VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,137
- 17,908
Si jambo la kulikalia kimya. Lazima niseme ukweli juu ya jambo hili. Ukweli wa heri na si wa shari. Ingawa ni jambo linaloruhusiwa kikatiba na kisheria kuwepo kwa uwezekano wa mtu binafsi kumshtaki mwingine kijinai, masuala yote ya kijinai yapo chini ya Ofisi ya Mashtaka ya Taifa iliyo chini ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini almaarufu kama DPP. DPP hufanya kazi zake kwa ukaribu na jeshi la polisi hususani Idara ya Upelelezi ya Polisi inayoongozwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai aka DCI.
Ndiyo kusema, mwenye mamlaka ya kushtaki kijinai kikawaida ni DPP. Yeye huchunguza na kuendesha kesi mahakamani kupitia Mawakili walio chini yake. Na kwakuwa msingi mkubwa wa kesi za jinai ni uwepo wa ushahidi usioacha shaka, DPP hulazimika kukusanya ushahidi na kuuwasilisha mahakamani dhidi ya yule anayemshtaki. Upatikanaji wa ushahidi huweza kuanzia hata kwa watu wa kawaida sana mtaani. Watu husema ukweli ingawa huwa si ukweli 'rasmi'.
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewasilishiwa maombi ya kushtakiwa kijinai kibinafsi na aliyekuwa Mbunge wa Ubungo na mwanahabari Saed Kubenea. Maombi ya Kubenea ya kutaka kumshtaki kijinai Makonda yapo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na yatatajwa kesho. Kubenea ameomba kuruhusiwa, kupitia Mawakili wake, kumshtaki Makonda kijinai. Inadhaniwa kuwa Kubenea anao ushahidi wa jinai husika.
Sasa, DPP na Serikali kwa ujumla kweli hazina ushahidi wa jinai alizozitenda Makonda wakati akiwa mkuu wa wilaya na mkoa hadi ajitokeze Kubenea? Kubenea amepataje ushahidi wa kijinai dhidi ya Makonda ulioishinda Ofisi ya DPP na Serikali kwa ujumla? Hima DPP ichukue kesi dhidi ya Makonda kutoka kwa Kubenea (kwakuwa inaruhusiwa kisheria) ili kuondoa fedhea hii kwa Serikali ya Mama Samia. Muda ni huu!
Wasiojulikana sasa wamejulikana?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Kilosa, Morogoro)