Huwezi kusema hakuna hati maana inawezekana iko mahali ni muhimu madai yawe kwamba Hati ya Makubaliano ya Muungano yawekwe wazi kwa Umma maana ni haki yao kuijua na kuitambua .
Pili baada ya uwepo wa hati kuwa wazi sasa madai ya kubatilishwa kwa sababu wanazo ona ni za Haki kwa Sasa kuliko wakati ule iliposainiwa yanaweza kuwekwa mbele ya Mahakama!
Hapo kwenye uwekundu nadhani wafanye haraka mchakato wa kuibadilisha ,sioni mahusiano ya Katibu Mkuu wa UN na Makubalianao ya Muungano na kinyume na hapo kesi inaweza kukosa mashiko.
Katibu mkuu wa Un ameingia hapo kwa kosa la kuikubalia tanzania ijiunge na UN na kusajiliwa na katibu huyo na kukifuta kiti cha Zanzibar.
Hivyo kuna umuhimu mkubwa sana ashitakiwe kwani kama walalamikikaji wakishinda kesi basi kiti cha Znz katika UN kitarejeshwa na kile cha tanzania kitafutwa.
Angalia mashitaka hayo kwa jicho la tatu kwani yamekwenda skuli kweli kweli.