwa sipendi kukaa kimya. Wewe unayejiita "dudus" acha tabia ya ududu dudu. Huu upotoshaji umeutoa wapi? Tabia ya dudu ni kuharibu, kwahiyo nawe umekuja kuharibu siyo? acha tabia zako hizo za kibaguzi, hayo makundi unayoyaainisha ni ya mwelekeo wa uchochezi na wala hayana tija kwa taifa letu.

Tujenge taifa letu acha kuleta mambo yako hapa. Ubaguzi huo baki nao mwenyewe huko huko! Tanzania hatujazoea ubaguzi ndiyo maana Katiba Inayopendekezwa inaainisha kuwa “urithi tulioachiwa na Waasisi wa Taifa letu wa kujenga nchi yenye umoja wa watu wake ambao hawabaguani kwa misingi ya ukabila, dini, rangi, jinsi, ulemavu au ubaguzi wa aina nyingine yoyote”

Ndiyo maana Baba wa Taifa Mwl. Julius K. Nyerere aliwahi kusema “Msituingize kwenye karne ya 21 tukiwa kwenye basi la Udini, Dini inatusu nini sisi? Hebu acheni huo upumbavu na ni hatari kwa mustakabali wa taifa letu”.

Kwa Busara yake muasisi wa taifa hili aliliona hilo, leo hii wewe kwa ujinga wako uturudishe huko? Kamwe tabia hii siyo ya kufumbiwa macho na kila Mtanzania anayependa nchi yake kwa manufaa ya sasa na ya vizazi vijavyo.
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Kura ya Maoni kampeni za NDIO na HAPANA zinaanza
Kesho tarehe 31 Machi, maana kampeni ni siku 30 kabla ya siku ya kupiga kura ya maoni ambayo ni Aprili 30.

Je unaijua kamati yako ya ndio au hapana?

Je mmetangaziwa lolote na Tume ya Uchaguzi juu ya kuanza kwa kampeni?

Kama hapana,

kataa mwenendo wa maisha ya kuvunja sheria, kwa namna maandalizi yalivyo hatuwezi kuwa na Kura ya Maoni bora.
Kibanga Ampiga mkuu kimya kimya mkuu nimekuelewa na nijua hiyo kitu haipo ingawa kuna watu wametutonya wanataka kuifanya mwezi wa nanae lakini vyovyote itavyokuwa tutapiga kura ya hapana
 
Last edited by a moderator:
Kibanga Ampiga mkuu kimya kimya mkuu nimekuelewa na nijua hiyo kitu haipo ingawa kuna watu wametutonya wanataka kuifanya mwezi wa nanae lakini vyovyote itavyokuwa tutapiga kura ya hapana

Tatizo lililopo hapa ni uelewa na taarifa. Inashangaza sana ninyi ndiyo watoa hoja na ninyi hao hao mnatoa majibu ya vitu vilivyo nje ya uwezo wenu. Mmekuwa wasemaji wa NEC? Kwanini msiwaachie NEC kazi yao wafanye, nasi tuwaulize watupe majibu? Hizi "nec" za mtaani zisizorasmi ni hatari sana maana zinalisha watu taarifa wanazotaka wao kusikia na sii watu wanataka kusikia nini. Acheni hizo tabia za kudanganya danganya. Penda uzalendo, Jenga taifa lako.
 
umeambia za kutonya na sio taarifa au MWASI MWAKENDA au na wewe ni kama wale
 
Last edited by a moderator:
Mimi nauliza tu, watu wameshaandikishwa wote?? na sheria ilisema lazima ziwepo siku 60 za elimu kwa wananchi ili waielewe na hilo lilikuwa jukumu la tume ya uchaguzi, sasa zimekuwa siku 30?? Lubuva anasema siku 30 wanaweza waandikisha maliza watanzania wote?? Hii nchi tuna matatizo makubwa sana, na kwa mwendo huu tutabaki omba omba milele yote.. vitu vya muhimu hatuna maandalizi, lakini vitu vya kijinga kama kukimbiza mwenge, sijui ..day, hizo pesa zake huwa zipo na zinaandaliwa mapema tu...

naanza kuamini kuna baadhi ya watu wanataka kwa makusudi kabisa kulitumbukiza taifa katika machafuko.
 
