Kesi ya kupinga uwekezaji wa DP; Mahakama sasa ithibitishe yale maneno ya Rostam yalikuwa ya ukweli au uongo!

Kesi ya kupinga uwekezaji wa DP; Mahakama sasa ithibitishe yale maneno ya Rostam yalikuwa ya ukweli au uongo!

Maelekezo tayali yameanza na ndio maana uamuzi wa kesi umesogezwa mbele kupisha siku ya wakulima ambayo mama mwenye nyumba yupo kule, na huku bunge wameitisha maoni ya kubadili Sheria kwa sababu wanajua watashinda kesi kwa vyovyote iwavyo
 
RA meant what he said !! That's the fact !!!
 
Kwahiyo mleta mada unataka Mahakama itoe hukumu ambayo itakufurahisha wewe? wakitoa hukumu kinyume na matarajio yako ndio utaona kua hawapo sawa?


Nijuavyo mimi,Mahakamani kabla ya kusomwa hukumu,husomwa maelezo ya mwenendo wa kesi na vifungu vya sheria vilivyosababisha hukumu hiyo kutolewa.
 
Kwahiyo mleta mada unataka Mahakama itoe hukumu ambayo itakufurahisha wewe? wakitoa hukumu kinyume na matarajio yako ndio utaona kua hawapo sawa?


Nijuavyo mimi,Mahakamani kabla ya kusomwa hukumu,husomwa maelezo ya mwenendo wa kesi na vifungu vya sheria vilivyosababisha hukumu hiyo kutolewa.
Hayo ni maoni yako! Mada mezani iko wazi kwamba mahakama ithibitishe kwamba wako imara kutafsiri sheria
 
Ndugu Rostam Aziz ALIKOSEA...

Na kwa sababu ALIKOSEA na kutambua KOSA lake ,haraka akaomba RADHI....

Kama ilivyo MIHIMILI yote....ndani yake kuna binadamu....yako makosa ya baadhi yao lakini kamwe haifanyi MIHIMILI hiyo kustahili kushambuliwa kwani ni MISHIPA YA DAMU ya taifa.....

Watanzania tunakimbilia mahakamani kutafuta HAKI ZETU na huwa tunazipata....

Mahakamani ni sehemu ya MWISHO ya kutafsiri sheria zetu....hapawezi kuwa sehemu inayostahili kurushiwa mawe hovyo......

#Mwenyezi Mungu Aendelee Kulilinda Dola La Tanzania na Mihimili yake
Umeandika kwa uchungu sana kuhusu mustakabari wa haki katika nchi husika.
Wewe unaonekana ni Mzalendo halisi.
Ila ikiiangalia tone ya sauti na body language ya muweka hazina wetu kabla na baada ya kukiri kosa kuna kitu utakigundua.
Wanasema situation talks aloud
 
Maagizo kutoka juu kwenye mambo ya serikali lazima...
 
Wewe kama nani wa kuiamuru mahakama?

Hivi nyie mnamfaham Rostam au mnamsikia na kumuona tu kwenye vyombo vya habari?

Nikudokeze kidogo?mFikiri kabla hujajibu. Usilolijuwa ni usiku wa kiza.
Zomba Zomba Zomba!

Jifunze kusoma mstari kwa mstari na kumuelewa mwandishi usikurupuke.
Pia usiendeshwe na mihemuko na hisia kama kijana akiwa ame balehe au kuvunja ungo. Huyo mume wenu na bwana wenu Rostam yeye ni kama punje ya mchanga katika Taifa hili. Amini usiamini siku inakuja na wakati umekaribia.

Nakukumbusha tu soma alama za nyakati, hao miungu watu mnaowategemea anguko lao limekaribia.
 
[emoji120][emoji120]

Ndugu yangu sina taifa jengine isipokuwa nyumbani kwetu Tanzania...

Ndugu yangu sioni taifa jengine bora duniani isipokuwa taifa langu Tanzania.....

Sioni PEMA pa kukimbilia isipokuwa nyumbani hapa....

Taifa letu ni la mfano na la kipekee....hatufanani na wengi watuzungukao.....

Mapungufu ya baadhi yetu watanzania ni ya kibinadamu na tuna haki na ulazima wa kuyarekebisha kuwa bora lakini sababu hizo si za kufanya TULICHUKIE TAIFA LETU ,TUCHUKIANE NA KUSAHAU MAZURI YAKE NA YA WATU WAKE [emoji120]
Asante sana kwa uzalendo. Nyie ndio hazina iliyobaki.

Nakuambia Tanzania bado ni nchi ambayo raia wake wanapendana na kuheshimiana sana. Na pia wanaheshimu sana viongozi wao.

Tatizo ni moja tu.
Baadhi ya viongozi wanajiona kama Malaika vile, kwamba hawakosei.

Wananchi wanataka kusikilizwa maoni yao na kufanyiwa kazi au kujibiwa kwa kutoka moyoni.

Kama Kiongozi anakosea ni vema akili kuwa amekosea na atarekebisha hayo makosa, kwa maslahi mapana ya nchi na wananchi wake.

Nchi zenye amani kama Sudani zilikuwa ya amani sana. Ni viongozi hawa hawa wasio sikiliza wananchi ndio wameiingiza kwenye machafuko.

Basi ni vema sana ukitumia Hekima zako kuwashauri waendesha nchi kuwa wameaminiwa kuwawakilisha mamilioni ya watu.

Wawe wenye usikivu kwao na sio kuwasikiliza watu wa nje ambao wengi wao sio wazalendo.

Asante sana kwa mchango wako mzuri sana kwa Taifa letu.
 
Zomba Zomba Zomba!

Jifunze kusoma mstari kwa mstari na kumuelewa mwandishi usikurupuke.
Pia usiendeshwe na mihemuko na hisia kama kijana akiwa ame balehe au kuvunja ungo. Huyo mume wenu na bwana wenu Rostam yeye ni kama punje ya mchanga katika Taifa hili. Amini usiamini siku inakuja na wakati umekaribia.

Nakukumbusha tu soma alama za nyakati, hao miungu watu mnaowategemea anguko lao limekaribia.
Siku mbona zipo siku zote, hazijaanza leo na hazotaisha leo, zitaendelea kuja na kuondoka, wewe na mimi tutaondoka tutaziacha.

Huna ujanja kwa Rostam, kumbuka hilo.

Wakati wewe unabishana khusu gati mbili tatu za bandari, yee anauza ges Tanzania, Kenya na Zambia.
 
Kuandika tu hujui.."tayali"....

Utajua kufikiri vyema ?!![emoji15][emoji1787][emoji1787]

Kusogezwa mbele kesi kunaingiliaje maamuzi ya kesi ?!!!

Je ASILAUMIWE aliyepanga kusikilizwa hiyo kesi kipindi cha sherehe za 8/8 bali ilaumiwe KALENDA ya matukio ya kitaifa ambayo ilianza JANUARI MOSI ?!!!
Acha kukurupuka kama umepaliwa na gongo, kama hujaelewa pita kimya kimya kama unaaga maiti
 
ukisikia paukwa pakawa ujuwe ndo imeisha hivyo
 
Back
Top Bottom