Na mweshimu Mh. Lissu sana kama Mbunge na Mwanasheria anayejua kujenga hoja na anayejua kutetea wataje wake.
Ninachotaka kusema hapa Mh. Lissu ni binadamu, si Mungu wa sheria. Hivyo ninaamini wapo wanasheria wengine wanaoweza kumbana kama watatumia mbinu zile anazozitumia yeye ila wakiwa wameziboresha. Kama ungetumia jicho la tatu kusoma post yangu ungegundua kuwa nilikuwa na wahimiza wanasheria wengine waboreshe mbinu zao za kiuanasheria na pia hata yeye (Mh. Lissu) astuke. Astuke asije akabweteka (kwa uungu wakisheria wa baadhi ya wenzake wanaompa) na baadaye akawaabisha TLS. Wanasheria wengine badala ya kubuni na kuboresha mbinu za kukabiliana na changamoto za kiuanasheria wawapo kazini, wanavizia kumsikiliza Mh. Lissu tu anavyofanya vitu vyake mahakamani ili nao watumie mbinu zake hizo (tena kibaya zaidi kwa kukopi na kupesti) katika shughuli zao.
Kwa utaratibu huu wanasheria hawa hawataweza kuwasaidia watanzania. Ndiyo maana nimeandika hicho kilichokuprovocke ili wabadilike! Ila ukweli unabaki pale kuwa kwa mbinu hizo mbili nilizozisema awali, kama Mh. Lissu hataboresha mbinu zake, anaweza kutolewa kwenye reli wakati anamfanyia mtu cross examination kama mtu huyo atazitumia mbinu nilizoeleza!
Tusimfanye Mh. Lissu Mungu wa sheria ila tumtumie kama role model tu wa kisheria na tujifunze kwake ila tusimkopi.
=====
Utakuwa umenielewa.