Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Hiyo misingi ya common law sio lazima iwe na mamlaka kila mahala!...

Kama mtu anajua some law item kwanini asiongelee bana?

A plea of autrefois convict ([ame="[URL="http://en.wikipedia.org/wiki/Law_French"]Law French - Wikipedia[/URL]"]Law French[/ame] for "previously convicted") is one in which the defendant claims to have been previously convicted for the same offence and that hence they cannot be tried again. A plea of autrefois convict can be combined with a plea of not guilty (autrofois acquit).

Kwani hayo tunayojifunza shuleni hayana maana bana? Kwanini mtaala wetu usiwekwe kufuata hiyo sheria ya nchi unayoisema wewe?

That's why I like Law. One mistake one goal. Tusilazimishe hisia kwenye haki na sheria. Tufuate sheria zinasemaje ktk hili.
 
Umesema sawa, lakini bado watuhumiwa hawa wanaweza kukutwa na hatia ya mauaji kama Mahakama ya Rufaa ya Tanzania itafikia uamuzi kwamba...
Mheshimiwa suala tulilokuwa tunajadili ni kuhusu kushtakiwa upya sio uamuzi wa hana hatia kubatilishwa na mahakama ya rufaa. Naelewa kuwa Mahakama ya Rufaa inaweza kubadilisha uamuzi wa kutokuwa na hatia na kuwa na hatia. that is within the power of appellate court but that was not the subject matter of discussion then.

Naungana na wachangiaji kuwa utaratibu wetu wa uchunguzi wa makosa ya jinai bado una matatizo sana tu. hatuna wataalamu wa kutosha kufanya kazi hiyo kwa makini na hata hao waliopo bado kuna matatizo ya rushwa ambayo yanaadhiri mfumo wa uchunguzi na hata uendeshaji wa mashtaka nchini.

Kuna jambo ambalo kila siku nilikuwa naliwaza sana na ambalo linaweza kusaidia mfumo wetu wa Sheria. ni swala la plea bargaining, mfumo ambao unatumika sana katika nchi zilizoendelea na hata Afrika Kusini wanao huo utaratibu ambapo kama kuna mtu unafikiri anajua jambo ambalo linaweza kusaidia katika uchunguzi lakini huyo mtu vile vile ni mtuhumiwa basi unafanya makubaliano naye na kuweza kuwa shahidi kwa upande mmoja na yeye kutoshitakiwa au kushtakiwa kwa kosa dogo au kupewa kifungo kidogo. hili lingetumika katika Zombe kesi ingefaa sana. Yule mtuhumiwa aliyefariki na hata yule yule mmoja wa mwisho (simkumbuki jina) walikuwa na taarifa muhimu sana ambazo zingeweza kufanikisha kuwatia baadhi ya watuhumiwa hatiani lakini aidha waliutoa nusu nusu au waliuficha wakijua kuwa hata wao ni watuhumiwa.

Ukiangalia kwa makini wale watuhumiwa wawili walikuwa wanaact on orders and they had crucial information. nafikiri kwa mfumo huo hata yule aliyekufa asingefikia mauti yake kabla hata ya kutoa ushahidi. Najua kuna criticism kuhusu huo mfumo lakini we need to seriously consider it and evaluate its pros and cons. Hii ingesaidia sana hata katika kesi za EPA.
 
Siruhusiwi kuzungumzia kesi iliyopo mahakamani. Ingawa nachelea kusema kuwa kama kwa kosa aliloshitakiwa Zombe na wenzake la mauaji ya wafanyabiashara wa morogoro. Kuna uezekano labda less than 20% kushinda. naona Serikali tu inajikosha kwa ananchi.

Mimi ningefikiri wangeshitakiwa kwa kosa la kupanga mauaji ya wafanyabiashara na hatimaye kuwaua wafanyabiashara wa morogoro.


