Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Kesi ya Babu Seya na wanae - Ukweli ni upi haswa?

Dawa ni moja tu, iwapo akitaka kubaki salama sharti aje madhabahuni kwa ajili ya TOBA. Hakuna dhambi isiosameheka!!! Mungu huwa anasamehe dhambi/uovu wa wanadamu. Akishatubu kwa Mungu aanze kumtumikia Mungu katika maisha yake yote.!

Tofauti na hivyo, ataomba kurudishwa kule gerezani alikokuwa.

JESUS IS LORD !

Mkuu unawapangia tena ratiba zao na Mungu. Wanadamu wana njia zao za kuongea na Mungu wao katika kuomba kusamehewa.

I stand to be corrected
 
Sasa mbna hymen and anus evidence ina claim was intact
Umeona ee! Uchunguzi wa kitabibu ulionesha sehemu ya mbele madogo walikuwa bado na bikra zao na nyuma palikuwa hapajabuguziwa.

Walifungwa watuhumiwa wote 4 kwa kosa hilo hilo alafu baada ya miaka michache wale wadogo 2 wakaachiwa huru hapo wengi ndio tulishtuka na kuona hiyo kesi ni fake.

Mwisho wa siku watu wanaotafuta umaarufu wa kisiasa wameitumia fulsa na imependeza zaidi. Dr Shika kwisha habari yake.
 
Kwani kesi iliendeshwa kwa kiingereza na hao watoto walitoa ushahidi kwa lugha hiyo hiyo?
 
Je kwanini hawakuweka sample ili wafanye DNA badala ya kusikiliza tu ushahidi usio na exhibit.
 
yule mzee seya nimemuangalia ni kama ana hofu flani hivi.nadhani yeye alifanya huo ufirauni kweli.papii ni innocent nadhani
 
BIN ADAM SIJUWI ROHO MBAYA ZITAWAPELEKA WAPI
YAAANI MNAPENDEZWA NA MWENZENU ANAPOPATWA NA TATIZO
BIN ADAM KUWENI NA HURUMA KWA WENZENU
 
Kesi za namna hii huwa znatokea na watu hutumikia vifungo vyao bila tabu...lkn mbn kwa kesi ya hawa watu imekuwa na ukakasi saaana, ww huwezi kujiuliza kulikoni!?
kama ungekuwa ulishawahi kufanya kazi mahakamani, na kidogo ukawa karibu na magerezani etc utakuja kuelewa kuwa kati ya watu 100 wanaosemekana wamebambikwa kesi, na specifically kwa kesi kama hii iliyoanzia subordinate, ikaenda high court, ikaenda court of appeal, na ikarudi tena court of appeal for review na kote watu wenye akili zao wakasema Nooooo, utaelewa kuwa sio rahisi kubambikwa kesi kihivyo.

watu wengi ambao huwa wanabambikwa kesi huwa ni kule Primary court, huko ndio wengi sana na wachache subordinate courts (district &RM), lakini kwa High court na kuendelea ni nadra. na huko subordinate ukibambikwa huwa hazikatishi high court, lazima high court ipige chini tu. ila ukiona case imeenda hadi review court of appeal, hakika ni ngumu kusema mtu alibambikwa. ukienda gerezeni kwa watu ambao kesi zao zilianzia High court au wale ambao zimepita hadi court of appeal, hautakuja kukuta hata mtu mmoja anayesema alibambikwa...wengi huwa wanakuwa wamefanya na wanakiri hivyo wakiwa kule ndani gerezani lakini wakiwa mahakamani wanaruka hatua mia nane. wenzio tunaijua mahakama na tunaijua magereza na wafungwa kiundani sana ninaongea kwa experience ya kutosha.
 
Utawala wa awamu hii unafanya kazi zaidi kwa kutumia idara ya Usalama wa Taifa, na inaashiria taarifa walizompa(ukiachilia proceedings za kimahakama ambazo huwa zina ukakasi sana no wonder tuna wafungwa wengi ambao walishitakiwa pamoja[jointly accused] lakini hawajuani na walionana kwa mara ya kwanza baada ya kuwa kwenye kesi moja) ni kuwa jamaa kesi yao haikuwa na ukweli.Siamini kama mzazi mtu anaweza kuwaachia watu wenye kesi kama yao.Hiyo njia ni ya mkato sana japo hata hiyo hao jamaa wanaweza wakalishwa matango pori wakampoteza kiranja wao.Kesi inatia mashaka sana kwakuwa walikamata familia nzima na Papii hajatajwa kwenye huo ushaidi,ilikuwaje akapatikana na hatia?
 
Mimi nilimjibu Yule aliyesema watarudishwa tena na DPP ndo nikasome kazi ya DPP ilishaisha .Hili swala hali wezi kurudi tena kwenye litigation kwa sababu ya kanuni ya res judicata.
hahaha, ndio raha ya kuwa na first year kwenye hii mijadala. ndugu, ukienda kwenye mtihani wako huko chuo, elewa kuwa res judicata upo tu kwenye civil, kwenye criminal haipo. kesi ya babu seya ni criminal....hapo ulitakiwa uwe umefundishwa na mwalimu wako kitu inaitwa "Autrefois convict" jaribu kuperuzi hayo madesa yenu utaelewa maana yake. nenda section 280(1) CPA utakuta kitu kinaitwa Plea of autrefois acquit and autrefois convict. piga shule dogo.
 
2010 mmoja wa vibinti hivyo nilimuona Mt. Vernon,NY nikiambiwa baadae kuwa alifika huko baada ya kuwa sehemu ya mashahidi na kutenda vyema!!!
2+2=4 inamaana gani Unapo statement ya alifika huko baada yaku toa ushahidi ¡! HATARI!!!!
 
Utawala wa awamu hii unafanya kazi zaidi kwa kutumia idara ya Usalama wa Taifa, na inaashiria taarifa walizompa(ukiachilia proceedings za kimahakama ambazo huwa zina ukakasi sana no wonder tuna wafungwa wengi ambao walishitakiwa pamoja[jointly accused] lakini hawajuani na walionana kwa mara ya kwanza baada ya kuwa kwenye kesi moja) ni kuwa jamaa kesi yao haikuwa na ukweli.Siamini kama mzazi mtu anaweza kuwaachia watu wenye kesi kama yao.Hiyo njia ni ya mkato sana japo hata hiyo hao jamaa wanaweza wakalishwa matango pori wakampoteza kiranja wao.Kesi inatia mashaka sana kwakuwa walikamata familia nzima na Papii hajatajwa kwenye huo ushaidi,ilikuwaje akapatikana na hatia?
usalama wa taifa ndio bashite au?
 
Hivi Inamaana hawa akina Babu Seya hawakuwa na Mawakili wa kuwatetea hadi Wakatiwa hatiani kwa Ushahidi wa Kubumba?
Marando ndie alikuwa.wakili wao, ndio maana nikasema labda atakuja kusimulia alichokigundua katika kesi hii.
 
Back
Top Bottom