Kesi iliyofungiliwa na Adv Kisabo kuhusu walipo kina Soka kusililizwa kesho Dar mahakama Kuu

Kesi iliyofungiliwa na Adv Kisabo kuhusu walipo kina Soka kusililizwa kesho Dar mahakama Kuu

Wamethibitisha vipi huyo Soka aliitwa na polisi.

Tukisemaga hawa wanasheria wabongo wengi vihiyo inaonekana kama kejeli.

Binafsi ningeomba kwanza mahakama iamuru kampuni inayompatia huyo Soka na wenzake itoe number zilizopiga simu zao siku ya mwisho kujiridhisha kama ni number ya kituo cha polisi. Baada ya hapo ndio utoe lawama, lakini kutumia sweeping statement tu hizo ni baseless accusations hata kama kweli kuna mkono wa polisi.

Lawama za CDM kwa polisi inaweza tengeneza copycat kidnappers and killers kwa kutumia mbinu ya kupigia watu simu kujifanya wao ni polisi na kuwaambia waende mahala fulani.

Ifike wakati viongozi wa CDM wawe makini na kauli zao hasa kipindi hiki ambacho vitendo vya utekaji na mauaji vimeshamiri.
 
Hii kesi ya kisiasa na itatoa shule ya somo la uraia juu ya haki zako raia yeyote mtuhimiwa kabla ya kukakamtwa na baada ya kufikishwa polisi una haki gani zilizotamkwa ambazo Polisi na kwa kiasi pia mahakama hawataki uzifahamu wewe mwananchi
 
REJEA MWAKA 2023

MAHAKAMA YAIBANA POLISI KWA KUKAA NA MTUHUMIWA SIKU 18
Mahakama Kuu, Masjala ya Dar es Salaam imeliamuru Jeshi la Polisi nchini kumfikisha mahakamani Mkurugenzi wa Kampuni ya Nezak Investment Limited, Zakaria Kapama ambaye yuko mahabusu kwa siku 18 bila kufikishwa kortini.

Kifungu cha 32 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA) ya mwaka 1985 na marekebisho yake, kinataka mtuhumiwa kufikishwa mahakamani ndani ya saa 24, isipokuwa kwa makosa yale ambayo adhabu yake inakuwa ni kunyongwa hadi kufa.

Kwa mujibu wa kifungu hicho, ikiwa haiwezekani, basi mtuhumiwa aachiwe kwa dhamana, lakini kumekuwa na kilio katika vituo mbalimbali vya polisi kuwa, baadhi ya watuhumiwa husota muda mrefu mahabusu za polisi bila kufikishwa kortini kwa wakati.

Amri hiyo ilitolewa jana na Jaji Wilfred Dyansobera, baada ya maombi ya jinai yaliyowasilishwa mahakamani na Kapama dhidi Mkuu wa Kituo cha Polisi (OCS) cha Oysterbay, Kamanda wa Polisi Kinondoni na Inspekta Jenerali wa Polisi.

Katika maombi hayo namba 132 ya 2023, Kapama alimuunganisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), kama mjibu maombi wa nne na aliiomba Mahakama kuwaagiza wajibu maombi hao kumwachia wanavyomshikilia au kumweka kizuizini isivyo halali.

Pia, aliomba kama hawatamwachia, basi Mahakama iwaamuru wajibu maombi kufika mahakamani kueleza sababu za kumnyima uhuru wake, kumzuia, kumuweka kizuizini nje ya muda wa kisheria na kuwataka kutimiza majukumu kwa mujibu wa sheria.

Kupitia kwa wakili wake, Deogratias Butawantemi, Kapama ambaye pia kampuni yake inamiliki KP Motors inayohusika na uagizaji wa magari, anaeleza Septemba 29 mwaka huu 2023 alikamatwa na polisi na kuwekwa mahabusi Kituo cha Oysterbay.

Kwa mujibu wa hati ya kiapo chake, hadi anawasilisha maombi hayo juzi alikuwa bado anashikiliwa kituoni hapo bila kupewa dhamana wala kufikishwa mahakamani, kama sheria za nchi zinavyoelekeza.

Akitoa uamuzi wa maombi hayo jana, Jaji Dyansobera aliwaagiza Mkuu wa Kituo cha Polisi Oysterbay na wajibu maombi wenzake, kuhakikisha mleta maombi huyo anafikishwa mbele ya Mahakama na amri hiyo itekelezwe sio zaidi ya siku ya leo (Jumatano).

(Imeandikwa na Daniel Mjema)

Soma Hukumu : Ya Jaji Wilfred Dyansobera, wa Mahakama Kuu ya Tanzania

Source : Zakaria Anthony Kapama vs. Officer Commanding Station Oyterbay (OCS) & 3Others) (Misc. Criminal Application No. 132 of 2023) [2023] TZHC 21830 (17 October 2023)
 

'DEUS SOKA HAJAWAHI KUTUKANA ANADAI KATIBA MPYA''GODBLESS LEMA AMWAGA MACHOZI SAKATA LA SOKA KUTOONEKANA


View: https://m.youtube.com/watch?v=45MPo0bTWig

Godbless Lema azungumzia masuala mtambuka yatakavyo athirika na kufeli kwa mfumo haki jamii, bunge na serikali kulinda haki ya raia kuishi huru na kuwa kuacha kujishughulisha ktk siasa siyo suluhusho.

Godbless Lema anasema ipo siku utagombana na mtu ktk masuala yasiyo ya kisiasa kama kusingiziwa n.k ukaishia kutekwa, kupotezwa, kutopelekwa mahakamani ndiyo utajua umuhimu wa kesi hii ya Deus Soka inavyoweza kukukumba ktk hali yoyote nje ya siasa ...

Atahadharisha pia yakuwa wawekezaji makini na wadau wa maendeleo kutoka nje wanafuatilia hali ilivyo Tanzania hivyo kuathiri uchumi wetu ...
 
Mlio Dar fikeni kwa wingi!

Polsi tusiwalaumu, huenda kuna amri toka kwa wakubwa zao kuwa washikilie/waue. Kama IGP, Waziri Masauni, and all other top authorities wamekaa kimya, means wanahusika na amri hizi!
Vijana wapatiwe ushauri wa kujiongezea kipato siasa za Africa haziwezi wasaidia. Ukipoteza maisha watu watakusikitikia na utakuwa mtaji wa wanasiasa wa vyama pinzani, huu ni ujinga, unawapa hasara ndg zako kwa faida ya watu wachache
 
Back
Top Bottom