Naatakia Swaumu njema
Nasriyah
 
Ni kwamba katika hukumu hiyo Jaji aliitwa na Serikali na kuagizwa hakutane wakuu wa wizara ya mambo ya ndani ili kutazama mambo makuu yafuatayo kabla ya hukumu...
Siamini kabisa kama Tanzania wamefikia kiwango hicho cha kuichezea mahakama na sheria zake
 
HATIMA ya Mkuu wa zamani wa Upelelezi mkoani Dar es Salaam, Abdallah Zombe na wenzake tisa ya kurudi kazini ipo mikononi mwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) baada ya mkrugenzi huyo kukamilisha mchakato wa rufani.

Zombe na wenzake Jumatatu walishinda kesi ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini wa Mhaenge, mkoni Morogoro na dereva teksi mmoja mkazi wa Manzese, jijini Dar es salaam iliyokuwa ikiendeshwa katika Mahakama Kuu chini ya Jaji Salum Massati.

Akizungumza katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Msemaji Msaidizi wa jeshi hilo, Suzan Kaganda alisema hati ya watu hao itategemeana sana na serikali upande wa jamhuri kukata rufaa ama la.

"Kwasasa hivi hatuwezi kusema kama watarudi kazini ama la kwa sababu, kwanza hatujapata ile hukumu rasmi mbali ya kusoma katika vyombo vya habari. Labda baada ya siku saba kuanzia leo tutakuwa kwenye nafasi nzuri ya kusema kitu," alisema Kaganda na kuongeza:

"Kusema kama watarudi kazini ama vipi itategemea kama kweli serikali itakata rufaa ama vipi. Kama serikali itakuwa imekata rufaa hatutaweza kusema chochote kwa sababu kesi itakuwa imerudi mahakamani."

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Idara ya Sheria ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu amelilaumu jesho hilo kwa kushindwa kufanya upelelezi wa kutosha katika kesi hiyo.

Alisema Jeshi la Polisi ama lilizembea au lilifanya makusudi kuficha ushahidi wa kumtia hatia Zombe na wenzake.

"Ili mtu aweze kushitakiwa ni lazima kuwepo na ushahidi usio na mashaka kuthibitisha kosa lake. Lakini ushahidi uliopelekwa Mahakama Kuu na jeshi ulikuwa haujitoshelezi.

Ukweli ni kwamba, Watanzania hatuna jeshi la polisi linalofanya kazi kwa maadili. Mimi tangu nianze kazi ya uwakili sijawahi kushindwa kesi na waendesha mashitaka wa polisi. Kwanza hawajui kazi na wamesomea sheria kwa miezi sita tu. Ndiyo maana hata upelelezi walioufanya kwenye kesi ya Zombe ulikuwa ni wa kibabaishaji," alisema Lissu na kuongeza:

"Hata ukiangalia, Zombe alikuwa ni Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Dar es Salaam, hivyo waliofanya upelelezi ni hao hao vijana wake, unadhani wangeweza kumchoma(kumkandamiza)?"

Naye Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia (DP), Mchungaji Christopher Mtikila amesema serikali haikutakiwa kukata rufaa kupinga hukumu ya Zombe na wenzake tisa badala yake ingebadili mashitaka na kuwakamata tena watuhumiwa hao mara baada ya kuachiwa huru.

Akizungumza na Mwananchi jana alisema serikali serikali haikupaswa kushindwa katika kesi hiyo kwa kuwa ilikuwa na kila kitu.

"Mahakama ndio imeshamuachia huru Zombe na wenzake ingawa Watanzania waliamini kuwa watuhumiwa hao wangeswekwa jela, ila serikali imesababisha hali hiyo, kwani ilikuwa na uwezo wa kubadilisha mashitaka na kuwakamata tena akina Zombe," alisema Mtikila na kuongeza:

"Hivi karibuni tumeona katika kesi inayomkabili Liyumba (Amatus), aliachiwa huru, lakini muda huo huo hati ya mashitaka ikabadilishwa na akakamatwa tena, hivyo kitendo cha serikali kusema kuwa itakata rufaa hawa watu wanaweza kukimbia."

