Kesi namba 457: Mahakama yasema Maxence Melo na Micke William hawana Kesi ya kujibu! Yawaachia huru

Kesi namba 457: Mahakama yasema Maxence Melo na Micke William hawana Kesi ya kujibu! Yawaachia huru

Mungu ni mkubwa, hii kesi imetukosesha amani sana, kwahiyo tutalipwa fidia ya usumbufu, au?
 
Mahakama zetu japo zinabanwa kuwa HURU ila zinajitahidi kutoa HAKI.
Haya ya kuwa huru au kutokuwa huru ni hakimu na hakimu. kuna ambao wako tayari kujiuza kwa fedha, ahadi ya cheo, kofia, fulana, khanga, vitenge, pilau, nk. wengine hata kutishwa tu kidogo basi wananywea. ila wapo mahakimu wenye misimamo. tunachohitaji ni kuwa na mfumo ambao serikali haiwezi kumtisha au kumhonga hakimu.
 
Mwisho wa madhalimu ni hasara

Mola ashukuriwe
Wameamua tuu kuwachia huru no sawa na timu muifunge kumi mkaiachia goli moja LA kufutia machozi..hivyo tumefutwa machozi na goli moja huku tumefungwa kumi
 
Hongera sana Peter Kibatala!
 
Hongereni sana Kampuni nzima ya Jamii Media, Mtandao wa JamiiForums, Watendaji wake Wakuu wote Maxence Melo , Mike Mushi , Asha D Abinallah , Moderators, Wafanyakazi na Members wote wa JamiiForums kwani haya maamuzi ni ushindi wetu sote ambao kila mara tunautakia mema huu Mtandao pendwa kabisa wa Kiswahili duniani.

Naomba Member yoyote mwenye hizi nyimbo mbili ( 2 ) ninazozipenda zifuatazo waniwekee hapa ili niburudike nazo:

  1. Hakuna Mungu kama Wewe ( Cosmas Chidumule )
  2. Hawawezi Kushindana ( Goodluck Ghoozebert )
Na naomba hizi nyimbo ziwaendee wale ' Visokolokwinyo ' wote wenye mioyo ya Husuda / Kisununu kwa Mtandao huu wa JamiiForums. Na niwaambie tu kwamba hata wafanyeje Mtandao huu una baraka zote za Mungu wa Ibrahim, Isaka na Yakobo pamoja na Mtume Mohamed SAW hivyo utadumu milele na daima. Niwaonye pia hao ' Visokolokwinyo ' wote kwamba ole wao waendelee Kuufuatafuata huu Mtandao wa JamiiForums hakika ' Makofi ' ya adhabu na mateso ya Mwenyezi Mungu / Allah / Maulana hayatawaacha.

Sasa ni mwendo mdundo na kanyaga twende tu!
 
Back
Top Bottom