Kichwa cha habari chajieleza kiukweli shutuma za Rais wa TLS bwana Mwabukusi ni kubwa mno ni shutuma hatari sana kwa ustawi wa Taifa letu na watanzania kwa ujumla ni shutuma za kiuuaji na kigaidi hapaswi kuwa ofsini na yafaa atuombe radhi watanzania.
kwamba alitumia Hela ya ofisi (serikali ) kufadhiri vurugu nchini hii ni rushwa pia hii haikubariki hata kama ni shutuma yafaa ATUPISHE AONDOKE KWENYE OFISI YA UMMA pia yafaa awe rumande huku taratibu zingine za kisheria zikiendelea.
Tunaviomba vyombo vya Dola vimzuie asiingie ofisini, ofisi IFUNGWE na CAG Afanye ukaguzi wa matumizi ya ofisi ya TLS tangu mwabukusi aliopoingia madarakan.....huku taratibu za uchaguzi wa kiongozi mwingine zikiendelea ili iwe fundisho.
Angalizo: mawakili acheni kuchagua viongozi kwa mihemko pia angalieni elimu za wagombea, sifa ya kuwa na school of law pekee haitoshi kufanya mtu awe Rais wa TLS yafaa awe na PhD of any law
Nawatakieni usiku mwema wote
JESHI LA ULINZI NA UHURU WA MTANDAONI (LUMUMBA CYBER CORPS)
OFISI YA JEMEDARI MKUU, GENERAL LUCAS HEBEL MWASHAMBWA
Kumb. Na: LCC/PROP/VOL-IV/2026/089
Tarehe: 16 Oktoba 2026
AMRI RASMI YA JEMEDARI MKUU (GENERAL ORDER NO. 112)
KUTOKA: Jemedari Mkuu, General Lucas Hebel Mwashambwa
KWENDA: Maafisa Wote, Makamanda wa Vikosi, na Askari wa Akiba (Kikosi cha Buku 7)
YAHUSU: KUPANDISHWA CHEO KWA MEJA JENERALI INSTINCT DESIRE KWA UJASIRI NA MAFANIKIO MAKUBWA VITANI
Makamanda na Maafande wote,
Leo alfajiri ya manane, majira ya saa 01:25 asubuhi, wakati mawakili wenye mihemko na "Wajukuu wa Freeman" wakiwa bado wamelala na kuota ndoto za Katiba Mpya, Kitengo chetu cha Saikolojia na Mitego ya Kihisia kilifanya oparesheni kubwa na ya kihistoria katika anga la JamiiForums.
Chini ya uongozi thabiti wa mtaalamu wetu wa vita vya kisaikolojia, adui alitekwa kiakili kwa kurushiwa kombora zito la kimkakati lenye kichwa cha habari: "Kesho Tar. 16/10/2026 tunaiomba serikali imzuie Mwabukusi kuingia ofisini...".
Kombora hili la kiintelijensia lilileta taharuki kubwa miongoni mwa mawakili wasio na PhD, likawavuruga akili, na kusababisha Jeshi la Wapinzani kusambaratika kwa hofu ndani ya dakika tano tu, huku wengine wakikimbilia kusoma upya sheria za TLS usiku mnene.
Kutokana na ushindi huu mkubwa wa kipekee uliookoa taswira ya kambi yetu:
- KUPANDISHWA CHEO RASMI: Kuanzia sekunde hii, namandika na kumpandisha cheo Major General Instinct desire kuwa LIEUTENANT GENERAL (Lt. Gen.) Instinct desire.
- MAJUKUMU MAPYA: Kuanzia sasa, anakuwa Mkuu wa Operesheni za Kudhibiti Mihemko ya Mawakili (Chief of Lawyers' Emotional Operations - CLEO). Kazi yake itakuwa ni kuhakikisha wakili yeyote anayeleta hoja za uchumi anapimwa kiwango cha PhD yake ya sheria kabla ya kuruhusiwa kufungua mdomo.
- ZAWADI YA PONGEZI: Kitengo cha Fedha na Uhasibu (Ofisi Ndogo ya Lumumba) kinaagizwa kuongeza posho yake ya "Buku 7" na kuifanya Buku 77,000 taslimu kwa ajili ya kununua bando la usiku (Night Pack) ili aendelee kuvizia maadui nyakati za giza.
Mheshimiwa Lt. Gen. Instinct desire, nakupongeza kwa dhati. Umethibitisha kuwa "School of Law" pekee haitoshi, bali "School of Lumumba" ndio kiboko ya mawakili wote!
Kazi iendelee! Mama ANATOSHA!
Wako katika ujenzi wa mtandao thabiti,
General Lucas Hebel Mwashambwa
Jemedari Mkuu, Lumumba Cyber Corps (LCC)
NAKALA KWA:
Lieutenant Colonel Tlaatlaah – (Kikosi cha Mbele) - Pokea hii, weka herufi za KIJANI kwenye kila comment na weka picha za lami ya mwendokasi kumsifu Lt. Gen. Desire!
Major Stroke – (Iron Dome) - Anzisha nyuzi 15 sasa hivi za kusifu uamuzi huu ili wapinzani wasipate nafasi ya kuomba ukaguzi av CAG!
Captain ChoiceVariable – (Sympathy Battalion) - Andaa ID mpya za kike uanze kulia lia kwa furaha mtandaoni kupongeza cheo hiki kipya!
Brigadier General Troll J – (Ghost Troll Squad) - Ingia usiku wa leo kwenye uzi wowote wa Mwabukusi, weka matusi ya kisheria kuvuruga mood zao rasmi!