Mahakama Kuu Kanda ya Manyara imekubaliana na maombi ya Chadema ya kuendelea na kesi ya msingi, huku ikitupilia mbali mapingamizi yaliyowekwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa dhidi ya chama hicho kuendelea na kesi hiyo.
Kesi hiyo iliyosikilizwa leo Oktoba 2, 2025 na Jaji Nenelwa Mwihumbi, ilifunguliwa na CHADEMA kupinga maamuzi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya kutowatambua viongozi wa walioteuliwa na Baraza Kuu Januari 22, 2025.
Itakumbukwa Agosti 28, 2025 Mahakama hiyo ilifuta amri ya Msajili wa Vyama Vya Siasa ya kuzuia Ruzuku ya Chadema na kutowatambua Katibu Mkuu, Manaibu wake na Wajumbe Watano wa Kamati Kuu waliothibitishwa na Baraza Kuu Januari 22, 2025 baada ya Uchaguzi Mkuu wa ndani ya Chama.
Uamuzi huo wa Msajili ulifutwa mpaka kesi ya msingi itakaposikilizwa na ndio imeanza kusikilizwa leo.
Kesi hiyo inaendeshwa na Jaji Nenelwa Mwihambi ambaye aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Sheria wa Bunge la Tanzania baadaye akateuliwa kuwa Katibu wa Bunge kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Uamuzi wa leo Oktoba 2
Akizungumza na vyombo vya habari nje ya mahakama hiyo baada ya kusikilizwa kwa maombi ya pande mbili, Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika ameeleza...
Uamuzi wa awali
Katika uamuzi uliotolewa na Jaji Devotha Kamuzora Agosti 28, 2025, kwanza alitoa ruhusa kwa CHADEMA ya kufungua kesi ya mapitio ya Kimahakama ndani ya siku 14 dhidi ya uamuzi wa Msajili Wa Vyama Vya Siasa wa kutotambua uteuzi uliofanywa na Baraza Kuu tarehe 22 Januari 2025 na kuacha kutoa ruzuku.
Pili, Jaji alitoa zuio la muda dhidi ya utekelezaji wa uamuzi wa Msajili wa barua yake ya tarehe 27 Mei 2025 wa kutotambua uteuzi wa Katibu Mkuu, Manaibu wake na wajumbe wa Kamati Kuu waliothibitishwa na Baraza Kuu tarehe 22 Januari 2025 na kuacha kutoa kupeleka ruzuku kwa Chadema mpaka yatakapofanyika maamuzi ya mwisho juu ya maombi yaliyokusudiwa kuwasilishwa na Chadema.
Baada ya hukumu hiyo hapo juu Chadema iliwasilisha ndani ya siku 14 maombi yake kamili ya kwa Mahakama kufanya mapitio na kubatilisha kwa kudumu/ukamilifu maamuzi ya Msajili.
Serikali kwa upande wake imefanya mambo matatu kwa niaba ya Msajili: Mosi, umewasilisha notisi ya kukata rufaa Mahakama ya rufaa dhidi ya uamuzi wa Jaji wa tarehe 28 Agosti 2025, Pili, majibu na viapo kinzani dhidi ya maombi yetu tuliyowasilisha mahakamani. Tatu, pingamizi dhidi ya maombi yetu.
Leo tarehe 2 Oktoba ndio usikilizaji ulipaswa kuendelea. Pande mbili zimewasilisha. Jaji mpya Nenelwa Mwihambi ameahirisha kesi saa 4 amesema atatoa uamuzi wake saa 8 mchana.
Katibu Mkuu wa chama,John Mnyika akiwa Mahakama Kuu masijala ya Manyara kuhudhuria kesi iliyofunguliwa na chama dhidi ya Msajili wa vyama vya Siasa kupinga.