Kesi ya ardhi kama hii sheria inasemaje? Mtu kununua kiwanja na kupata hati, ila akafungwa jela na Watu wakavamia kiwanja chake

Hakuna hii hebu weka kifungu cha sheria? Hii ni kwenye marejeo tuu. I.e precedent

Kwani tuna bishana?utakataaje wakati hujui,acha wanasheria waje watakutajia hicho kifungu,!!ila fahamu hilo kuwa kuna kifungu cha sheria hicho,kuna watu wengi yameshawakuta.
 
Habari wadau

Nina imani humu kuna wataalamu wa sheria za ardhi. Na pia wapo watu wenye uzoefu na mgogoro wa ardhi kama huu wa baba yangu mdogo.

Mwaka 1988 baba yangu mdogo alinunua kiwanja maeneo ya yombo vituka kutoka manispaa ya temeke.

Alilipia malipo yote yaliyohitajika. Na kupewa hati ya kiwanja chake (certificate of occupancy)

Wakati anajipanga kuanza ujenzi mnamo mwaka 1990 akaamua kwenda kwenye kiwanja chake akawa amepanda miti ya miembe.

Akaendelea kulipia kodi za serikali za ardhi.

Mwaka 1994 baba mdogo alipata na kesi ya mauaji... alipigana na mtu kazini kwake bahati mbaya huyo mtu alifariki.

Kesi ikapelekwa mahakamani ikasikilizwa mwishoni kabisa baba mdogo akahukumiwa kufungwa miaka 30. Hivyo akapelekwa gerezani kutumikia hukumu yake.

Mwaka jana december baba mdogo akafanikiwa kutolewa jela. Na kurudi uraiani.

Baada ya kurudi uraiani. Akatuambia ndugu tumsaidie kujenga kwenye kiwanja chake hata chumba kimoja ili apate pa kuishi amalizie maisha yake. Wazo likapita.

Akaenda kwenye kiwanja chake ili aandae mazingira ya ujenzi. Shida kubwa alipofika kwenye kiwanja chake kakuta kuna familia inaishi.

Imejenga chumba na sebule. Na inadai hapo ni kwao wamerithi kutoka kwa baba yao. Ambaye ameshafariki toka mwaka 2013.

Wakamuitia Mjumbe na viongozi wa kata kudai baba mdogo anataka awazulumu kiwanja chao.

Baba mdogo akaeleza stori nzima ilivyokuwa na akatoa na documents za kiwanja chake alizopewa na manispaa ya temeke miaka ya 90. Akatoa hati ya kiwanja certificate of occupancy. Na document ingine aliyopewa wakati ana register imeandikwa certificate of title. Watu kuzicheki zile documents kweli ni halali.

Ile familia iliyokuwa inaishi yenyewe haina document yeyote ya kiwanja zaidi ya muhtasari wa kikao cha familia wakati wa mirathi.

Wanadai hapo ni kwao ila hawajui marehemu baba yao hati zake aliweka wapi. Hivyo hawana hati.

Mjumbe na watu wa kata wamemshauri baba mdogo aende mahakamani.

Maana wao hawamjui. Ila hiyo familia wanaijuia kwa miaka mingi inaishi hapo na hata majirani wote wanatambua kama ndio wamiliki wa hapo.

Na wakasema sheria inammilikisha kiwanja mtu mwingine. Kama ikitokea mmiliki hujakiendeleza kiwanja chako kwa miaka mingi.

Hivyo baba mdogo hana haki maana yeye ndie aliefanya ujinga wa kutoendeleza kiwanja chake mapema. Ama kuwaambia ndugu zake wakiendeleze kwa niaba yake wakati yupo jela

Naombeni msaada wa ushauri wataalamu wa ardhi. Je, mahakamani baba mdogo atatoboa kweli?
Nadhani baba mdogo wako bado ana haki maana wamethibitisha hati ni yenyewe na kwa sheria ya Tanzania umiliki wa hati unakoma pale hati inapokuwa revoked (kufutwa) na mwenye nguvu ya kufuta ni Rais tu kwa hiyo kwa mtazamo wangu bado ni mmiliki halali, na hao wanaoishi hawakuwa na doc yoyote kwa hiyo walikuwa ni wavamizi tu maana hiyo sio ardhi ya kijiji kwamba kijiji kinahamisha umiliki wa ardhi kiholela
 
asikudanganye mtu ardhi ni historia, atueleze kila mmoja alipataje pataje hiyo ardhi, hiyo ya kusema miaka kumi na mbili inatumika kwenu msiojua sheria
 
Miaka 100 ya kiwanja chake kumulikiwsha mwingine endapo hakijaendelezwa bado haijatimia, haki ipo kwake...
 
Habari wadau

Nina imani humu kuna wataalamu wa sheria za ardhi. Na pia wapo watu wenye uzoefu na mgogoro wa ardhi kama huu wa baba yangu mdogo.

Mwaka 1988 baba yangu mdogo alinunua kiwanja maeneo ya yombo vituka kutoka manispaa ya temeke.

Alilipia malipo yote yaliyohitajika. Na kupewa hati ya kiwanja chake (certificate of occupancy)

Wakati anajipanga kuanza ujenzi mnamo mwaka 1990 akaamua kwenda kwenye kiwanja chake akawa amepanda miti ya miembe.

