Kesi ya kutaka Muungano ufutwe yaanza rasmi Znz

Kesi ya kutaka Muungano ufutwe yaanza rasmi Znz

Wadai katika kesi hiyo wakiongozwa na mwanaharakati Rashid Salum Adiy, wanadai kuwa hakuna hati ya makubaliano ya muungano inayodaiwa kusainiwa Aprili 22, mwaka 1964 siku mbili kabla ya siku ya muungano, Aprili 26. Wafunguaji kesi hiyo wanadai kuwa, mambo kadhaa yanayohusu Muungano yalikuwa batili na kwa hiyo wanaitaka Mahakama Kuu ya Zanzibar itamke hivyo iliiruhusu kuzaliwa kwa dola huru ya Zanzibar yenye mamlaka kamili.

Huwezi kusema hakuna hati maana inawezekana iko mahali ni muhimu madai yawe kwamba Hati ya Makubaliano ya Muungano yawekwe wazi kwa Umma maana ni haki yao kuijua na kuitambua .
Pili baada ya uwepo wa hati kuwa wazi sasa madai ya kubatilishwa kwa sababu wanazo ona ni za Haki kwa Sasa kuliko wakati ule iliposainiwa yanaweza kuwekwa mbele ya Mahakama!

Walalamikiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Baraza, Mwanasheria Mkuu wa Muungano na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mtaifa.

Hapo kwenye uwekundu nadhani wafanye haraka mchakato wa kuibadilisha ,sioni mahusiano ya Katibu Mkuu wa UN na Makubalianao ya Muungano na kinyume na hapo kesi inaweza kukosa mashiko.
 
Kama ipo na waitoe, tusiandikie mate wakati wino upo, tupewe huo mkataba wa muungano, tujue ulitiwa saini lini na wa muda gani, mi nasema kwamba hata kama upo hawawezi kuutoa kwa sababu umeshaisha muda wake, muungano ulikuwa wa makubaliano wa miaka kumi tu, sasa ili tuweze kuupata huo mkataba wa muungano cha kwanza ni kuudai lini umetiwa saini hapo ndio tutaweza kuujua kama umekufa au uhai, tumechoka kutapeliwa na watu wachache kwa manufaa yao na familia zao, let us gooo
Huwezi kusema hakuna hati maana inawezekana iko mahali ni muhimu madai yawe kwamba Hati ya Makubaliano ya Muungano yawekwe wazi kwa Umma maana ni haki yao kuijua na kuitambua .
Pili baada ya uwepo wa hati kuwa wazi sasa madai ya kubatilishwa kwa sababu wanazo ona ni za Haki kwa Sasa kuliko wakati ule iliposainiwa yanaweza kuwekwa mbele ya Mahakama!

Hapo kwenye uwekundu nadhani wafanye haraka mchakato wa kuibadilisha ,sioni mahusiano ya Katibu Mkuu wa UN na Makubalianao ya Muungano na kinyume na hapo kesi inaweza kukosa mashiko.
 
Muuungano ukivunjika....
Watanzania bara itabidi tuitwe Watanganyika...

Tanganyika doesn't sound good as Tanzania

Maana ya Tanganyika:
Tanga means Kutanga tanga and Nyika means mwituni
Mtanganyika=> Mtu wa kutangatanga mwituni.....
Sitaki kuitwa Mtanganyika mm, bora Muungano usivunjike, Udumu Muungano Milele Daima
Tanga maanayake si kutanga tanga,hili ni neno la Kia jemi ,maana yake ni greenland.nchi yeye rutumba,kijani kibichi.
 