Mtikila alisema hukumu hiyo imetokana na jaji huyo kutumia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na kusisitiza kuwa katika kesi yoyote kama ushahidi utatolewa kinyume, hukumu inaweza kuwa tofauti na kosa lenyewe.

Kituo cha Msaada wa Kisheria na Haki Binadamu (LHRC) kwa upande wake kimeunga mkono msimamo wa Jamhuri wa kutokuridhishwa moja kwa moja na hukumu hiyo na sababu zilizotolewa na Jaji Masatti za kuwaachia huru washtakiwa wote katika kesi hiyo.

Akizungumza na Mwananchi juzi Fulgence Massawe alisema LHRC imeipokea hukumu hiyo kwa mkanganyiko mkubwa, kwani kilichotokea ni vigumu kukubalikwa kwa jamii na wanasheria.

Hata hivyo, Massawe alisema hatua ya Jaji Massati kuwaachia huru washtakiwa hao haina maana kuwa hawakuhusika katika mauaji hayo, isipokuwa kwa kosa waliloshtakiwa nalo.

"Hatuwezi kukubaliana moja kwa moja na Jaji Massati kuwa washtakiwa wote wale hawana hatia", alisema wakili Massawe na kuongeza:

"Kuua si lazima wewe uwe 'ume-shoot' umempiga risasi. Kuna kushiriki kosa maana kuna washtakiwa wengine walikiri kuwepo kwenye tukio na hawakuwahi kutoa taarifa za tukio hilo. Katika sheria tunasema acha haki itendeke hata kama anga zitadondoka," alisema wakili Massawe.

Tayari serikali imeanza mchakato rasmi wa kukata rufaa kupinga hukumu ya akina Zombe rasmi jana.

Akizungumza na Mwananchi jana, Wakili wa Serikali, Angaza Mwipopo alisema tayari wamekwishawasilisha taarifa ya kusudio la kukata rufaa kupinga hukumu tangu juzi.

"Tayari tumekwishawasilisha 'notes' (taarifa) ya kukata rufaa tangu jana (juzi)ambayo ndio mwanzo wa mchakato wa rufaa," alisema Mwipopo.

Wakili Mwipopo alisema waliwasilisha taarifa hiyo ya kukata rufaa juzi kwa Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu kwa ajili ya kuipeleka Mahakama ya Rufaa na kwamba, kwa sasa wanachosubiri ni nakala ya hukumu hiyo pamoja na mwenendo wa kesi hiyo.

"Kisheria tulitakiwa kuwasilisha Notes ya nia ya kukata rufaa ndani ya siku 14 tangu siku ya kutolewa hukumu, lakini sisi tumewasilisha baada ya siku moja tu," alisema Mwipopo na kuongeza,

"Kwa hiyo kwa sasa tunasubiri kupata 'copy' ya 'judgement' (nakala ya hukumu), na 'proceedings' (mwenendo wa kesi) ili tuweze kuwasilisha sababu zetu za kukata rufaa," alifafanua Wakili Mwipopo.

Katika hatua nyingine, mmoja wa mawakili wa serikali waliokuwa wakiendesha kesi hiyo walisema hatua ya washtakiwa wote katika kesi hiyo kuachiwa huru kwa maelezo kuwa hakuna ushahidi wa kutosheleza kuwatia hatia, ni kama vile wamefungwa goli la mkono wa Mungu.

Katika hukumu yake aliyoitoa Jumatatu juma hili, Jaji Massati ambaye ni wa Mahakama ya Rufaa, aliwaachia huru washtakiwa wote tisa katika kesi hiyo iliyokuwa ikimhusisha aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Dar es Salaam(RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi(ACP) Abdallah Zombe kwa maelezo kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kuwatia hatiani kwa mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili.

Zombe na wenzake walikuwa wakishtakiwa kwa tuhuma za kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara wa madini Sabinu Chigumbi, Ephram Chigumbi na Mathias Lunkombe toka Mahenge, pamoja na dereva teksi wa Manzese Dar es Salaam Juma Ndugu.

