Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

yah! Zombe's folks walihakikisha Afande Lema anakufa kabla ya kutoa ushahidi wake pia wakawachinyia baharini akina Afande Saad Alawi ili ionekane wamekimbia na kutishwa msala mzima.

kwa hiyo kesi inaweza kuzaa kesi!
 
Na James Magai

MAWAKILI wa Serikali katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, mkoani Morogoro na dereva wa teksi wa jijini Dar es Salaam, jana walipigilia msumari wa mwisho katika hoja zao na kuainisha kanuni tatu ambazo mahakama inaweza kuzitumia kuwatia hatiani.


Sambamba na kanuni hizo, mawakili hao pia walimkemea na kumtaka mshtakiwa wa kwanza katika kesi hiyo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Abdallah Zombe aache kujifananisha na Yesu Kristo kwa kuwa hastahili kufanya hivyo.


Mawakili hao, ambao ni waendesha Mashtaka, walitoa msimamo huo walipokuwa wanawasilisha hoja zao za mwisho ambazo zilikuwa zikijibu hoja mbalimbali zilizowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi katika kesi hiyo.


Zombe, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam ( RCO) na wenzake tisa, wanashtakiwa kwa makosa manne ya kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara hao katika msitu wa Pande ulio nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.


Katika hoja zao za mwisho, mawakili wa utetezi waliibua changamoto mbalimbali kuhusu ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka wakidai kuwa, umeshindwa kuwahusisha moja kwa moja washtakiwa katika mauaji hayo na kuiomba mahakama iwaachie huru washtakiwa wote.


Lakini jana mawakili hao wa serikali, waliieleza mahakama jinsi washtakiwa hao walivyofanya mauaji hayo kwa kutumia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na mashahidi wa upande wa mashtaka.


Kiongozi wa jopo la mawakili hao, Revocatus Mtaki aliieleza mahakama kuwa kwa mujibu wa sheria, washtakiwa hao wanabanwa kwa kanuni nne kuthibitisha bila shaka kuhusika kwenye mauaji hayo.


Alizitaja kanuni hizo kuwa: Mtu anayeonekana na mtu kwa mara ya mwisho kabla ya mtu huyo kufikwa na mauti ndiye anayepaswa kueleza mazingira yaliyosababisha kifo cha mtu huyo.


"Katika kesi hii ni jambo la kushangaza kuwa, marehemu walikamatwa wakiwa hai na kesho yake wakakutwa wamekufa kwa majeraha ya risasi na washtakiwa hawaelezi mazingira ya vifo vyao," alidai Mtaki.


Katika kuitia nguvu hoja yake Mtaki alirejea kesi moja ambayo mshtakiwa, licha ya kukana kuhusika katika mauaji ya mtu mmoja, hakutaka kueleza ni jinsi gani mtu huyo ambaye kwa mara ya mwisho alikuwa naye, alimtoka na baadaye akakutwa amekufa.


"Mtukufu Jaji, na hawa washtakiwa hawaelezi ni jinsi gani watu waliowakamata wakawafunga pingu baadaye wakakutwa wamekufa. Hili ni jambo la kushangaza," alisisitiza Mtaki.


Mtaki aliieleza mahakama kuwa ingawa ni kweli mshtakiwa wa kwanza Zombe alisema hakuwepo katika maeneo yote ya tukio, na kwamba washtakiwa wengine katika maelezo yao wamekana, walikiri kuwepo katika maeneo ya matukio Sinza na ukuta wa Posta, lakini wakakana kwenda Pande bado hawaelezi kuwa walikuwa wapi.


Aliomba mahakama ione utata wao wa kukana kwenda kwenye eneo la mauaji ambalo ni msitu wa Pande bila kueleza walikuwa wapi kuwa hakutetereshi ushahidi uliotolewa mahakamani na kuiomba mahakama iwatie hatiani wote.


