Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru

Kuwa na chombo cha kutoa Elimu au michango ya mawazo tofauti hapa Afrika ni Tatizo. Lakini hatuwezi kuwa kama kisiwa lazima vyombo vya kujenga, kuelimisha na kukosoa Kwa njia isiyofaa wawepo kwenye jamii.
 
It sounds like Our privacy "compromised"
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jamii Forums, Maxence Melo (40) kulipa faini ya Sh3 milioni baada ya kutiwa hatiani katika shtaka moja la kuzuia Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi #MwananchiUpdates
 
Mnachekelea kutozwa faini! Hamjaona hapo katiwa hatiani kwa kukwamisha upelelezi?
Kinachofuata sasa wakitaka info zenu watapewa.
 
Milioni 70+ au miezi 5 jela, then milioni 3 au mwaka mmoja jela....😳ila mambo ya kisheria siyajui sana...akili yangu ndo imenifikirisha hivyo....
 
Hehe hela wanayoingiza kila siku kwa matangazo tu. Tatizo ni je baada ya hili serikali itakua inaomba data za kila mtu wanayemtaka humu JF?
Ndio hapo wasije kuwa wameingia makubaliano

Sent from Tapatalk
 
8 Apr 2020
Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu
Dar-es-Salaam, Tanzania

BREAKING: MKURUGENZI JAMIIFORUMS AHUKUMIWA KWENDA JELA AU KULIPA FAINI YA MILIONI 3.

Mkurugenzi wa mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo amehukumiwa mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Mil 3 baada ya kukutwa na hatia ya kuzuia jeshi la polisi kutekeleza majukumu yake. Kesi hii namba 456 ya mwaka 2016 ilinguruma kwa miaka minne na hukumu imetolewa leo. Mawakili kuandika notisi ya nia ya kukata rufaa kesho dhidi ya hukumu hiyo.


Source: Global TV online

N.B
Na hili litapita salama na mtandao wetu utaendelea kuwa huru. Tupo pamoja Mkurugenzi wa JamiiForums.

Mahojiano Mapungufu katika Katiba na mchakato wake (EXCLUSIVE INTERVIEW) ya JamiiForums na Balozi Khamis Kagasheki PT3

Mahojiano haya yalifanyika 29/05/2015 Balozi Kagasheki akizungumzia maisha na kazi zake kiujumla
Source : Jamiiforums
 
Back
Top Bottom