Mi naomba washinde na maamuzi ya mahakama yaangukie katika Z'bar kuwa dola huru ili Watanganyika tujipange vizuri sasa.
Watanganyika wanaotaka Tanganyika yao wamazidi kuongezeka siku hadi siku.
Tatizo la kesi hii ni kwamba, kesi inasikilizwa katika mahakama ndogo.
Mahakama isiyo na ubavu wa kutengua muungano.
Kwa kweli kesi hii ni sawasawa na kisikiliza Kisutu, hakuna cha maana hapo.
 
bora wa zenji wajitoe tu, maana hao ndio wana malalamiko saana na huu muungano. Mimi raisi wao yaani mgombea mwenza wa raisi wangu ambaye ndio makamu wa raisi wangu hata kura yangu haioni, kwenye kuchagua raisi wangu kura zao zinahesabiwa! kodi zetu wanagaiwa, ardhi zetu wanamiliki..... zenji sijawahi kukanyaga wala karafuu zao zijawahi hata kuzinusa halafu leo hii naitwa mkoloni....watanzania tusikubali, bora uvunjwe tu muungano tena uvunjwe leo hii!
 
Eee Mola wajalie waliofungua kesi hiyo busara na hekima na hakika tunaomba washinde kesi hiyo.
Natamani hukumu ya kuvunja muungano ingetolewa pengine wzn wangepumua.

Pamoja na hayo tunawaomba nao wafanye jitihda
1. Wamuombe makamu wa rais aache kazi hiyo aliyopata kwa uzanzibar wake
2. Wabunge wagome kabisa kuja Dodoma
3. Huko BLW mswada upelekwe harana na inshallah upitishwe na asilimia 100
4. Wzn wanofanya kazi katika serikali ya muungano waondoke na kurudi kuijenga znz yenye neema haraka.

Watanganyika, tuwaombee heri wenzetu haraka sana na tuwasaidie kuharakaisha kazi yao
1. Tuwaondoe katika fursa za muungano ili wajisikie wana umuhimu wa kurudi kwao.
2. Tukate misaada a kibajeti, elimu na mishahara ikiwa ni pamoja na umeme ili kuwaharakisha warudi kwao.
3. Watu waanze kugawana majumba ili wznz wajihisi wapo ugenini na kuondoka haraka, wakija waje kama wageni.

Mungu atajalia inshallah watashinda kesi na kupata znz yenye neema. Tuwaombee na tuwasaidie inapobidi
 
kwanini wakati wa muungano Zanzibar ilipewa hadhi ya nchi mpaka kuitwe muungano wa nchi mbili?labda wangelifanya mkoa haya matatizo yasingetokea zanzibar ina hadhi ya mkoa na siyo nchi.

Huwatendei haki. Viko visiwa vidogo sana kuliko Zanzibar lakini ni nchi kamili.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Watanganyika wanaotaka Tanganyika yao wamazidi kuongezeka siku hadi siku.
Tatizo la kesi hii ni kwamba, kesi inasikilizwa katika mahakama ndogo.
Mahakama isiyo na ubavu wa kutengua muungano.
Kwa kweli kesi hii ni sawasawa na kisikiliza Kisutu, hakuna cha maana hapo.

Sasa wanajisumbua nini kufungua case ambayo wanajua haitakuwa na effect yoyote? Au what they care is just to draw people's attention kuwa wako serious? Wapeleke mahakama kuu ya Tanzania ambapo maamuzi yatakuwa na effect. Mi naona wanajisumbua tu. Hili swala litawezekana pale CCM itakapoangushwa kwenye uchaguzi mkuu tu.
 
Kwanini Tanganyika isijitowe na kusema kuanzia leo Tanganyika ni huru?

Hivi Tanganyika ipo?
ijitoe ya nini?
kelele zenu ndo zmetuchosha makupe nyie,
nyie hamtaki, afu sisi tuwasaidie kujitoa ebo!
Tokeni, mkitaka kutoka, au mnyamaze kabisa.
 
ijitoe ya nini?
kelele zenu ndo zmetuchosha makupe nyie,
nyie hamtaki, afu sisi tuwasaidie kujitoa ebo!
Tokeni, mkitaka kutoka, au mnyamaze kabisa.

Nyie kina nani. Unanchekesha!

Mie ni Mtanganyika na mpaka leo siioni faida ya huu Muungano na nnaitamani Tanganyika yangu aliyoiyeyusha Nyerere. Nauliza Tanganyika yangu iko wapi?
 