Kanuni ya pili ambayo Wakili Mtaki aliiomba mahakama iitumie kuwatia hatiani washtakiwa hao, ni ya kuwa na nia moja. Aliieleza mahakama kuwa washtakiwa wote walikuwa na nia ya pamoja dhidi ya marehemu.


Alisema kuna ushahidi mbalimbali unaowaunganisha washtakiwa hao kuwa walikuwa na nia ya pamoja tangu kuwakamata marehemu, kutokuwapeleka katika kituo chochote cha polisi, kwenda Pande na kwenda kupongezwa kwa kazi hiyo, kutoa taarifa zisizo sahihi kwenye timu za upelelezi za polisi wala kuripoti tukio hilo mahali popote.


"Hata kwenye Tume ya Jaji Kipenka (Tume ya Rais) ambako walikuwa huru kutoa taarifa sahihi, hawakufanya hivyo," alisema Mtaki.


Alisisitiza kuwa nia ya pamoja si lazima washtakiwa wawe wamekaa na kupanga njama za kufanya uhalifu, na kwamba mwenendo na matendo yao kabla na hata baada ya tukio unaweza kuthibitisha kanuni hiyo.


Mtaki aliitaja kanuni nyingine kuwa ni maelezo ya ungamo ambayo mshtakiwa huyo alitoa mbele ya mlinzi wa amani, ambaye ni hakimu wa mahakama ya mwanzo akikiri kosa.


Mtaki alisema katika maelezo yaliyo mahakamani yamewataja na washtakiwa wengine pia katika kesi hiyo.


"Kwa hiyo tunaomba mahakama yako tukufu izingatie hizo kanuni na kwa ushahidi wote uliotolewa mahakamani hapa iwaone kuwa washtakiwa wote wana hatia," alisema Mtaki.


Hata hivyo, Mtaki katika kuhakikisha kuwa washtakiwa wote hawaponi katika ghadhabu ya mkono wa sheria, aliiomba mahakama iwatie hatiani kwa kosa mbadala Zombe na mshtakiwa wa 13, Koplo Festus Gwabisaba, ikiwa mahakama itaridhika kuwa hawahusiki kwa kuwa kwa ushahidi ulioko mahakamani, wao hawakwenda katika eneo la mauaji katika Msitu wa Pande.


"Kama mahakama itaona kuwa mshtakiwa wa kwanza (Zombe) na wa 13 (Gwabisabi) hawakushiriki katika mauaji kwa kuwa kwa ushahidi ulioko mahakamani hawakwenda Pande, basi iwatie hatiani kwa kosa Accessory after the facts (mshiriki baada ya kosa) chini ya kifungu cha 213,387(i) na 388 cha Penal Code," alidai Mtaki.


Mtaki aliieleza mahakama kuwa kila kesi huamuliwa kwa mazingira yake na kuitaka mahakama kuzingatia mazingira ya kesi hiyo ambayo alisema kuwa washtakiwa wote ni askari polisi, baadhi yao wakiwa ni maofisa na wapelelezi walio na uzoefu.


"Kwa hali hiyo shauri hili linapaswa lipewe mtazamo wa kipekee kabisa kwa kuzingatia ushahidi wa pande zote na hatimaye mahakama yako tukufu iweze kufikia uamuzi wa haki ambao sisi tunaamini kuwa washtakiwa wote wana hatia ya mashtaka haya," alisisitiza Mtaki.


Awali, akianza kutoa hoja zake za mwisho kujibu hoja za mawakili wa utetezi, Mtaki aliieleza mahakama kuwa kwa mujibu wa sheria upande wa mashtaka walikuwa na jukumu la kuthibitisha mambo manne katika kesi hiyo.


Aliyataja mambo hayo kuwa ni kuthibitisha kuwa marehemu walikufa, kwamba walikufa vifo visivyo vya kawaida, kwamba washtakiwa ndio waliowaua na kwamba washtakiwa hao walikuwa na nia ovu katika kutenda kosa hilo.


