Kesi namba 456: Jamhuri dhidi ya JamiiForums - Oilcom na Uchakachuaji/Ukwepaji kodi bandarini Dar

viva lissu, Mungu wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo atasimama nawe

kwa mtazamo wangu hii kesi ingefaa kuwa ya defamation lakini kwasababu imechanganyika na siasa basi imekuwa criminal case
 
Tuache mambo ya Vyama. Namshauri Mhe. Rais amteue Tundu Lissu kuwa Jaji wa Mhakama Kuu.
 

Mie sio mwanasheria ila nadhani unapokuwa unafanyiwa cross examination unatakiwa ujibu maswali kama unavyoulizwa, na hapo ndipo inapokuwa shida, ukienda kinyume tu na swali kwa nia ya kutaka kumtoa nje ya mstari wakili unarudishwa palepale na hakimu/judge. Anakurudisha uendelee kuulizwa maswali hata kama ni ya kuudhi.

Nakumbuka kwenye kesi ya magabacholi wakati wa Mtikila, wafuasi wake walikamatwa kwa kuzua tafrani baada ya mkutano wake Jangwani, huku wakiimba Mtikila Oyee na kuwatusi magabacholi.

Wakati wa kesi shahidi aliulizwa na Lamwai;

Lamwai: Hawa mliowakamata ni wafuasi wa Mtikila?
Shahidi: Ndio ni wafuasi wa Mtikila
Lamwai: Mlijuaje kuwa ni wafuasi wa Mtikila
Shahidi: Walikuwa wanaimba Mtikila, Mtikila, Mtikila huku wanatukana Magabacholi
Lamwai: Naomba uimbe, Mtikila, Mtikila...
Shahidi: Hapana siwezi kuimba
Hakimu: Tafadhali shahidi imba kama ulivyoelekezwa
Shahidi: Mtikila, Mtikila...
Lamwai: Je wewe ni mfuasi wa Mtikila?
Hiyo inaonesha jinsi ambavyo shahidi anapokuwa na wakati mgumu sana mahakamani hata kama ana uwezo na akili nyingi.
 
Serikali yetu inatumia nguvu kubwa kuandaa mashitaka bila kuandaa wanasheria wake na mashahidi. Kodi zetu zinatumika vibaya.
 
Kwan wanataka wamjue huyo Furhar ili iweje sasa?

Nilitegemea serikali ifutilie habari aliyoileta na kuwafungulia mashtaka hao Oilcom, wao wanatumia nguvu nyingi kumpata mleta taarifa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…