Watanganyika wanaotaka Tanganyika yao wamazidi kuongezeka siku hadi siku.
Tatizo la kesi hii ni kwamba, kesi inasikilizwa katika mahakama ndogo.
Mahakama isiyo na ubavu wa kutengua muungano.
Kwa kweli kesi hii ni sawasawa na kisikiliza Kisutu, hakuna cha maana hapo.
Isome vizuri katiba ya muungano inavosema ndio utajua kuwa mahakama ya zanzibar ina uwezo au haina uwezo wa kuufuta muungano huu feki.
 
Huwezi kusema hakuna hati maana inawezekana iko mahali ni muhimu madai yawe kwamba Hati ya Makubaliano ya Muungano yawekwe wazi kwa Umma maana ni haki yao kuijua na kuitambua .
Pili baada ya uwepo wa hati kuwa wazi sasa madai ya kubatilishwa kwa sababu wanazo ona ni za Haki kwa Sasa kuliko wakati ule iliposainiwa yanaweza kuwekwa mbele ya Mahakama!

Hapo kwenye uwekundu nadhani wafanye haraka mchakato wa kuibadilisha ,sioni mahusiano ya Katibu Mkuu wa UN na Makubalianao ya Muungano na kinyume na hapo kesi inaweza kukosa mashiko.

Katibu mkuu wa Un ameingia hapo kwa kosa la kuikubalia tanzania ijiunge na UN na kusajiliwa na katibu huyo na kukifuta kiti cha Zanzibar.

Hivyo kuna umuhimu mkubwa sana ashitakiwe kwani kama walalamikikaji wakishinda kesi basi kiti cha Znz katika UN kitarejeshwa na kile cha tanzania kitafutwa.

Angalia mashitaka hayo kwa jicho la tatu kwani yamekwenda skuli kweli kweli.
 
Sorry!Faiza hivi wewe ni ccm kweli?mbona huwaogopi akina nepi?

CCM ni chama kina chafata misingi ya demokrasia kuliko chama kingine chochote Tanzania.

Usemi wako unaonesha nyinyi mnawaogopa viongozi wenu wa chama.
 
wanaotaka muungano uvunjwe waangalie ni upande upi utaathirika,leo wanzibari wanajifanya wamoja heti wanataka nchi yao,unajua unafiki sio mzur sana mim sidhan kama wazenji ni wamoja hembu wakumbukeni wale wazee wa pemba waloenda UN heti kudai nchi yao mbaya zaidi nchi hiyo sio zanzibar ambayo leo wazanzibari wanataka iwe huru,nchi waloenda kudai ni pemba sasa kwa mazingira haya ni kwel wazanzibari ni wamoja? Na kama ni kwel kwanin wale wazee walienda kudai uhuru wa pemba?,je unguja sio zanzibar?.Mim nadhan hembu tukumbuke maneno ya baba wataifa juu ya muungano wetu mwl alikemea sana ubaguz kama leo wazenji wameanza kuwabagua wabara hakika hiyo dhambi itawatafuna milele,binafsi kama mbara sina hofu ya kufa kwa muungano ila nawaoenea huruma sana ndugu zangu wazenji wanaodanganywa na watu wachache heti muungano hauna faida kwao.HAKIKA ENDAPO MUUNGANO UTAKUFA WAZANZIBARI WATAYAKUMBUKA MANENO YA MWL NYERERE KWAN HAKUTAKUA NA ZANZIBARI HIYO WANAYOITAKA.Mungu ibarik Tanzania mungu ubarik muungano wetu
 
Paul Claud,

Je unajuwa wewe MEMORY CARD ya kule TARIME inayotekelezwa na Makhirikhiri? Yaani Kuuwa vikongwe, kukata na kunyofoa viungo vya albino, Kuchuna ngozi watu na Sasa kule tarime imeanza ya kuuwa wanawake na kuchukua viungo vyao vya Siri kwa tamaa ile ile ya kupata Utajiri.

Waulize NGO ya TWAWEZA watakujuza mengi kuhusu hayo.

Sijazungumzia mgogoro wa kuchinja na MoU ya kanisa na malalamiko ya waislam huko Tz Bara.

hakika tutaona mengi sana nje ya Muungano. Nahisi itameguka kama Suudan kwa misingi ya UDINI, Ukabila.

Pole sana
 
Back
Top Bottom