Mbali na Zombe wakishtakiwa wengine waliokuwa wamebakia katika kesi hiyo ambao pia waliachiwa huru juma baada ya watatu kuachiwa katika hatua ya awali na mmoja, Koplo Rashid Lema kufariki dunia April 3 mwaka huu, ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Wilaya ya Kinondoni (OC-CID) Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni, na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa kituo cha Polisi Urafiki Mrakibu Msaidizi wa Polis (ASP) Ahmed Makelle.

Wengine ni WP 4593 PC Jane Andrew, CPL Emmanuel Mabula, PC Michael Sonza, CPL Ebeneth Saro, C/CPL Rajab Bakari na D/CPL Festus Gwabisabi.

Washtakiwa hao walikuwa wanatuhumiwa kwamba, waliwaua wafanyabiashara hao Januari 14, mwaka 2006 katika Msitu wa Pande ulioko Mbezi Luis nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, kwa kuwapiga risasi.
 
Tumechoka na kusikiliza na kusoma mabandiko ambayo actually ni mawazo ya watu. Twambie kwamba umeambiwa na masha au nani siyo unaleta mawazo yako hapa. Katika majeshi yote, hizo nyenzo ulizosema zinatumika tu iweje tanzania zisitumike...

Duh! mh...kweli jeshi na polisi ni kitu kimoja? Sheria za jeshini ni tofauti na za uraiani. Ndo maana zinaitwa Marshal Laws. Na mjeshi anapelekwa katika marshal court. Huwezi fananisha hivi viwili mh.
 
hana jipya kwani uwezekano wa kushinda rufani yake ni mdogo sana.

naona anajaribu tu kuwalaghai wadanganyika kwa uzembe na kukosa umakini katika kufungua kesi hiyo.

Hakika amelitia gharama na aibu serikali
 
Wanatupiga madongo ya macho, hawa wakina Zombe ndio wamekwisha toka hakuna lolote litakalowarudisha lupango!! Walioshitakiwa kesi ya EPA, Mramba, Mgonja na Yona nao wataachiliwa kwa staili hiyo hiyo ya kukosa ushahidi wa kujitosheleza!! Wadanganyika, mnakumbuka kesi ya Kiula? Alipoachiwa, DPP alisema serikali ingekata rufaa mpaka leo Ziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii na hao wakina Zombe itakuwa hivyo hivyo.
 
2852478.jpg

Zombe alipokuwa akitoka mahakamani baada ya kuachiwa huru Wednesday, August 19, 2009 9:32 AM
OFISI ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka nchini imeanza mchakato wa kuwasilisha rufaa ya kukataa maamuzi yaliyotolewa na Makakama Kuu dhidi ya hukumu iliyotolewa dhidi ya Zombe na wenzake Hatua hiyo imekuja baada ya kutoridhishwa na hukumu hiyo iliyotolewa Jumatatu ya wiki hii katika Maakama Kuu dhidi ya washitakiwa hao wa mauaji.

Hivyo kufuatia hukumu hiyo Serikali imeshafikisha rufaa hiyo katika mahakama hiyo kukata rufaa juu ya hukumu hiyo.

Mbali na Serikali wadau mbalimbali wa sheria wakiwemo wanaharakati, wanasheria wanaitaka na sio kuiomba serikali itoe maamuzi haraka juu ya hatua hiyo iliyochukuliwa na Mahakama hiyo nchini.

Hivyo kwa taarifa iliyotolewa jana na ofisi ya mashitaka wamewaomba wananchi watulie na kuitaka sheria ifate mkondo wake.

Hukumu hiyo imefanya wakazi wa jiji na kwingineko kutoridhika na maamuzi hayo yakuwaachia huru washitakiwa hao wa makosa ya mauaji ya kukusudia ya wafanyabiashara watatu wa madini akiwemo na dereva tax mmoja.

