Kesho mambo yakienda vizuri nitafukuzwa kazi chanzo ni marafiki

Urafiki wetu umepelekea huyo bwana kujua mpaka mambo yangu mengi ya siri
Kosa lako lilianzia hapa, KAZINI HUWA HAKUNAGA RAFIKI huyo ni mtumwa mwenzako au mfanyakazi mwenzako Waingereza wanasema ni co-worker

Kilichowakutanisha ni kazi sio urafiki. Fanya kazi rudi kwako epuka vikundi vya kukaa pamoja wakati wa mapumziko au mnapotoka.

Mambo ya kikazi tu ndiyo yawakutanishe nje ya hapo kimbia baada ya kipenga cha kufunga ofisi

Hata mademu wa kazini sio wa kutongoza wala kulomba.
 
Wakuu salaam!
Husikeni na kichwa hapo juu, Naishukuru Tume imeamua kwa moyo mkunjufu kuniacha niendelee na kibarua japo kwa uangalizi maalumu tena wa karibu mnoo.

Jobless mimi ni ndugu yenu na sitoacha kuwa ndugu yenu likitokea la kutokea tena mkataa kwao mtumwa nitarejea


Wenu sakwe bin sakwe
Binadamu mashakaπŸ™
 
hongera mimi kama familia yako nimefurahi kuendelea kubaki hapo huku unajipanga ikitokea umetimuliwa usije kukaa kitaa bure,, am happy for you sakwe
 
mimi kwa umri wangu huwa sina na sitawahi kutengeneza urafiki eneo la kazi, kwanza sipendi mazoea na mtu yeyote ya kupitiliza, tujuane kikazi tuachane kikazi. tunaweza kufahamiana na kupeana za fursa za machaka mapya ila sio kuwa marafiki, urafiki mwiko.
 
ufanye kazi sasa achana na kina idd na john hao ni ma-spy wa boss mkuu
 
hongera mimi kama familia yako nimefurahi kuendelea kubaki hapo huku unajipanga ikitokea umetimuliwa usije kukaa kitaa bure,, am happy for you sakwe
Asante sana Mkuu nitakuwa makini sana tena sana asante kwa dua nyingi sina la kulipa
 
Hili ni zaidi ya funzo kwangu mkuu nimelibeba asilimia zote
 
Sasa unajuaje kuwa kesho ndio unafukuzwa kazi?
 
Kwanini usipige maombi ya kuvunja mipango hiyo lakini baada ya kutubu kwa dhati halafu uone nini kitatokea na uje kutuambia hapa.
 
Karibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…