saigilomagema
JF-Expert Member
- Jun 5, 2015
- 4,683
- 7,222
Naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati anatuambia nchi Ina umeme wa ziada, Cha ajabu kukatika kwa umeme kupo pale pale. Huku Arusha wilaya ya Arumeru halmashauri ya Meru tangia usiku mpaka sahizi hakuna umeme tuko gizani shida ni Nini? Wakati huo KUANZIA kesho Marais wa nchi za Africa wanaanza mkutano wa siku 2 kesho kujifunza kwetu. Wanakuja kujifunza Nini? Huko DSM watakakofikia hawaukatiki?