Awali Ilidaiwa kuwa aliyekuwa mkuu huyo wa upelelezi Abdallah Zombe aliwagiza maofisa waPolisi kwenda kuwaua wafanyabiashara hao kwa amri.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2852478&&Cat=1
 
Nawaombeni wote mtafakari haya yafuatayo:

1) Ni Watanzania wangapi, wasiokuwa na hatia hata kidogo, wameuwawa wakiwa chini ya ulinzi wa polisi, kuanzia kwenye vituo vidogo (police post) hadi vituo vikubwa (police station) na vituo vikuu (central police station) kuanzia mwaka 2000 hadi leo?

2) Ni Watanzania wangapi, wasiokuwa na hatia hata kidogo, kwa kushindwa tu kujieleza vizuri mahakamani, kwa kuwa hawakuweza kumudu gharama za kulipia utetezi wa wakili, wamefungwa na kwenda jela, tena kwa makosa ya kubambikiza (kwani askari Polisi wamedaiwa kuwafahamu wahalifu halisi, lakini kwa mapatano yao na wahalifu hao wakaamua wabakie mtaani, ili wasio na hatia waende jela badala yao), kuanzia mwaka 2000 hadi leo?

Mkipata majibu ha maswali hayo mawili, basi mtakuwa mmesonga mbele katika kuipata sababu ya Zombe na wenzake kuachiwa huru.

Tuendeleza mjadala.
 
Barubaru!

Wewe kijana una matatizo ya akili! Tatizo ni kwamba waTZ asilimia 90%ni wachovu wa kusoma kama una umri wa kutosha na angalau akili ya kuvuka barabara ya Morogoro au Mandela unayo rejea matukio yafuatayo,,Mtoto wa Rupia aliua mtumishi kwa ajili ya ndoo moja ya maziwa akaachiwa huru (Rupia alikuwa Katibu Mkuu Ikulu); Amran Kombe aliuwawa na Mkapa eti alikuwa jambazi askari walikwisha achiwa; Ditopile kampiga risasi dereva wa Daladala kapewa dhamana!!! Mungu akachukia akampeleka mbele ya haki!!!!

Aliyekuwa Mkurgenzi manispaa ya Temeke aliua mtu kwa risasi hata mahakamani hakufika!! Bado tu huamini na Chenge kaua warembo wawili hata lock up hakufika kwani kushikiliwa angalau kwa siku saba kwa kuua in any circumstances unatakiwa ukae rumande hata kwa usalama wako wasije wafiwa wakakukongoli hilo halikufanyika na nakuhakikishia ukate shingo yangu Andrew Chenge sanasana atapigwa faini.

Sasa wewe barubaru kweli kichwani mwako kuna ubongo au mboji!!! Watu wengine bwana wanachefua jambo dogo tu!!!! hawaelewi je makubwa inakuwaje??????
 
Hi si kweli na sidhani kama huyu aliyekuambia ni afisa wizara ya mambo ya ndani.

Jamhuri ya muungano inmihimili mitatu yaani Bunge,mahakama na serikali(executives).

Na mihimili hii haingiliana kiutendaji wala kimaamuzi. leo inakuwaje eti mahakam imeingiliwa katika maamuzi na serikali?

Nadhani mtoa hoja akajipanga upya kwa hili,nadhani serikali walitakiwa kuwa makini katika shitaka lao hasa katika upelelezi,haingii akilini eti waliangizwa kwa mdomo wakawaue raia wema, wakati kazi ya jeshi la polisi ni kulinda maisha ya raia wema na mali zao.


Post iliyowekwa ina ukweli fulani,kwani mimi nafanya kazi katika wizara hiyo ni kuwa kikao hicho kilifanyika siku kumi kabla ya hukumu hiyo lakini hapakuwepo jaji wal halkimu,alikuqwepo katibu mkuu wa wizara,IGP,Mawaziri eote na watendaji wengine wa wizara hiyo na kutoka jeshi la polisi.

lengo ilikuwa ni kujadili madhara yatakayojitokeza iwapo wenzake na zombe wangeshjtakiwa kuwa wangebadilisha mfumo wa utendaji wa jeshi hilo.