Akaendelea kulipia kodi za serikali za ardhi.

Mwaka 1994 baba mdogo alipata na kesi ya mauaji... alipigana na mtu kazini kwake bahati mbaya huyo mtu alifariki.

Kesi ikapelekwa mahakamani ikasikilizwa mwishoni kabisa baba mdogo akahukumiwa kufungwa miaka 30. Hivyo akapelekwa gerezani kutumikia hukumu yake.

Mwaka jana december baba mdogo akafanikiwa kutolewa jela. Na kurudi uraiani.

Baada ya kurudi uraiani. Akatuambia ndugu tumsaidie kujenga kwenye kiwanja chake hata chumba kimoja ili apate pa kuishi amalizie maisha yake. Wazo likapita.

Akaenda kwenye kiwanja chake ili aandae mazingira ya ujenzi. Shida kubwa alipofika kwenye kiwanja chake kakuta kuna familia inaishi.

Imejenga chumba na sebule. Na inadai hapo ni kwao wamerithi kutoka kwa baba yao. Ambaye ameshafariki toka mwaka 2013.

Wakamuitia Mjumbe na viongozi wa kata kudai baba mdogo anataka awazulumu kiwanja chao.

Baba mdogo akaeleza stori nzima ilivyokuwa na akatoa na documents za kiwanja chake alizopewa na manispaa ya temeke miaka ya 90. Akatoa hati ya kiwanja certificate of occupancy. Na document ingine aliyopewa wakati ana register imeandikwa certificate of title. Watu kuzicheki zile documents kweli ni halali.

Ile familia iliyokuwa inaishi yenyewe haina document yeyote ya kiwanja zaidi ya muhtasari wa kikao cha familia wakati wa mirathi.

Wanadai hapo ni kwao ila hawajui marehemu baba yao hati zake aliweka wapi. Hivyo hawana hati.

Mjumbe na watu wa kata wamemshauri baba mdogo aende mahakamani.

Maana wao hawamjui. Ila hiyo familia wanaijuia kwa miaka mingi inaishi hapo na hata majirani wote wanatambua kama ndio wamiliki wa hapo.

Na wakasema sheria inammilikisha kiwanja mtu mwingine. Kama ikitokea mmiliki hujakiendeleza kiwanja chako kwa miaka mingi.

Hivyo baba mdogo hana haki maana yeye ndie aliefanya ujinga wa kutoendeleza kiwanja chake mapema. Ama kuwaambia ndugu zake wakiendeleze kwa niaba yake wakati yupo jela

Naombeni msaada wa ushauri wataalamu wa ardhi. Je, mahakamani baba mdogo atatoboa kweli?
Ndugu Freshman,
1.Je, suala hili ni habari ya ukweli au ni hadithi ya kutunga tu??
2. Endapo kama hii ni habari ya ukweli, je, huyo baba yako bado anayo dhamira thabiti kabisa ya kuhitaji hiyo ardhi yake?? Je, yuko seriously kabisa kuhusu hilo?
Naomba unithibitishie Kwanza kuhusu haya masuala haya mawili kwanza.
Aidha,
3. Je, nyaraka zake zote za umiliki wa ardhi/kiwanja hicho bado anazo?
Kama uko serious kabisa na Jambo hili na endapo kama kweli yote uliyoandika hapa ni ya kweli, naomba u-scan hizo documents zake zote kisha unitumie kwenye DM yangu ili niweze kumsaidia kwa kile ambacho nitaweza kumsaidia(ushauri wa bure bila gharama yoyote), ili aweze kuanzisha mchakato mzito wa kuirejesha hiyo haki yake aliyoipoteza.
Aidha, natanguliza ushauri wa awali kwake kwamba ASIKURUPUKE HATA KIDOGO kuanzisha kesi Mahakamani kuhusu jambo hili kabla hajapata kwanza ushauri wa kina na wa kutosha kabisa, na ushauri ulio sahihi kuhusu mgogoro wa aina hii, anaweza kukwama moja kwa moja mbele ya safari endapo kama hajatulia na hajajiandaa vizuri kwenye suala hili katika hatua hii ya mwanzo, tafdhali mfikishie ujumbe huu. Atulie, asikurupuke.
Vile vile, kama itawezekana nitumie na nakala ya hukumu ya Kesi ya Jinai aliyohukumiwa nayo huko miaka ya nyuma (1994), kama hawezi kuipata hiyo hukumu basi nitumie Namba ya Kesi hiyo(afuatilie Mahakamani alikohukumiwa au Gereza la mwisho kutumikia kama haikumbuki namba ya kesi), ni muhimu sana kuzingatia Jambo hili kwa sababu kesi ya ardhi atakayotakiwa kuianzisha ina vikwazo vingi sana vya yeye kushinda endapo kama hajajiandaa vizuri.
Nitumie pia na namba zake za simu, ili kurahisisha mawasiliano na kupata ufafanuzi zaidi kutoka kwake pale itakapohitaji kufanya hivyo.
Asante, nasubiri feedback kutoka kwako.
 
Napenda watu wanaosaidia wenzao.Allah akubariki na akuongoze katika Kila hatua ya hiyo kesi.
 
Back
Top Bottom