"Mtukufu Jaji, katika kutekeleza jukumu hili tuliita mashahidi 37 na kutoa vielelezo 25 na ni rai yetu kuwa tumelitimiza jukumu hilo mbele ya mahakama hii," alisema Mtaki na kutaja mashahidi waliohusika kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao katika kila kipengele.


"Tumetoa ushahidi mwingi kuthibitisha marehemu hao wanne walikufa; tumethibitisha kuwa walikufa vifo visivyo vya kawaida kwa kuwa marehemu wote walikutwa wakiwa na majeraha ya risasi shingoni zilizopigwa kutokea nyuma na kutokeza kwa mbele," alidai Mtaki na kuongeza:


"Hiyo inaonyesha hivyo si vifo vya kawaida wala ajali. Ni rai yetu kuwa ile dhana ya kwamba kulikuwa na mapambano baina ya marehemu na polisi haina nguvu kwa sababu risasi zisingetokea shingoni wote. Parten Shooting ilikuwa Systematic."


Mtaki aliieleza mahakama jinsi walivyotekeleza jukumu lao kwa kuwaunganisha washtakiwa na mauaji hayo kwa pamoja na kisha kuainisha kila mshtakiwa jinsi alivyohusika akitumia ushahidi mbalimbali uliotolewa mahakamani hapo.


Katika kuongeza nguvu hoja zake wakati akiithibitishia mahakama jinsi mshtakiwa mmoja mmoja alivyotiwa hatiani na ushahidi bila kuacha mashaka, Mtaki aliiomba mahakama pia izingatie sababu ambazo ilizitumia katika uamuzi wake kuwa washtakiwa hao walikuwa na kesi ya kujibu.


Akihitimisha ushahidi jinsi unavyomhusisha Zombe na mauaji hayo, Mtaki alimtaka mshtakiwa huyo asijifananishe na Yesu kama ambavyo wakati wa hoja zake za mwisho wakili wake Jerome Msemwa alimfananisha.


Msemwa katika kuhitimisha hoja zake Mei 7 mwaka huu aliieleza mahakama kuwa mteja wake (Zombe) ni kama Yesu Kristo, kwani ameshtakiwa katika kesi hiyo bila kosa kama Wayahudi walivyomshtaki na kumsulubisha Yesu bila hatia.


Msemwa aliitahadharisha pia mahakama kutoa hukumu yake kwa haki si kama Pilato alivyomhukumu Yesu hata bila kuwa na hatia na kwamba baada ya kifo chake ndipo Wayahudi hao wakaona kuwa hakika alikuwa ni Mwana wa Mungu na kwamba hakuwa na kosa.


Akijibu hoja hiyo jana, Mtaki alisema Zombe hastahili kufananishwa na Yesu kwa sababu kwanza, licha ya jaji wa ile kesi ya Yesu alikuwa Pilato ambaye alikuwa katili sana, aliwauliza Wayahudi kuwa walikuwa na ushahidi gani dhidi ya Yesu na hakuna aliyejibu, badala yake wakapiga kelele tu kuwa asulubiwe.


"Sisi hatukupiga kelele, tumeleta ushahidi kamili hapa mahakamani. Tofauti na Pilato, wewe Mtukufu Jaji ni mtu wa haki unazingatia haki na utatoa uamuzi wa haki. Hivyo kwa mfano huu mshtakiwa wa kwanza asilinganishwe na Yesu," alisema Mtaki.


Akizungumzia ushahidi wa aliyekuwa mshtakiwa wa 11, marehemu Koplo Rashid Lema ambao ulipingwa na mawakili wa utetezi, Mtaki aliieleza mahakama kuwa ushahidi wake ni halali kutumika mahakamani kwa kuwa wakati maelezo yake yakiwasilishwa mahakamani, alikuwapo.


"Ingawa maelezo yake yalipingwa na baadhi ya washtakiwa, yeye aliyakubali kuwa ni yake na kwamba ndivyo alivyoyatoa. Hivyo ingawa amekufa, ushahidi wake utaendelea kutumika kwa sababu tayari ulishafanyiwa ‘Cross examination' (mahojiano ya uhakiki) kupitia kwa mashahidi waliouwasilisha," alisema.


Lema alitoa maelezo hayo kwa hiari kwa Mlinzi wa Amani na maelezo yake ndiyo yaliyoeleza mauaji hayo yalivyofanyika katika Msitu wa Pande. Maelezo hayo ya Koplo Lema yanaungwa mkono na maelezo ya mshtakiwa wa 12, Koplo Rajabu Bakari.


Baada ya mawakili wa serikali kumaliza kuwasilisha hoja zake kwa kutumia saa 3.10, Jaji Salim Masatti aliahirisha kesi hiyo kwa muda na baadaye kutoa muhtasari wa mwenendo mzima wa kesi kwa wazee wa Baraza ili nao waweze kutoa maoni yao kama washtakiwa wana hatia.


Akitoa muhtasari huo, Jaji Masatti pia aliwaelekeza wazee hao wa baraza namna ya kutoa maoni yao na kuwataka kutoyumbishwa na mambo yote waliyoyasikia hasa kwenye vyombo vya habari, huku akiwataka wazingatie ushahidi ulioko mahakamani.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi leo saa 8:00 wakati wazee hao watakapotoa maoni yao na baadaye Jaji Masatti atatangaza siku ya hukumu.


Zombe na wenzake tisa wanatuhumiwa kuwaua kwa makusudi wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge-Sabinus Chigumbi (maarufu kama Jongo), Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva wa teksi wa Manzese jijini Dar es Salaam, Juma Ndugu.


Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni SP Christopher Bageni, ASP Ahmed Makelle, WP Jane Andrew, Koplo Emmanuel Mabula, Michael Sonza, Ebeneth Saro, Rajab Bakari na Festus Gwabisaba.


Washtakiwa hao wanadaiwa kufanya mauaji hayo Januari 14, 2006 katika Msitu wa Pande ulio wilayani Kinondoni, nje ya jiji la Dar es Salaam

source;mwananchi
 
sasa sijaelewa bado kama hakimu kasema wako guilty hawa wazee wa baraza wao shughuli yao ni nini? hebu tufafanulieni mnaoijua sheria ya nchini kwetu!
 
Nilikuwa sijaipata hii ya Zombe kujifananisha ya Yesu..lol. Watu wengine bana yaani badala ya kujitetea kwa hoja zisizo shaka wanaleta makufuru.

Sasa kwanini uongee crime wakati unaogopa jela?
 
Wana JK kuna mtu ameuliza namna ya kutoa maji yaliyoingia sikioni wakati wa kuogelea. Simple, tia maji kwenye sikio (yes tia maji) halafu inama upande wa hilo sikio na maji yote yataka. Najua kutakuwa na woga kufanya hivyo lakini trust me, yatatoka kirahiisi kabisa
 
Hawa wapo watakao somewa vifungo vifupi wapo watakao toka subilini.
 
Kwa mujibu wa maelezo ya hakimu leo,kupitia radio-one stereo:

Washtakiwa wooooote wakiongozwa na Zombe mwenyewe wamekutwa na hatia,na watahukumiwa kwa mujibu wa sheria!

Hakimu ameongea mengi sana,akizungumza ukiukwaji wa maadili ya taaluma kwa maaskari hao.Pia ameelezea namna alivyopitia upande wa ushahidi dhidi yao na kutoa hitimisho WOTE WANA HATIA!na watahukumiwa

Kesi itaendelea tena kesho,baada ya baraza la wazee kukaa
!


WAKUU,nadhani tupo kwenye episode ya mwisho mwisho,stay tuned!
Learned brothers mnisaidie; hawa wazee wa baraza wanaweza kuinfluence hukumu kwa kiasi gani; to put into perspective; assume hakimu alishaona kwa mujibu wa sheria mtuhumiwa anatakiwa afungwe maisha je wazee wa baraza wanaweza wakajenga hoja hadi hakimu akashawishika kubadili hukumu? Pls help.
 
Learned brothers mnisaidie; hawa wazee wa baraza wanaweza kuinfluence hukumu kwa kiasi gani; to put into perspective; assume hakimu alishaona kwa mujibu wa sheria mtuhumiwa anatakiwa afungwe maisha je wazee wa baraza wanaweza wakajenga hoja hadi hakimu akashawishika kubadili hukumu? Pls help.

katika level fulani ya mahakama ni lazima wawepo,katika kumuadvice hakimu,HIZI NI PROTOCALS za mambo ya mahakamani mkuu!

On the serious note:hawa watu ni knowledgable na mambo ya kesi,mara nyingi wanakuwaga ni mahakimu wastaafu.

ikumbukwe kwamba wanamuadvice tu hakimu!
 
Wana JK kuna mtu ameuliza namna ya kutoa maji yaliyoingia sikioni wakati wa kuogelea. Simple, tia maji kwenye sikio (yes tia maji) halafu inama upande wa hilo sikio na maji yote yataka. Najua kutakuwa na woga kufanya hivyo lakini trust me, yatatoka kirahiisi kabisa

Mazee umejibu vyema. Ila ingependeza iwapo hili jibu ungeliweka kwenye thread husika hapa. Ingependeza zaidi.

By the way, karibu jamvini sheikh. Halaf una undugu na Yahaya wa Barca? 😀
 
katika level fulani ya mahakama ni lazima wawepo,katika kumuadvice hakimu,HIZI NI PROTOCALS za mambo ya mahakamani mkuu!

On the serious note:hawa watu ni knowledgable na mambo ya kesi,mara nyingi wanakuwaga ni mahakimu wastaafu.

ikumbukwe kwamba wanamuadvice tu hakimu!

Thanks for clarification.
 
Wana JK kuna mtu ameuliza namna ya kutoa maji yaliyoingia sikioni wakati wa kuogelea. Simple, tia maji kwenye sikio (yes tia maji) halafu inama upande wa hilo sikio na maji yote yataka. Najua kutakuwa na woga kufanya hivyo lakini trust me, yatatoka kirahiisi kabisa

Kweli kuna watu wako-careless, JK au JF? Na hii thread ya kutoa maji kwenye sikio imetoka wapi hapa? Tuwe serious na makini wajameni
 
yaani huyu Zombe anyongwe!! ametesa sana watu na sasa anavuna alichopanda..Mi niliwahikwenda pale central kumuwekee dhamani dereva wangu yaani kwa macho yangu kuna kibaka aliletwa akawa anamuhoji akamzimia sigara kivuani!!! yule kijana alipata maumivu sana
 
Jamani hii haijakaa vizuri habari haielezi ukweli wa matukio.

Kwa mujibu wa maelezo ya hakimu leo,kupitia radio-one stereo:

anayesikiliza kesi hiyo ni jaji na sio hakimu.

Washtakiwa wooooote wakiongozwa na Zombe mwenyewe wamekutwa na hatia,

Hawajakutwa na hatia bado, kilichofanyika ni jaji kutoa mwongozo kwa washauri wa mahakama ili wamsaidie kufikia uamuzi.( angalia habari gazeti la mwananchi aya ya nne toka mwisho) Katika kesi za mauaji Jaji anashirikiana na washauri wa Mahakama ( court assessors) katika baadhi ya vitu.

watahukumiwa kwa mujibu wa sheria!

Hii itakuwa baada ya Jaji kuwakuta na hatia baada ya kuchambua ushahidi wa pande zote mbili ( mashtaka na utetezi), maelezo ya mwisho ( final submissions) na maoni ya washauri wa Mahakama na kuandika hukumu.

Hakimu ( Jaji ) ameongea mengi sana,akizungumza ukiukwaji wa maadili ya taaluma kwa maaskari hao.Pia ameelezea namna alivyopitia upande wa ushahidi dhidi yao na kutoa hitimisho WOTE WANA HATIA!na watahukumiwa ( hawana hatia bado kama ilivyoelezwa hapo juu)
 
Back
Top Bottom