Kesi namba 457: Mahakama yasema Maxence Melo na Micke William hawana Kesi ya kujibu! Yawaachia huru

Kesi namba 457 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) inayohusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kodi Bandarini Dar na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania imeendelea leo Juni 01, 2018 katika Mahakama ya Mkazi, Kisutu.

Akisoma shauri hilo Hakimu Godfrey Mwambapa amesema Washitakiwa hawana kesi ya kujibu na hiyo Mahakama imewaachia huru kuanzia leo.

Hili ni moja kati ya mashauri 3 yaliyokuwa yanawakabili washtakiwa. Kwa mantiki hiyo, bado kuna mashtaka 2 yatakayotajwa mahakamani hapa Juni 18.

Kesi hii namba 457 iliyokuwa ikiikabili JamiiForums, ilihusu kampuni ya CUSNA Investment ambayo ilidaiwa kufoji nyaraka bandarini, kukwepa kodi na kuwatesa wafanyakazi wazalendo na kupendelea wageni toka nje ya nchi.

Katika kesi hii, Polisi walitaka JamiiForums iwapatie taarifa za mwanzisha mada Kwayu na mchangiaji mmoja AMRISHIPURI ili waweze kuwakamata na kuwahoji kutokana na ukiukwaji wa taratibu, JamiiForums inadaiwa kuwa ilikataa kutoa taarifa binafsi za mwanachama wake kwa kuamini kuwa chanzo hiki cha taarifa kilikuwa na nia njema hivyo kutaka kwanza iwepo Hati ya Mahakama inayoridhia kukamatwa kwa mhusika na kuelezwa kosa lake.

"MICKE WILLIAM and MAXENCE MELO MUBYAZI on diverse dates between 10th of May, 2016 and 13th day of December, 2016 at Mikocheni area within Kinondoni district in Dar es Salaam Region being the Directors of JAMII MEDIA COMPANY LIMITED operating a social media network commonly known as Jamii Forums as managers and founders , while knowing that the Tanzania Police forces is conducting a criminal investigation on posts containing false information against CUSNA INVESTMENT and OCEAN LINK, published by its members in the said social media network with user names of KWAYU JF Senior —Expert member and AMRISHIPURI, intentionally and unlawfully concealed the identities of said members with intent to obstruct the said investigation."
View attachment 791198

Kujua kesi hii ilipoanzia na kujua kuhusu kesi nyingine dhidi ya JF soma =>Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums

Hivyo hivyo Boss Max.

So, now ni ruhusa kutiririka au?
 
Hii ni habari njema. Lakini hizi lugha zenu za kisheria wakati mwingine ngumu kuzielewa.

Walishtakiwa kwa makosa mangapi? Na hii hukumu inamaanisha hawana tena kesi yeyote na mahakamani?
Ndio maana ya kuachiwa huru ina maana kesi imefutwa na file limechomwa moto
 
Poleni waungwana Melo na Mike na hongereni kwa kupata haki yenu.tunawatakia kila la heri katika mengine yote, ili tuendelee kujenga nchi yetu kwa mawazo tofauti tofauti.
 
Kwi! Kwi! Kwi! Imegonga mfupa hiyo kudadeki ! Ifike wakati tuweke ukweli hata kama mchungu , nyinyi wanaccm mnaitumia jf lakini wakati huohuo chama chenu kinapambana kuimaliza na huku mnaangalia tu , tuwaeleweje ?
Ni wanafiki sana hawa watu.
 
Kesi namba 457 (Jamhuri v Maxence Melo na mwenzake Micke William) inayohusu kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link kudaiwa kukwepa kodi Bandarini Dar na kunyanyasa wafanyakazi wa kitanzania imeendelea leo Juni 01, 2018 katika Mahakama ya Mkazi, Kisutu.

Akisoma shauri hilo Hakimu Godfrey Mwambapa amesema Washitakiwa hawana kesi ya kujibu na hiyo Mahakama imewaachia huru kuanzia leo.

Hili ni moja kati ya mashauri 3 yaliyokuwa yanawakabili washtakiwa. Kwa mantiki hiyo, bado kuna mashtaka 2 yatakayotajwa mahakamani hapa Juni 18.

Kesi hii namba 457 iliyokuwa ikiikabili JamiiForums, ilihusu kampuni ya CUSNA Investment ambayo ilidaiwa kufoji nyaraka bandarini, kukwepa kodi na kuwatesa wafanyakazi wazalendo na kupendelea wageni toka nje ya nchi.

Katika kesi hii, Polisi walitaka JamiiForums iwapatie taarifa za mwanzisha mada Kwayu na mchangiaji mmoja AMRISHIPURI ili waweze kuwakamata na kuwahoji kutokana na ukiukwaji wa taratibu, JamiiForums inadaiwa kuwa ilikataa kutoa taarifa binafsi za mwanachama wake kwa kuamini kuwa chanzo hiki cha taarifa kilikuwa na nia njema hivyo kutaka kwanza iwepo Hati ya Mahakama inayoridhia kukamatwa kwa mhusika na kuelezwa kosa lake.

"MICKE WILLIAM and MAXENCE MELO MUBYAZI on diverse dates between 10th of May, 2016 and 13th day of December, 2016 at Mikocheni area within Kinondoni district in Dar es Salaam Region being the Directors of JAMII MEDIA COMPANY LIMITED operating a social media network commonly known as Jamii Forums as managers and founders , while knowing that the Tanzania Police forces is conducting a criminal investigation on posts containing false information against CUSNA INVESTMENT and OCEAN LINK, published by its members in the said social media network with user names of KWAYU JF Senior —Expert member and AMRISHIPURI, intentionally and unlawfully concealed the identities of said members with intent to obstruct the said investigation."
View attachment 791198

Kujua kesi hii ilipoanzia na kujua kuhusu kesi nyingine dhidi ya JF soma =>Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums

This is sweetest gift of the new month.

Thanks judiciary for doing your responsibility!
 
Yaani hiyo kesi haina mashiko kabisa toka mwanzo ilionekana ni ya kumfurahisha mtu tuu yaani anaetumia JF katoa uozo wa bandari kuhusu mafuta na Mh na Waziri Mkuu ni mashahidi kuhusu huko leo anaetoa taarifa anatafutwa kwa kushtakiwa tena...yaani wezi wanakumbatiwa ilitakiwa Takukuru kama ipo ndio waanzie hapo kujua kinachoendelea huko...
 
Big up. Nchi ya matamko acheni kutupiga ban tuwararue nchi wanaifanya kama kibanda cha biashara zao. hawajui kuwa nchi inaendeshwa kwa katiba.
 
Back
Top Bottom