Kesi ya kupinga uwekezaji wa DP; Mahakama sasa ithibitishe yale maneno ya Rostam yalikuwa ya ukweli au uongo!

Maelekezo tayali yameanza na ndio maana uamuzi wa kesi umesogezwa mbele kupisha siku ya wakulima ambayo mama mwenye nyumba yupo kule, na huku bunge wameitisha maoni ya kubadili Sheria kwa sababu wanajua watashinda kesi kwa vyovyote iwavyo
 
RA meant what he said !! That's the fact !!!
 
Kwahiyo mleta mada unataka Mahakama itoe hukumu ambayo itakufurahisha wewe? wakitoa hukumu kinyume na matarajio yako ndio utaona kua hawapo sawa?


Nijuavyo mimi,Mahakamani kabla ya kusomwa hukumu,husomwa maelezo ya mwenendo wa kesi na vifungu vya sheria vilivyosababisha hukumu hiyo kutolewa.
 
Hayo ni maoni yako! Mada mezani iko wazi kwamba mahakama ithibitishe kwamba wako imara kutafsiri sheria
 
Umeandika kwa uchungu sana kuhusu mustakabari wa haki katika nchi husika.
Wewe unaonekana ni Mzalendo halisi.
Ila ikiiangalia tone ya sauti na body language ya muweka hazina wetu kabla na baada ya kukiri kosa kuna kitu utakigundua.
Wanasema situation talks aloud
 
Maagizo kutoka juu kwenye mambo ya serikali lazima...
 
Wewe kama nani wa kuiamuru mahakama?

Hivi nyie mnamfaham Rostam au mnamsikia na kumuona tu kwenye vyombo vya habari?

Nikudokeze kidogo?mFikiri kabla hujajibu. Usilolijuwa ni usiku wa kiza.
Zomba Zomba Zomba!

Jifunze kusoma mstari kwa mstari na kumuelewa mwandishi usikurupuke.
Pia usiendeshwe na mihemuko na hisia kama kijana akiwa ame balehe au kuvunja ungo. Huyo mume wenu na bwana wenu Rostam yeye ni kama punje ya mchanga katika Taifa hili. Amini usiamini siku inakuja na wakati umekaribia.

Nakukumbusha tu soma alama za nyakati, hao miungu watu mnaowategemea anguko lao limekaribia.
 
Asante sana kwa uzalendo. Nyie ndio hazina iliyobaki.

Nakuambia Tanzania bado ni nchi ambayo raia wake wanapendana na kuheshimiana sana. Na pia wanaheshimu sana viongozi wao.

Tatizo ni moja tu.
Baadhi ya viongozi wanajiona kama Malaika vile, kwamba hawakosei.

Wananchi wanataka kusikilizwa maoni yao na kufanyiwa kazi au kujibiwa kwa kutoka moyoni.

Kama Kiongozi anakosea ni vema akili kuwa amekosea na atarekebisha hayo makosa, kwa maslahi mapana ya nchi na wananchi wake.

Nchi zenye amani kama Sudani zilikuwa ya amani sana. Ni viongozi hawa hawa wasio sikiliza wananchi ndio wameiingiza kwenye machafuko.

Basi ni vema sana ukitumia Hekima zako kuwashauri waendesha nchi kuwa wameaminiwa kuwawakilisha mamilioni ya watu.

Wawe wenye usikivu kwao na sio kuwasikiliza watu wa nje ambao wengi wao sio wazalendo.

Asante sana kwa mchango wako mzuri sana kwa Taifa letu.
 
Siku mbona zipo siku zote, hazijaanza leo na hazotaisha leo, zitaendelea kuja na kuondoka, wewe na mimi tutaondoka tutaziacha.

Huna ujanja kwa Rostam, kumbuka hilo.

Wakati wewe unabishana khusu gati mbili tatu za bandari, yee anauza ges Tanzania, Kenya na Zambia.
 
Acha kukurupuka kama umepaliwa na gongo, kama hujaelewa pita kimya kimya kama unaaga maiti
 
ukisikia paukwa pakawa ujuwe ndo imeisha hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…