Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Kesi ya Abdallah Zombe: Mashitaka, hatia, hukumu na yanayojiri

Kama ndivyoulivyosikia its ok. Ni vema hata udhihirishe kuwa hicho ndicho ulichosikia...justify what you heard sir!
 
Hapa Tanzania kuna tatizo kubwa sana, Na kama tutaendelea kuendekeza ujinga wa jinsi hii hatutafika popote..

Kwa kitendo hiki tu inaonyesha ni jinsi gani Tanzania tulivyo kosa sheria za haki za uhuru wa vyombo vya habari.

Kama ile sheria ya haki za binadamu ambayo Jaji ameshindwa kuitumia mbele yake.
 
Kwa nilivyokusoma barubaru inaonekana kuna udhaifu mkubwa kwenye ufunguzi wa kesi yaani ofisi ya DPP imechemka.

je kuna uwezekano wa kushinda kama Serikali itakata rufaa?

naomba jibu lako.
 
Sidhani kama kweli ila kama kweli sababu si hizo tu zipo nyingi katika mwenendo mzima wa utekelezaji kazi na majukumu ndani jeshi na serikali....pia naona ingeua ari ya polisi na hali duni,vitedea kazi duni etc....najua wameiukia kuogopa sabotage........
 
Sidhani kama kweli ila kama kweli sababu si hizo tu zipo nyingi katika mwenendo mzima wa utekelezaji kazi na majukumu ndani jeshi na serikali....pia naona ingeua ari ya polisi na hali duni,vitedea kazi duni etc....najua wameiukia kuogopa sabotage........
This is propaganda , and wa TZ kwa propaganda na wapa jiti, ndo fani aliyotuachia baba wa taifa, fani nyingine tunasuasua labda .......
 
Waswahili tunasema ndio imetoka hiyo ,hakuna serikali wala babu yake serikali wote lao moja,mshtakiwa ni ccm alitumika kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa ,majaji ndio hao mawakili ndio hao ,sasa kwa akili zenu atafungwa mtu hapi ? Mechi hii ndio hivyo ishatiwa kapuni ,tunababaishwa siku mbili tatu ikitoka rufaa itakuwa uchaguzi tayari wananchi wameshaipa kura serikali kwa kukata rufaa. 😀 Tusubiri mechi ya mafisadi tuone kama matokeo yatakuwa sare na haya.
 
Tungoje NEC na CC ndiyo wanaweza kuamua vyema lakini ma jaji wa JK wote hawana maamuzi
 
Mie naamini issue si majaji bali ni wanasheria. Ukifuatilia mtiririko wa kesi unaona kabisa wanasheria wetu hawakuwa makini. Na ndio hao wanaosaini mikataba inayotuumiza mpaka leo.
 
Mie nafikiri Wizara ya sheria inatakiwa kusafishwa maana kuna negligence kibao. Kama huna strong evidence sioni sababu ya kuweka watu rumande kwa muda mrefu au kupeleka kesi mahakamani. Somebody needs to do the job here. Wee subiri utasikia Mramba, Yona na Mgonja wameshinda kesi. Tuko hapa, watch............
 
Ni sehemu ya udaku hakuna la maana hapa kama ndo hivyo si hata huko kwa rumande wasingenda.
 
Kwa uchache wa maoni yangu ni kuwa kuachiwa huru hasa Zombe, kisheria ni kwamba Zombe alipandikiziwa kesi. Sasa kama polisi ambaye ni RPC mzima anaweza kupandikiziwa kesi, je "those who earns a dollar per day" si ndio waliojaa magerezani?

Anyway, nadhani kesi ya Zombe na wenzake imeisha. Tuangalie mbele.
 
Jamani labda huyu Zombe ana tatizo la kisaikolojia, asaidiwe!!! Isije kuwa damu ya wale marehemu inamsumbua, anahitaji maombezi !!!

Zombe ana kazi kubwa sana ya kuishi na jamii,kimtizamo inaonekana ni mtu mkorofi sana na mwenye roho mbaya kupindukia.Kwa wale watu wa Tanga wana jua na maanisha nini.

hana lolote Zombe, bangi tu.
 
Back
Top Bottom