Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 18,772
- 8,939
kila siku tbc wanarusha hiyo ndiyo kampeini ndugu
Mkuu hao watakuwa wamevunja sheria ambayo ilipitishw Bungeni, na kesho ndio Rasmi siku ya kwanza Ya kampeni ili kura iweze kufanyika Tarehe 30/4/2015, na hili lisipo fanyika Maana yake ni Sheria Imevunjwa na nadhani itabidi sheria irudishwe bungeni na Tarehe mpya Ipangwe ili kampeni zianze na tarehe mpya ipangwe.
kila siku tbc wanarusha hiyo ndiyo kampeini ndugu
nina mashaka kama wewe ni mtanzania. Maana sisi tunajua nchi inavyoendeshwa. Pia tambua katika hatua za kusonga mbele huwa 0,+1 au 0,-1 huvyo zote ni hatua. Sisi tunapiga hatua kwa kurudi nyuma.
Katiba ishafeli,hakuna kitu
kwa mujibu wa sheria ya kura ya maoni kampeni za ndio na hapana zinaanza kesho tarehe 31 machi, maana kampeni ni siku 30 kabla ya siku ya kupiga kura ya maoni ambayo ni aprili 30.
je unaijua kamati yako ya ndio au hapana?
Je mmetangaziwa lolote na tume ya uchaguzi juu ya kuanza kwa kampeni?
Kama hapana,
kataa mwenendo wa maisha ya kuvunja sheria, kwa namna maandalizi yalivyo hatuwezi kuwa na kura ya maoni bora.
katiba ishafeli,hakuna kitu
mimi niko kundi la banana (ndizi); vipi mwenzangu? Chungwa au? Kimsingi, kama magamba wangeendesha mchakato inavyotakiwa, katiba ilitakiwa kuwa na makundi mawili tu - ndio au hapana. Lakini saa hizi kila mtu anaongea lake:-
(a) kuna wa ndio (magamba and the like)
(b) kuna wa hapana (maaskofu)
(c) kuna waliosusa (ukawa)
(d) kuna undecided (masheikh wa kadhi)
(e) kuna wasio na mpango (wanaouza nyaraka za nchi kwa tende)
(f) n.k.
Mbona wanalumumba hawajibu jitokezeni
Mimi nauliza tu, watu wameshaandikishwa wote?? na sheria ilisema lazima ziwepo siku 60 za elimu kwa wananchi ili waielewe na hilo lilikuwa jukumu la tume ya uchaguzi, sasa zimekuwa siku 30?? Lubuva anasema siku 30 wanaweza waandikisha maliza watanzania wote?? Hii nchi tuna matatizo makubwa sana, na kwa mwendo huu tutabaki omba omba milele yote.. vitu vya muhimu hatuna maandalizi, lakini vitu vya kijinga kama kukimbiza mwenge, sijui ..day, hizo pesa zake huwa zipo na zinaandaliwa mapema tu...
christine nakuonea huruma maana umeingia kichwakichwa na kisha kuropoka katiba imeshafeli bila kueleza imefeli kivipi? Acha kujilisha upepo hili goma linasonga kwa spidi ya ajabu we kalia kuzubaa unakosa kuungana na mamilioni ya watanzania watakaoiunga mkono katiba pendekezwa.
Epuka kupoteza kura yako!
tunaenda kwenye kura ya maoni kwa vitambulisho vipi? Vipya au vya zamani?
yani nawewe kwa akili yako unataka kuipigia kura ya ndio katiba ya joka lenye makengeza?