Tatizo lililopo hapa ni uelewa na taarifa. Inashangaza sana ninyi ndiyo watoa hoja na ninyi hao hao mnatoa majibu ya vitu vilivyo nje ya uwezo wenu. Mmekuwa wasemaji wa NEC? Kwanini msiwaachie NEC kazi yao wafanye, nasi tuwaulize watupe majibu? Hizi "nec" za mtaani zisizorasmi ni hatari sana maana zinalisha watu taarifa wanazotaka wao kusikia na sii watu wanataka kusikia nini. Acheni hizo tabia za kudanganya danganya. Penda uzalendo, Jenga taifa lako.

mahaba mabaya sana,yaani mpaka muda huu huoni kama kuna tatizo,hata kichwani hujiulizi kuwa mambo hayaendi sawa licha ya kuisubiri hiyo neccm itoe taarifa?
 
Hueleweki unataka kujua au kufahamu nini. Kapumzike kama umechoka. Wakati unapumzika chukua nakala yako jisomee Katiba Inayopendekezwa upate uelewa vizuri ili tushirikiana kuijenga nchi yetu.
MWASI MWAKENDA nikiangalia hiyo picha yao inanichanganya lakini nakumbuka tu ngoja nikapumzike

but nipo na katiba inaypondekezwa, rasimu ya warioba na kipeperushi kizuri kabisa cha jukwaa la katiba
 
naanza kuamini kuna baadhi ya watu wanataka kwa makusudi kabisa kulitumbukiza taifa katika machafuko.

Narudia tena, inwezekana nawe Kozo Okamoto unauliza maswali bila hata kufuatilia mjadala. Mmekuwa wasemaji wa NEC? Kwanini msiwaachie NEC kazi yao wafanye, nasi tuwaulize watupe majibu? Hizi "nec" za mtaani zisizorasmi ni hatari sana maana zinalisha watu taarifa wanazotaka wao kusikia na sii watu wanataka kusikia nini. Acheni hizo tabia za kudanganya danganya. Penda uzalendo, Jenga taifa lako.
 
uzalendo?ndo nini?ndo mdudu wa aina gani.....kama ingekuwa ni uzalendo hebu soma hii quote ya juzi tu.....uzalendo unakuja kwa vibovu kama hivi????????????????????????????????,

"Katiba hii imezingatia na kutambua makundi mbalimbali na mimi sina haya kuwaeleza kuwa tuipitishe kwani licha ya upungufu ilionao, haifikii hii ya sasa. Tusipoipitisha tutaendelea kuitumia hii na sidhani kama kuna Rais atakuja na kuanza na mchakato wa Katiba, hivyo hii hii tuipitisheni kama ina upungufu utafanyiwa maboresho kwani Katiba siyo Msahafu au Biblia."
 
mkuu ni kweli katika mambo yasiyowezekana kokote yawezekana tanzania kama mfu alipiga kura na kuwa counted do you think nini kitawashinda

Jamani, acheni kujazana uongo usio na msingi. Tumia busara angalau kidogo tu! Tutakuelewa, kwa huo uongo wenu mnaopeana kamwe hatuwezi kufika popote. Pata taarifa sahihi kwa wahusika ambao ndiyo jukumu lao. Katiba ni yetu sote na taifa ni letu sote. Penda uzalendo, Jenga taifa lako.
 
christine nakuonea huruma maana umeingia kichwakichwa na kisha kuropoka katiba imeshafeli bila kueleza imefeli kivipi? Acha kujilisha upepo hili goma linasonga kwa spidi ya ajabu we kalia kuzubaa unakosa kuungana na mamilioni ya watanzania watakaoiunga mkono katiba pendekezwa.

Epuka kupoteza kura yako!

Mkuu waambie hao, kura zisipotee kabisa. Mimi binafsi kura yangu ni HAPANA kwa katiba ya gaba chori joka lenye makengeza mwizi mkubwa!!
 
Mkuu waambie hao, kura zisipotee kabisa. Mimi binafsi kura yangu ni HAPANA kwa katiba ya gaba chori joka lenye makengeza mwizi mkubwa!!

Tatizo ninaliliona hapa ni hisia za watu na sii uhalisia wa vitu. Uhalisia wa Katiba Inayopendekezwa asili yake ni sisi Watanzania. Kama ilianzia kwetu, hizi porojo zinatoka wapi? Mara huyu mara yule! Jamani Hii Katiba ipo kihalali na ilianzishwa kwa utaratibu maalumu. Kwa nini utaratibu tuliyojiwekea wenyewe tunajifanya siyo wetu? EWE MTANZANIA MPENDA AMANI NA NCHI YAKO. SONGA MBELE ILI TANZANIA IPATE KATIBA BORA INAYOMJALI KILA MWANANCHI.
 
Back
Top Bottom