Kesi ishakuwa ngumu hii, No Reforms No Election imeshawazidi nguvu System na CCM

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Kutokana na kupokelewa kwa kiwango cha kutisha ajenda ya No Reform No Elections napenda kuwashauri system na CCM wasitishe mradi wao wa kutoa fedha kwa madalali eti kuonesha Chadema inakufa

Hiki Chama badala ya kufa ndo kinazidi kupendwa kwa kiwango cha kutisha na Watanzania.

jioneeni ya leo Kahama wenyewe!
 
Samia aache kuvimbishwa kichwa na chawa,hoja ya mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi ili uwepo uchaguzi wa huru na wa haki siyo ya Chadema ni hoja ya kitaifa. Ukiwepo uchaguzi wa huru na haki hata akishinda Samia yeye mwenyewe atajisikia fahari kuwa amechaguliwa na Watanzania lakini wanachokwenda kufanya Urais wake hauna thamani kwani utakuwa umepatikana kwa hila na udanganyifu jambo ambalo hata yeye nafsi yake inalijua.
 
Ndumuz
 
Aloo!

Yuko wapi Lucas Mwashambwa na mwenzie Tlaatlaah ???

Njoeni huku mtupatie tathmini ya uhai wa chama pinzani.

Wapi Mbowe?

Wapi Msigwa?

Wapi TAL?

Wapi Bony Yai?

Wapi Silinde?

Wapi Nassary?

Wapi Mwita Waitara?

Wapi Humphrey Polepole na Bashiru??

Wapi CPA Amos McCullough na wale G55 wabunifu wa siasa za kisasa?

Wapi ZZZ na agenda kuu za kitaifa???

Ni hayo tu wakuu.

Nasikia watani wa Jangwani wanamwambia kila mtu: HATUCHEZI NG'O!

Napendekeza sana Rais Samia afanye kitu hao jamaa walazimishwe kucheza, watake wasitake - tena kwenye uwanja wa Amani Zenj!

Ikiwezekana wekundu wa Msimbazi wapigwe faini pesa ndefu kwa kuogopa kupeleka timu uwanjani ile tarehe 8!
 
Sasa aje yule product ya GMO Lucas Mwashambwa aseme hizi ni za 2015
 
Kwa mujibu wa serikali, agenda ya mabadiliko ya uchaguzi zilishazingatiwa na kufanyiwa marekebisho stahiki.

Sasa ni wakati wa kujiamini na kuvaa magwanda ya mapambano ili kukutana kwenye boksi la kura!
 
tahmini ya wanaojiengua chadema au? kutoka zanzibar au bara?
 
Huko mbeleni Mwashambwa litakuwa ni msamiati katika lugha ya Kiswahili kuelezea kiwango cha juu cha unagiki, uchawa na upungufu wa akili.

Mtu atakapoambiwa, wewe ni Mwashambwa, atajiona ubinadamu wake una madhaka.
Kweli kama ilivyokuwa neno Kilaza na Kihiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…