Binafsi toka mwanzo wa kuifahamu kesi hii iliyojaa kila aina ya mbwembwe na umaarufu kwa sababu ya washtakiwa wenyewe siku zote na kwa mtazamo wangu na upande wa pili unisamehe ila imani yangu ni kwamba pale hakuna kesi zaidi ya siasa chafu na visasi vya kila aina,chuki na ubinafsi wa nafsi ndio vilivyofanya paka leo hii familia ya Nguza Viking ikiteseka bila sababu.Yashasemwa mengi sana kuwa kuna mlono wa mtu pale na hata ukiangalia mwenendo mzima wa kesi utakubaliana nami pasipo shaka kuwa pale kuna ujanja unaofanyika ingawa ni ngumu na siwezi kutibitisha moja kwa moja ila rai yangu na maombi yangu juu yao waweze kuwa huru tena na kama walifanya kweli basi uhuru wao hakika hautadumu huku uraiani...Mtazamo wangu binafsi.