baada ya kikao waliandika ripoti na kuipeleka kwa rais sijui ilikuwa ni ya nini

kwa hiyo katika JF msibeze post kwani hta mimi nimeshangaa imefikiaje humu.

kama mnakumbuka issue kama za EPA,Richmond,nk zilianzia humu kama tetesi na sasa zinaigharamu nchi.

nafanya kila njia kupata ilie ripoti na kuweka hapa

aliweka hii post nadhani atakuwa hapa wizarani
 
Kwahiyo kutokana na hoja hiyo hata yule aleyewaua (ambaye anatafutwa) haina maana kumtafuta maana atamwaga siri zote. Ni kiini macho kingine kwa Watanzania. Polisi hawana mpango wa kuwakamata wahusika.
 
Mimi niloangalia picha za zombe nje ya mahakama(baada ya kuwa huru) zina kupa tawasira kuwa hakuachiwa kwa maana hakuafanya mauaji ila kashinda kwa status yake! hebu kapekue zile picha halafu angalia body language yake
 
Residents shun vote over Zombe acquittal

By Joster Mwangulumbi, Mahenge

The recent acquittal of the assistant commissioner of police, Mr Abdallah Zombe along with eight other police officers, over murder charges, is increasingly becoming expensive to the ruling CCM and its government.

In new twist of events, residents of Epanko ward in Mahenge District, have resolved to boycott the forthcoming civic election exercise to show their discontent to the recent High Court judgement, which found all accused persons not guilty of the grisly murder.

To register their sentiments, they have decided to boycott the opinion polls organised by the ruling party. The polls are meant to screen potential candidates, and to pick the best a CCM members to contest the civic polls against opposition candidates.

Last week, Judge Salum Massati, acquitted ACP Zombe and eight of his colleagues on grounds that the case was not tenable in law.

The acquittal drew criticism from a cross the country, including residents of Mahenge District where the murdered gemstone dealers came from.

The gemstone dealers murdered on January 14, 2006, were Sabinus Chighumbi, Ephraim Chighumbi, and Mathias Lukombe, all residents of Mahenge. The fourth deceased was a Dar es Salaam taxi driver, Juma Ndugu.

The CCM opinion polls in Ulanga District was scheduled to last for three days from August 22 to 24, but CCM members in Epanko and Changamoto branches boycotted the exercise.

Epanko ward is made up of six villages of Epanko Kati, Epanko B, Lui, Itatila, Changamoto and Mbera.

The residents had not only boycotted the opinion polls, but held in a meeting to arrange the demonstration to protest against Judge Masatti's judgement.

But a CCM leader at Changamoto branch, expressed disappointment yesterday when members failed to show up for the exercise.

I was distributed to CCM members wishing to vie for "councillorship in different wards, and many people collected and filled the forms ready for opinion polls today. But since the judgement was pronounced, things have changed," said the branch secretary Mr Pasias Lyanihera.

"The residents now say that there is no need to participate in the process because they have been disappointed by the judgement which set free people whom they call murderers," added Mr Lyanihera.

He said when he asks people to participate in the opinion polls, he always is ridiculed, saying they can not participate in the vote under such circumstances.

"People here have decided to reject this year's polls to elect civic leaders, which means our party will miss candidates," said Mr Lyanihera.

The judgement is also said to have reversed plans by over 300 people to join CCM during the planned visit by the Vice President, Dr Ali Mohammed Shein, in the near future.

According to Epanko village chairman Simon Kuhanga, at his recent meeting with the residents of his village, people agreed to demonstrate today to protest the judgement.

The protest march will cover a distance of 11km from Epanko Primary School to Mahenge town. About 400 artisan miners from communities in the villages where mining is conducted, are expected to participate in the march.

Acquitting the police officers, Judge Massati said: "The case against Mr Zombe and his fellow police officers was not made up, but was based on strong suspicion, which is not sufficient to convict the charged persons."


Source: Citizen (25/08/2009)

Makada wa CCM hili mnaliona?
Kuna haja ya kufanya hivi Mbagala!, Buhemba!, nk?
Nawakilisha!!
 
Back
Top Bottom