Kesi nyingine ya Lengai Ole Sabaya kuanza hivi karibuni

Kesi nyingine ya Lengai Ole Sabaya kuanza hivi karibuni

Ngongo

Platinum Member
Joined
Sep 20, 2008
Posts
20,654
Reaction score
35,887
Wakuu heshima sana,

Wakati wowote kuanzia Jumatatu Mfungwa wa kifungo cha Miaka 30 Bwana Lengai Ole Sabaya anatarajiwa kupandishwa kizimbani kujibu mashtaka ya wizi wa kuaminika na wenzake watatu ambao wote ni wafungwa wa kifungo cha muda mrefu (30 years)

Lengai Ole Sabaya alitengenezewa gari lake binafsi,mwenye garage akampatia gharama za spares na ufundi Tsh 450,000.Lengai Ole Sabaya badala ya kulipa gharama za matengezo ya gari lake akamgeuzi mwenye garage ajatoa EFD Receipt na hivyo anasababisha upotevu wa fedha nyingi za serekali. Mafundi na mmiliki wa garage wakawekwa chini ya ulinzi na kutishiwa kufunguliwa kesi ya uhujumu uchumi na kutakatisha fedha. Baada ya majadiliano ya muda mrefu Mmiliki wa garage akakubali kutoa kiasi cha Tsh 90,000,000 ili kuepuka kufunguliwa mashtaka ya uhujumu uchumi.

General Sabaya bila aibu alikwenda kuchukua kiasi chote cha fedha Bank mwenyewe huku mwenye Garage akishikiliwa na wasaidizi wake nje ya Bank.
 
Hivi malyamungu kumbe alikuwa wa idd amin.. humu bashite anavyoitwaga malyamungu nikajua humu ndio kabatiszwa
Yaani Maliyamungu alikuwa chawa mkuu wa Idi Amino,Kazi zote chafu za kuteka watu,kuua,kufilisi wafanyabiashara alikuwa anafanya yeye kwa weledi mkubwa sana kama ilivyokuwa Bashite na case za wakina Manji,MO,Saa8, Lissu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom