Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Hii yote ni maigizo. Serikali na Jeshi la Polisi lilikuwa linajua fika kuwa Polisi mmoja ametoroka na ndie muuwaji walikuwa wapi miaka 3 kumtafuta hadi mahakama iseme kuwa muhusika afikishwa mahakamani inamaana walikuwa hawajui mtuhumiwa anatakiwa kutafutwa kwa udi na uvumba popote alipo duniani ili aje ashtakiwe?

2. Hapa tunadanganywa kama watoto wadogo mauwaji yalifanyika tangu 2006 watuhumiwa wamekaa ndani (mahabusu) miaka 3 uchaguzi mwakani,kwahiyo hapa ni propaganda za kujisafisha kuelekea ktk uchaguzi mwakani. Watajipanga kukata rufaa hadi watakapo maliza kujipanga mwaka huu umekwisha.

3. Hivi kesi za wanajeshi wawe JWTZ,JKT,FFU,MAGEREZA,NAVY,ANGA na hata POLISI si huwa wanakuwa na mahakama za kejeshi huwa wanashtakiwa kijeshi ama hapa kwetu hatuna mahakama za kijeshi??
 
Tunachojiuliza baadhi yetu ni kama UANASHERIA ni TAALUMA? Haiwezekani Serikali IKAUA, kisha IKAPELELEZA, IKASHTAKI, IKAENDESHA MASHTAKA halafu ikasubiri MAHAKAMA itoe HAKI kwake! Yote haya kwa gharama ya mlipa KODI wa NCHI hii!
Waachieni haraka akina Mramba, watu wa EPA ili gharama kubwa zinazotumika kuendesha kesi hizi zikanunue madawati mashuleni.
 
Home
arrow.png

*Yaomba wananchi wote wawe watulivu
*Jaji Kipenka, DCI Manumba wazungumza
*Wanasheria waponda utendaji ofisi ya DPP

Na Waandishi Wetu

SIKU moja baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam kuwaachia washitakiwa wa kesi ya mauaji ya wafanyabiashara iliyomhusisha Bw. Abdallah Zombe na wenzake wanane, Serikali imesema haijaridhishwa na uamuzi huo, hivyo imeanza mchakato wa kukata rufaa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari, Dar es Salaam jana na kusainiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mashitaka, Bi. Mary Lyimo, alieleza ;

"Tunaanza mchakato wa kukata rufaa kwa kutoa taarifa ya nia ya kukata rufaa katika Mahakama ya Rufaa Tanzania ambayo ndiyo ya juu kabisa na ya mwisho yenye kutoa msimamo sahihi wa kisheria."

Kufuatia hatua hiyo, Bi. Lyimo aliwaomba wananchi kuwa watulivu wakati taratibu hizo za kisheria zikiendelea na watafahamishwa maendeleo yake.

Wakati Serikali ikijipanga kukata rufaa, wanasheria nchini wametafsiri uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu wa kuwaachia washitakiwa hao kama msiba kwa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP), hivyo imeshauri kutokurupuka kukata rufaa kufuata shinikizo lililopo sasa kutoka kwa wananchi.

Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti, Dar es Salaam jana, wanasheria waliobobea katika taaluma hiyo, walisema katika historia ya nchi hii haijawahi kutokea ofisi ya DPP ikashindwa kesi vibaya kama ilivyotokea kwa hii ya Bw. Zombe na wenzake.

Akizungumza na gazeti hili mwanasheria aliyebobea kwenye masuala ya ushahidi , Profesa Abdallah Safari, alisema;

"Kwa kesi kama hii DPP alitakiwa kuwa makini, kama aliona ushahidi aliopelekewa na DCI ( Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai) haujitoshelezi angemrudishia na siyo kusukumwa na matakwa ya watu."

Alisema waliohusika kufanya upelelezi wa kesi hiyo ni Polisi ambao wapo chini ya DCI, hivyo kwa mazingira ya kawaida ni vigumu askari kuwapeleleza wenzao na kuja na ushahidi mzito wa kuwatia hatiani.

"Hii inaleta mkanganyiko ni kwa nini Polisi hawakuwatafuta waliowaua wafanyabiashara hao na kuwafikisha mahakamani?"Alihoji Prof. Safari na kuongeza kuwa kabla ya kesi kufikishwa mahakamani ni lazima DPP ajiridhishe kuwa kuna kesi inatakiwa kufunguliwa na pili awe na uhakika na ushahidi alionao kuwa utampatia ushindi mahakamani.

Alifafanua kuwa yeye aliwahi kuwa wakili wa Serikali Kanda ya Mbeya na kuna wakati alikuwa akipelekewa vielelezo vya kesi zikiwemo za mauaji zinazotakiwa kufunguliwa na alipoona hakuna ushahidi wa kutosha, alirejesha majalada kwa wapelelezi.

Pia alibainisha kuwa inawezekana kwenye kesi hiyo ushahidi ulikuwa unajitosheleza kuwatia washitakiwa hatiani, lakini ukawa umepwaya kutokana na jinsi ulivyowasilishwa na mawakili wa Serikali.

"Matokeo yake washitakiwa wameachiwa na watu hawana imani na vyombo vya dola," alisema na kuongeza kuwa hiyo imeleta picha mbaya kwa umma.

"Raia watiifu wameuawa mikononi mwa polisi, tena kwa kupigwa risasi na fedha zao zikachukuliwa...halafu ofisi ya DPP inashindwa kuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani!"Alisema kwa mshangao.

Kutokana na hali hiyo, Prof. Safari alisema kilichotokea kwenye ofisi ya DPP ni msiba. Alisema kama ofisi hiyo ina mpango wa kukata rufaa, isifanye hivyo kwa shinikizo lililopo badala yake itulie na kuwatafuta mawakili wanaojitegemea (anataja majina) ili waweze kusaidia ukataji rufaa.

"Inawezekana kuna makosa yametendeka katika nyanja mbili, wakati wa uwasilishaji ushahidi au katika upelelezi uliofanywa na ofisi ya DCI, watulie, ikibidi wasisite kupata msaada wa watu wengine nje ya ofisi ya DPP," alisema Prof Safari.

Akizungumzia watu hao kufia mikononi mwa Polisi, alisema hiyo ni kashfa nzito kwani hata wakati wa mkoloni haikuwahi kutokea.

"Polisi ndiyo wenye siri kubwa, watu wanashindwa kuwa na imani nao kwasababu wamefia mikononi mwao," alisema.

Alipoulizwa kama hatua ya kufikishwa mahakamani kwa watuhumiwa hao kulikuwa na shinikizo la kisiasa, Prof. Safari alikiri kuwa hilo linawezekana kwani Serikali ilitaka kuwadhihirishia wananchi kuwa inaweza kuchukua hatua, hasa baada ya kuandamwa na kashfa kadhaa.

Kwa upande wake, DCI, Bw. Robert Manumba, alipoulizwa ana maoni gani kuhusu madai yanayotolewa kuwa ushahidi uliokusanywa na polisi ulikuwa mwepesi ndiyo maana washitakiwa waliachiwa, alisema hakuwa na jibu.

"Sina maoni yoyote siwezi kusema ushahidi ulikuwa mzito au mwepesi," alisema kisha kukata simu.

Kwa upande wake wake, Jaji Kipenka Mussa, ambaye aliongoza Tume iliyoundwa na Rais Jakaya kikwete kuchunguza utata wa mauaji hayo na kubaini kuwa waliouawa hawakuwa majambazi, alipoulizwa ana maoni gani kuhusu hukumu hiyo, alijibu; " No comment!"

Gazeti hili lilipozidi kumdodosa hasa kuhusu umma alivyopokea hukumu hiyo, alijibu;
"Sisi haturuhusiwi kutoa comments (maoni), No comments! I am not going to give any comments! (akimaanisha sina cha kuzungumza, sitasema chochote), au unataka nikufanyie ujeuri wa kukukatia simu?," alihoji Jaji huyo.

Kwa upande wake wakili wa kujitegemea Bw. Tindu Lissu, alisema, wapelelezi wa polisi wanapaswa kubebeshwa lawama kwa kupeleka ushahidi hafifu mahakamani.

Alidai kuwa kwa jinsi ambavyo polisi wamekuwa wakihusika katika baadhi ya natukio ya uhalifu, utendaji mbovu, rushwa na uozo mwingine, kuna uwezekano mkubwa kuwa upelelezi haukufanyika vizuri.

"Ninachokwambia hapa ni possibility (uwezekano), kwa kuangalia hali halisi, sio fact (usahihi) maana ingebidi tutoe ushahidi lakini katika hili ushahidi wa polisi ulikuwa wa namna gani?

Unategemea polisi wanaofanya maovu wachunguze maovu? Ili mtu ahukumiwe kufungwa au kunyongwa lazima utolewe ushahidi usiokuwa na mashaka yoyote ya msingi," alisema Bw. Lissu.

Aliongeza kusema kuwa wasiwasi uliooneshwa na watu baada ya hukumu ya kusomwa unaonesha ni kiasi wananchi hawana imani na vyombo vya utoaji haki.

"Watu wanajua kinachofanyika katika vyombo vya dola, kuanzia kwa Jeshi la Polisi, Mahakama na kwingineko ambako haki inatolewa kwa kuangalia misingi ya wenye pesa na wasiokuwa na pesa," alisema Bw. Lissu.

Pia alishangazwa na waendesha mashitaka kushindwa kuwafungulia washtakiwa hao makosa madogo mpaka makubwa ili hata kama hawakushiriki moja kwa moja katika mauaji bado wangeweza kupatikana na hatia sehemu nyingine.

"Mwendesha mashitaka mzuri anapaswa kumshitaki mtu kuanzia makosa madogo mpaka makubwa. Kwa mfano kuna ushahidi ulitolewa kuwa Zombe alikwenda Kituo cha Polisi kuvuruga ushahidi, kwa nini hawakumshtaki kwa kosa la kuvuruga haki isitendeke?" Alihoji.

Akitoa maoni yake kuhusu uamuzi uliotolewa na Mahakama Kuu, Mwenyekiti wa TPP-Maendeleo, Bw. Peter Mziray, alisema unaweza kumharibia Rais Kikwete na kumfanya apoteze imani ambayo wananchi waliyokuwa nayo kwake tangu washitakiwa hao walipofikishwa mahakamani.

Mbali na athari hiyo, alisema sheria zina udhaifu mkubwa na kuwafanya majaji washindwe kutenda haki. "Kama sheria inasema aliyeua hayupo, basi ni mbovu haitufai!" Alisema.

Alisema majaji wanafuata sheria kuliko namna ya kutoa haki. Alisema hawapaswi tu kuangalia nini sheria inasema, bali wanatakiwa kutoa uamuzi wao kwa kuangalia mazingira na namna ya kutenda haki.

Bw. Mziray alisema kuwa Mahakama imeelezwa katika Katiba kuwa ni chombo cha kutoa haki, lakini haki hiyo haitendeke kutokana na majaji na wanasheria kujikita kwenye sheria zaidi.

Juzi Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Salum Massati aliwaachia huru washtakiwa waaliokuwa wakikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabishara wanne wa madini, kutoka Mahenge, Morogoro na dereva teksi wa Dar es Salaam baada ya kujiridhisha kuwa hawakuhusika katika tukio hilo.

Waliochiwa huru ni pamoja na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Zombe, ASP Christopher Bageni, ACP Ahmed Makelle, WP 4593 PC Jane Andrew, Koplo Emmanuel Mabula, PC Michael Sonza, Koplo Ebeneth Salo, Koplo Rajabu Bakari na Festus Gwabisabi.

Taarifa hii imetayarishwa na Reuben Kagaruiki, Edmund Mihale, Tumaini Makene na Peter Masangwa.
 
roho inaniuma sana watu hawa wanavyochezea hela zetu.
hivi kweli jk roho haimuumi watu wake wanavyodanganywa???
kila chenye mwanzo kina mwisho mungu wabariki watanzania
 
Jambazi wa NMB wa wizi uliofanyika wiki mbili tu zilizopita, kwa kuwa aliua askari ameshakamatwa, askari aliyeua na kutoroka miaka mitatu iliyopita hajapatikana hadi leo! @@***#%&*!!!!?????? eti sasa ndio wataongeza nguvu! kuna jambo........ polisi wamechangia sana kuanguka kwa serikali katika kesi hii ili kuwaokoka wenzao na kitanzi.
 
sasa wanalipwa mishahara kwa kodi za wananchi kwa kazi gani wanayoifanya kama wanashindwa hata kupeleka ushaidi wa kujitosheleza mahakamani,hiyo ndo sheria ya makosa ya jinai baba whenever there is a doubt with the evidence,the benefit of doubts favours the accused
 
Wakuu,hivi punde nimetonywa na kiongozi mmoja kutoka katika Wizara ya Mambo ya Ndani (Ni mtu ninayeheshimu maneno yake) sababu iliyopelekea zombe kuachiwa mbali na hukumu ya jaji ilivyosema.

Ni kwamba katika hukumu hiyo Jaji aliitwa na Serikali na kuagizwa hakutane wakuu wa wizara ya mambo ya ndani ili kutazama mambo makuu yafuatayo kabla ya hukumu.

Ni kuwa mfumo wa jeshi la polisi nchini tanzania uendeshwa klwa maagizo yasiyo kwenye maandishi yahani IGP,RPC,RCO nk hutoa maagizo ya mdomo kwa walioko chini yao.

hivyo katika tukio la akina zombe ndivyo ilivyofanyika kwa maana kuwa ilidaiwa kuwa wale waliotekeleza mauaji waliagizwa na wa,kubwa wao.

Lakini ni kuwa iwapo washtakiwa chini ya zombe au zombe mwenyewe wangehukumiwa asdhabu yoyote basi utaratibu wa polisi wa kufanya kazi kwa maagizo ya mdogo,simu nk ungekuwa umefutwa rasmi hali ambayo serikali iliona inaweza kuleta tatizo katika uendeshaji wa jeshi la polisi nchini.

hapa ni kwamba OCD hasingeweza kumpigia simu koplo na kuagiza kumkamata mwizi fulani mpaka yawepo maandishi.

nimeamua niweke hapa ili baadhi yetu tujue hilo,au kama kuna mwenye habari zaidi kuhusu kilichojiri katika kikao hicho wamwage hapa !
 
Maneno yako ni ya kubuni kwa kiasi kikubwa mbona vyanzo vya habari hii hukuweka??
 
duh! Kwa hiyo bongo unakamatwa bila amri ya wakubwa? Na kama huyu judge ameamua kufanya hivyo...ni ****! Angetakiwa ajitoe muhanga for real change!
 
Nji hii bwana we acha tu!

Inaudhi,inasikitisha na inachefua sana kuona kuwa DPP na Wanasheria wa nji hii wameshindwa kabisa kumtia hatiani Zombie na washirika wake katika mauaji haya.

Kwa kifupi na kwa uchungu nasema hivi WANASHERIA WETU NI VIHIYO KWA ASILIMIA 100. Huwezi kundesha kesi kwa miaka 3 huku ukiwa na vidhibiti vyote halafu mwisho wa siku unatuambia hakuna aliyeua. HAPA SHERIA HAIKUCHUKUA MKONDO WAKE baali umetumika usanii na ubabaishaji wa kisheria.

Nasema tena kwa herufi kubwa kwamba WANASHERIA WETU NI VIHIYO na ndiyo maana hata mikataba mingi ya Wawekezaji hapa Tanzania wanaingia kusaini mikataba ya KIHUNI ambayo mtu ukiisoma kwa makini unajiuliza mara mbili mbili kuwa hawa WANASHERIA WETU wanaposaini hii mikataba wanakuwa wamelala,hawaelewi?Ni rushwa?Ni lugha inawapiga chenga au ni nini hasa???Majibu ya maswali haya ni KUWA WAO NI VIHIYO.

Katika hili vilevile sitaacha kuwasema POLISI. JESHI LETU LA POLISI hamuna kitu. Huko nako kumejaa VIHIYO watupu. Wapo kwa ajili ya kukamata vibaka wanaoiba kuku mitaani hawa ndiyo wanaowakomalia na kuwafunga. Lakini ikija kwenye kesi kubwa kama za Kina Zombie hakuna kitu. Ni wizi mtupu.

Pengine ndiyo maana kesi nyingi za mauaji zinachukua muda mrefu sana kusikilizwa na mwisho wake ni watuhumiwa kuachiwa huru. Mara nyingi wananchi wamekuwa wanaamua kuchukua sheria mkononi kwa hofu kama hizi kuwa MTUHUMIWA AMEKAMATWA RED HANDED LAKINI AKISHA FIKA POLISI TU BAADA YA MUDA UNAMWONA MITAANI ANADUNDA NA HATA KUKUZOMEA WEWE ULIYEMFUNGULIA MASHTAKA!!!

Hivi hawa ndugu za marehemu wafanya biashara waliouawa na kina Zombie wakiamua KUCHUKUA SHERIA MKONONI WATAKUWA WAMEKOSEA???

Leo unatuambia eti unamtafuta muuaji wa hawa watu anaitwa Koplo Saad Alawi. Miaka yote 3 mlikuwa hamjui kuwa yeye ndiye muuaji???Hata kama atapatikana ni kweli ndiye aliyekurupuka tu from nowhere akachukua bunduki na kuwapeleka msitu wa Pande kwenda kuwaua tena akiwa peke yake pasi na amri za kina Zombie???Kuwa Koplo Saad Alawi ndiye aliyewakamata,akawanyang'anya zile pesa milioni 5,akawapakia kwenye gari la Polisi,akaendesha mpaka msitu wa Pande, akawapiga risasi na akarudi barracks akiwa peke yake!!!!.HAIWEZEKANI HATA KIDOGO.

Acheni porojo za kisanii enyi WANASHERIA NA POLISI. Mshukru tu kwamba Tanzania ni nji ya amani ambaye watu wake ni wapole na waungwana kupita kiasi.

Nawahakikishieni hukumu hii ingelitolewa nchi za wenzetu ambao hawataki ubabaishaji hiyo juzi hapa Dar pangekuwa hapakaliki. Watu wangelifanya riot na maandamano ya kupinga upuuzi kama huu. Lakini Wa-tz kimya, kama vile wananyolewa. Kwa kweli upole mwingine ni kama ujinga au uzezeta fulani.

Tujipe poole sana Wa-tz.
 
Last edited:
Wakuu,hivi punde nimetonywa na kiongozi mmoja kutoka katika Wizara ya Mambo ya Ndani (Ni mtu ninayeheshimu maneno yake) sababu iliyopelekea zombe kuachiwa mbali na hukumu ya jaji ilivyosema.

Ni kwamba katika hukumu hiyo Jaji aliitwa na Serikali na kuagizwa hakutane wakuu wa wizara ya mambo ya ndani ili kutazama mambo makuu yafuatayo kabla ya hukumu.

Ni kuwa mfumo wa jeshi la polisi nchini tanzania uendeshwa klwa maagizo yasiyo kwenye maandishi yahani IGP,RPC,RCO nk hutoa maagizo ya mdomo kwa walioko chini yao.

hivyo katika tukio la akina zombe ndivyo ilivyofanyika kwa maana kuwa ilidaiwa kuwa wale waliotekeleza mauaji waliagizwa na wa,kubwa wao.

Lakini ni kuwa iwapo washtakiwa chini ya zombe au zombe mwenyewe wangehukumiwa asdhabu yoyote basi utaratibu wa polisi wa kufanya kazi kwa maagizo ya mdogo,simu nk ungekuwa umefutwa rasmi hali ambayo serikali iliona inaweza kuleta tatizo katika uendeshaji wa jeshi la polisi nchini.

hapa ni kwamba OCD hasingeweza kumpigia simu koplo na kuagiza kumkamata mwizi fulani mpaka yawepo maandishi.

nimeamua niweke hapa ili baadhi yetu tujue hilo,au kama kuna mwenye habari zaidi kuhusu kilichojiri katika kikao hicho wamwage hapa !


Siamini maneno yako,nahisi ni kama umeeleza hisia zako,na pia ningeshauri kwa sasa tuachane na mambo ya kina Zombe tuendelee na mambo mengine,maana hili nalo naona linatuchukulia sana muda.
 
hujasema lolote la maana. wale wameua...kama walipewa maagizo ya maandishi, simu au ishara yoyote, basi kuna mtu alitoa maangizo hayo au hiyo ishara.
 
We are going to hear a lot of theories kuhusu hukumu hii ya Kina Zombe et al.
 
Mkuu kama kweli jaji aliitwa na kupewa order na wakuu wa wizara ya mambo ya ndani, ina maana sasa tuamini kuwa mahakama haiko huru. Ni branch ya executive na inapokea orders za kubananga sheria kwa interest za executive. Kama tumefikia hali hiyo basi mahakama haina maana tena ni afadhari tubaki na executive ifanye kila kitu.
 
Hivi wajameni, hawa DPP wako serious au ni kwamba wanazuga tuuuuuuuuuu??? Hebu tusubiri ndani ya siku 14 tuone!!! Sasa jamaa wako nje si ndiyo watafanya maajabu kuwashughulikia mashahidi!/kuharibu ushahidi???!!!
 
duh! Kwa hiyo bongo unakamatwa bila amri ya wakubwa? Na kama huyu judge ameamua kufanya hivyo...ni ****! Angetakiwa ajitoe muhanga for real change!
"you tried to fool all of us,but fooling someone who can fool you is what we call FOOLISH!!!
 
mkuu kama kweli jaji aliitwa na kupewa order na wakuu wa wizara ya mambo ya ndani, ina maana sasa tuamini kuwa mahakama haiko huru. Ni branch ya executive na inapokea orders za kubananga sheria kwa interest za executive. Kama tumefikia hali hiyo basi mahakama haina maana tena ni afadhari tubaki na executive ifanye kila kitu.

kabisa mkuu maana ya mahakama kuwepo inatoweka
 
Back
Top Bottom